Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, October 20, 2010

Zitto anadi gwanda, achangisha 800,000/- papo hapo!



Kampeni za Naibu Katika Mkuu wa CHADEMA Taifa, Zitto kabwe, katika jimbo la Sumbawanga mjini zimeendelea kuiweka pabaya CCM kutokana na kampeni zake kuwachambua kinagaubaga.
Watu zaidi ya 2,000 walifanya maandamano ya furaha kwa kumsindikiza mgombea ubunge wa jimbo hilo Mwalimu Norbert Yasembo. Pia, walitumia mkutano wa kampeni za CHADEMA kumchangia mgombea huyo fedha za kuwalipa mawakala wake kiasi cha shilingi zaidi ya 800,000/- katika harambee iliyoendeshwa na Zitto ambaye pia alijitolea kuchangia kampeni hizo kwa kuuza kombati yake kiasi cha shilingi 200,000/

Akihutubia katika mwendelezo wa mikutano ya kampeni ya CHADEMA mkoani Rukwa katika viwanja vya Rukwa High School jana, mbali ya kukataa kata kata dua za wananchi hao kumwombea kuwa Spika wa bunge lijalo la Muungano wa Tanzania, Kabwe alisema kuwa lazima CCM itambue kuwa hatua ya wananchi kuchangia kiasi hicho cha fedha ni mwisho mbaya kwake na kuwa itegemee kushinda kwa miujiza jimbo hilo.

“Nasema napongeza sana kwa mapokezi haya makubwa ambayo mmeonyesha kwangu na huu ni ushadidi kuwa mgombea wa CCM katika jimbo hili Aesha Hillary si chaguo halisi la wana jimbo la Sumbawanga mjini hivyo si vizuri kwa wachache waliobaki kupoteza kura zao kwa kumpa mgombea ambaye hatakiwi “

Alisema kuwa mkoa wa Rukwa, Kigoma na Tabora ni mikoa ambayo makao makuu yake bado hadi sasa hajaunganisha na lami hali ambayo inahitaji kuwapata wabungemakini watakaoweza kutetea wananchi wa mikoa hiyo kuwa ni sehemu ya wananchi wa mikoa ya Tanzania ambayo kwa sasa imeunganishwa kwa lami .

“Ndugu zangu, Tanzania ni moja na mikoa yote ya Tanzania wananchi wake ni walipaji wakubwa wa kodi, hivyo kitendo cha Serikali ya CCM kuendelea kuwabagua wananchi wa mikoa hiyo ni sawa na kuwaona kuwa hawafai kupewa huduma hiyo na dawa pekee ni wananchi wa mikoa hiyo kuunga na kuwanyima kura wagombea ubunge wa CCM na kuwapa wale wa CHADEMA ambao kupitia Rais mpya wa awamu ya tano kwa Tanzania Dk Wilbrod Slaa, wananchi wa mikoa hiyo wanapewa haki yao ya lami”

Kabwe alisema kuwa wananchi wa Tabora, Kigoma na Rukwa wasipokubali kuunganisha nguvu zao katika kuchagua wabunge wa CHADEMA, bado CCM itaendelea kuwafanya kuonekana kuwa wanyonge. Aliongeza kuwa, katika mkoa wa Kigoma kwa bunge lililopita mbunge wa upinzani alikuwa ni mmoja pekee huku katika mkoa wa Rukwa pia kulikuwa na mbunge moja hivyo ni vizuri Oktoba 31 wakaongeza idadi zaidi ili kuwe na idadi kubwa ya wabunge.

Hata hivyo, alisema kuwa kwa upande wake hana tatizo la jimboni kwake kwani tayari ameshinda na anasubiri kuapishwa na Rais wake Dk Slaa.

Katika hatua nyingine, Kabwe ameshangawa na hatua ya ulinzi mkali aliowekewa katika jimbo hilo la Sumbawanga mjini ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha askari polisi, askari magereza, pamoja na mgambo kufika kulinda mkutano jambo ambalo hajapata kuona askari magereza wakifika katika mikutano ya kampeni kama jimbo hilo la Sumbawanga mjini na kuwa yawezekana katika mkutano wake huo, wafungwa pia wamefunguliwa ili kujakusikiliza sera za CHADEMA.

Katika mkutano huo uliomalizaka kabla ya muda wa kampeni kuisha, wananchi walifanya maandamano makubwa huku biashara zao zikisimama kwa muda kwa ajili ya kusukuma gari la Zitto Kabwe pamoja na ile ya mgombea ubunge wa CHADEMA huku wakiimba kuwa wanataka mbunge Msomi wa CHADEMA sio CCM. Hatua hiyo ilionyesha kuwapa wakati mgumu askari polisi magereza na wale wa jeshi la polisi nchini kuwatuliza wananchi hao na kuwaomba viongozi wa CHADEMA kuwatuliza na kuwatawanya wananchi hao zaidi ya 2,000 kabla ya mgombea ubunge wa CHADEMA kuamua kuwatoroka viongozi wenzake ofisini ili waandamanaji hao watawanyike.

from: http://www.wavuti.com/4/post/2010/10/zitto-anadi-gwanda-mkutanoni-achangisha-800000-papo.html#ixzz12sZxXuaZ

MWANAFUNZI CHUO AVUTA MSHIKO WA SUPER



Huku droo ya Supa Pesa ikiendelea kutoa mamilioni kwa washindi wake kupitia bahati nasibu inayochezeshwa nchini kote, wikiendi iliyopita imemkuta mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma,tawi la Mwanza, Catherine Nyamoni, akibahatika kujinyakulia kiasi cha milioni moja fedha taslimu.Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 23, alisema,’ Kweli mimi nilikuwa kati ya watu ambao sitilii maanani michezo ya bahati nasibu wala kuwahi kushiriki kati shindano lolote maishani mwangu. Lakini wiki chache zilizopita nilipokuwa nasikiliza redio nyumbani, nilipata nafasi ya kumsikiliza mshindi wa milioni kumi akipigiwa simu kujulishwa kuhusu ushindi wake.
Basi pale ndipo nilipata hamasa kubwa na kuamua kutopitwa na nafasi ya kujaribu bahati yangu. Nilishiriki kwa kutuma ujumbe mfupi kama walivyoelekeza na baada ya kujaribu mara kadhaa nimepata ushindi. Namshukuru Mungu nimefanikiwa na kupata ushindi.’Catherine aliongezea kusema, ‘ Nitatumia hela za ushindi kuendeleza masomo yangu kwa kununua kompyuta itakayonisaidia kufanya kazi chuoni kwa ustadi zaidi na vilevile hela itakayobaki ninatarajia kutumia kama mtaji wa kuanzisha biashara ndogo ili kujipatia kipato cha kila siku.Kushiriki droo ya Supa Pesa ni rahisi, inahitaji kutuma ujumbe mfupi wenye neno SUPA kwenda namba 15777. Hii inakuwezesha wewe kuingia moja kwa moja kwenye ushindani wa shilingi milioni moja kila sikui na ukishiriki kutuma Ujumbe mfupi wa simu zaidi ya mara nne basi utakuwa kati ya washindani wa milioni kumi kila wiki.

Tuesday, October 12, 2010

JK Akiwa Mbinga







1. Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mtoto mlemavu Maria Chiwinga muda
mfupi baada ya kuwasili mjini Mbinga jana ambapo aliwahutubia wananchi
katika mkutano mkubwa wa kampeni.Dr.Kikwete aliahidi kumpatia mlemavu
huyo msaada ili aweze kuendelea vyema na masomo yake.

2.Wananchi wa mji wa Mbinga wakimkaribisha kwa ngoma mgombea
urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili mjini
hapo na kufanya mkutano mkubwa wa kampeni.

3. Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi mgombea ubunge jimbo
la Peramiho Jenister Mhagama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika
katika kata mpya ya Mtyangimbole, jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma jana

KIFAAA KINATAFUTA BWANAAAAA


mrembo ni Miss Temeke 2003/04, anaitwa Mariam Omary ambaye by now ni mkufunzi wa mashindano ya urembo hapa Bongo.
Huyu mto bana, amekaa chini na ku-discuss baadhi ya mwenendo wa life na kugudua kuwa anamisi kitu kimoja tu muhimu, yaani mwanaume.
So Mariam ni mtoto wa jijini pande za Mangomeni Morocco, ana age ya miaka 24, muonekano wake kiukweli mtoto ana shepu ya ki-miss na kwamba amelelewa katika mazingira sahihi ya Kitanzania. Hivyo basi, anatafuta mchumba mwenye umri wa kuanzia miaka 28 kuendelea mwenye sifa zifuatazo:
Mfanyakazi wa serikali au kampuni yoyote binafsi.
Awe na akili timamu.
Awe na Elimu ya kutosha.
Awe na uwezo wa kutunza familia na siyo Mariooo.
Awe tayari kupima ngoma.
Are you ready? Na je, una sifa zote hizo? Fanya fasta, mcheki kwa namba 0652-018355