Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, July 28, 2010

MAMBO HADHARANI KAMA KAWAIDA

wapendwa wa blog yenu ya umbea.com inawaomba radhi wadau wake wote kwa kipindi chote tulichokuwa hutuwapi yale yanayojiri kona zote za dunia hii nikutokana na kijana wenu kuwa sehemu ambayo haikuwa na net hivyo basi kuanzia jmosi ya week ijayo yaani tarehe 07\08\2010 mambo yataanza tena kama kawaida wadau wetu.KARIBUNI SANA

Monday, July 5, 2010

waliokuwa katika moto wazikwa congo!


Miili ya watu waliofariki baada ya mlipuko wa trela iliyokuwa imebeba mafuta kuanzisha moto mkubwa katika kijiji kimoja Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imezikwa leo katika makaburi mawili makubwa.
Watu wasiopungua 230 walikufa walikufa baada ya trela hiyo kupinduka na kulipuka, na moto mkubwa kutokea katika kijiji cha Sange.
Baadhi ya wale waliokufa ni watu waliokuwa wakichota mafuta. Lakini wengine waliteketea walipojipata katika mtego, wasiweze kutoka katika majumba, ikiwa ni pamoja na ukumbi mmoja wa filamu ulioshika moto.
Wanajeshi wa kudumisha amani wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa mashirika ya misaada, wamekuwa wakijaribu kuwasaidia waliojeruhiwa katika moto huo.
Kulingana na shirika la habari la Associated Press, siku ya Jumamosi wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu waliibeba miili katika mifuko ya plastiki, hadi katika makaburi mawili makubwa, nje kidogo ya kijiji cha Sange.
Jean-Claude Kibala, gavana wa Kivu ya Kusini, amesema yaliyotokea katika kijiji hicho ni mambo ya kutisha.
"Kuna miili kila mahali barabarani. Wakaazi wote wamo katika hali ya mshituko, hakuna aliye katika hali ya kulia wala kuzungumza kuhusu mkasa huo." Ajali hiyo ilitokea usiku wa Ijumaa.
Kijiji cha Sange kipo mwendo wa kilomita 70 kusini mwa mji wa Bukavu, katika Kivu ya Kusini, karibu na mpaka wa Burundi.
www.bbcswahili.com

toyota vx amazoni pichani inauzwa.



Toyota vx amazoni
Miles 43,000.
Mawasiliano zadi piga no:
0713300997 AU 0784298156

WIMBI la askari wa Jeshi la Polisi kujiua, limeendelea kushika kasi baada ya askari wa kike WP Suzana, aliyekuwa amepangiwa kuzuia magari ili msafara



Marafiki a.k.a Mashosti Wapendwa wa Da'Zena wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja leo jioni maeneo ya Sinza,jijini Dar walipokwenda kumpa hongera ya kujaaliwa kupata mtoto wa kike aitwaye Fatina.Kutoka kushoto ni Anti Mwanjaa a.k.a Mwanji,Da' Hanifa Mati a.k.a Hanifa Bonge pamoja na Da' Fatma Kasim a.k.a Fatma Kili.

Da' Zena akipewa hongera na zawadi tele kutoka Mama mdogo aitwaye Salma Kili na kupata picha ya ukumbusho kwa pamoja.

Polisi ajipiga risasi nne kituoni

WIMBI la askari wa Jeshi la Polisi kujiua, limeendelea kushika kasi baada ya askari wa kike WP Suzana, aliyekuwa amepangiwa kuzuia magari ili msafara wa Rais Jakaya Kikwete upite wilayani Tarime mkoani Mara kujiua.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, Sebastan Zakari alisema, Suzana alijiua majira ya saa 7.05 mchana ndani ya kituo cha polisi.

“Mimi niko kwenye msafara wa Rais, ni kweli nimepata taarifa kwamba kuna askari wetu wa kike amejiua, baada ya kutoka kwenye eneo lake (pointi), tuliyokuwa tumempangia baada ya msafara wa Rais kupita… sijajua chanzo gani kilichomsibu,” alisema Kamanda Zakaria.

Habari zilizopatikana kutoka Tarime zinasema WP Susana, baada ya kukosea kuelekeza msafara huo, alifuatwa na maafisa usalama wa taifa, ambao walimfokea kisha kuamuru akamatwe na kupelekwa mahabusu kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Chanzo hicho, kinasema kitendo hicho, kilionekana kumkera na kuamua kuchukua bunduki na kujipiga risasi nne kifuani.

Watu walioshududia tuko hilo, walisema askari huyo alikosea kuelekeza magari ya kwanza yaliyokuwa kwenye msafara, ambayo yalitakiwa kwenda eneo la Bomani ambako Rais alitakwenda ili asome taarifa ya wilaya.

Ilidaiwa baada ya kukosea, ndipo alipokamatwa na wenzake kisha kupelekwa kituo kikuu cha polisi Tarime, na kwamba huko alipewa vitisho na wakubwa wake wa kazi kutokana na kosa hilo.

Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Charles Samson, alithibitisha kupokea mwili wa askari huyo na kueleza kuwa alijipiga maeneo ya kifuani na risasi kutokea mgongoni upande wa kushoto ambako ni eneo la moyo.

Tukio ni la pili, kutoka baada ya juzi asubuhi askari polisi ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Tanzania Polisi Academy, Konstebo Nole Paul Njega, kujipiga risasi na kufumua kichwa chake chote, mjini Dar es Salaam. Habari zaidi bofya Hapa