Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, April 30, 2010

Mr Nice, Eti ni kweli Umefilisika??


Mmoja wa wanamuziki waliowahi kutesa sana na kutengeneza hela kwa hali ya juu Bongo Lucas Mkenda a.k.a Mr Nice ameibuka na kujibu tuhuma za kuambiwa kuwa amefilisika

“Mimi sijafulia bado niko juu kisanaa na muziki wangu haujachuja hata siku moja, hivyo watu wanaodai nimefulia pengine hawafahamu mipango yangu,” alianza kwa kujitetea alipokuwa anazungumza na Dar41.

“Hili suala la kufulia,limetoka wapi na nini maana ya mtu kufulia sioni sababu ya watu kusema nimefulia, sijafulia hao wanaosema hivyo wanasababu zao.”

“Huwezi kusema kuwa nimefulia kimuziki ama kifedha wakati aina ya muziki wangu hakuna mtu anaweza kuiga wala kuifanya bado niko mwenyewe na matoleo niliyoyatoa bado yanafanya vizuri sokoni.

“Kama kukaa kimya bila kutoa albamu mpya au kupanda jukwaani ama kutonyesha uwezo wako kifedha ndiyo maana ya kufulia basi mimi sijafulia tena niko juu zaidi.”

“Kuna watu waliofulia tunawafahamu na hatuwezi kuwasema walianza muziki kwa mbwembwe na baadaye wakakwama ghafla na hii ilitokana na kubebwa bebwa tu na baadhi ya watu kwa sababu ya faida za wachache lakini sio kweli kwamba wanauwezo mkubwa kisanaa.

“Baada ya kutoa visingo vyao ama albam zao za kuunga unga wakajiona masikio yanazidi kichwa na walipo achwa ili waonyeshe uwezo wao wenyewe wakashindwa hao ndiyo waliofulia sio mimi bwana mi niko juu sana.

“Ingawa kila msanii ana mipango yake kuhusu muziki ila mimi mipango yangu ni ya kimataifa zaidi na kamwe mtu hawezi kufahamu ninachofikiria katika suala zima la muziki ndiyo maana baadhi ya watu wanajaribu kutafuta maneno ya kusema juu yangu lakini ukweli ni kwamba mimi ni zaidi ya wanavyofikiria.”

“Ingawa ni vigumu kukataza watu wasiseme yale wanachofikiria lakini masuala mengine yanakera kuona mtu anasema mambo asiyokuwa na uhakika nayo. Kuthibitisha ninayoyasema nimepanua kazi yangu zaidi katika majukwaa ya kimataifa na hivi karibuni hilo litakuwa wazi.

“Mimi muziki kwangu ni kazi na ndiyo ajira yangu hivyo ni lazima niwe na malengo makubwa ili ninufaike katika maisha yangu yote kwa sababu nimebaini kuwa ni kazi pekee inayonifaa na kunipa mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi.

Vyandarua Vyageuzwa kuwa Net za Kuvulia Samaki!


Wakati Serikali na mashirika mbalimbali wakihangaika kugawa vyandarua kudhibiti ugonjwa wa malaria unaoua zaidi nchini, Wananchi wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara wamebadili kazi ya vyandarua kuwa vifaa vya kuvulia samaki badala ya kujikinga na mbu.
Akielezea kisa hicho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mhe. Jesse Mlaki amesema jitihada kubwa zimefanyika kuleta maendeleo makubwa ya kukabili ugonjwa wa malaria wilayani humo, lakini cha kusikitisha baadhi ya wakazi wamehujumu juhudi hizo.

Amesema kuna mafanikio makubwa yanayotokana na elimu ya kujikinga na maambukizi ikiwa ni sambamba na ugawaji wa vifaa kama vyandarua ambapo familia nyingi zimepata vifaa hivyo.

Aidha mkurugenzi huyo amewataka wakazi wake kutambua hatari ya ugonjwa huo nchini na kujitahidi kuwakinga wanawake na watoto wachanga wanaogeuka wahanga wa ugonjwa huo kutokana na maambukizi ya mbu.

Wahadhiri UDSM waanza mgomo!



Wakufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wameanza mgomo wa kutoingia madarasani kufundisha ili kuishinikiza Serikali kuwalipa na kuboresha mafao yao ya kazi.
Akielezea uamuzi huo kwa vyombo vya Habari leo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wahadhiri chuoni hapo Damas Nyaoro amesema kimsingi Wahadhiri wastaafu wanataabika kwa kutolipwa mafao yao kwa muda mrefu na wengine kupewa malipo madogo yasiyolingana na vigezo vya taaluma.

Amesema suala hilo la kuboreshewa mafao yao limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu na Serikali haijachukua hatua yoyote jambo linalozidi kuzorotesha hali ya Wahadhiri hao kimaisha.

Hatua hiyo ya Wahadhiri UDSM imechukuliwa katika wakati ambao Serikali inahaha kuzima mgomo mkuu wa Wafanyakazi wote ulioitishwa kufanyika siku chache zijazo mwanzoni mwa mwezi ujao.

power breakfast live kutoka kempinski


Kutoka kulia ni Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini Dr Kafumu,Muongozaji wa Kipindi Sebastian Maganga,Barbra Hassan,Paul James pamoja na Gerald Hando wakiwa Live asubuhi ndani ya hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk.

Fundi Mitambo mahiri wa Clouds FM Bwana Jakson akihakikisha kipindi cha Power Breakfast kinakwenda live bila matatizo asubuhi hii

Clouds Fm 88.4 kupitia kipindi chake cha Power Breakfast wakizungumza Live sasa hivi katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk (Frame tree Lounge) na Kamishna wa madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Dr.D.P Kafumu ,kuhusiana na masuala mbalimbali yahusuyo sekta ya madini ikiwemo na sheria yetu mpya ya madini ambayo baadhi ya watu wamekuwa na walakini nayo

MAMBO YA MATANGAZO HAyo!


Hahaha kwa wadau wote sio ya kukosa hii kazi kwenu!

Thursday, April 29, 2010

Aomba Kupelekwa Rumande kwa kukosa elfu kumi ya faini!


Mkazi wa Magomeni jijini Dar es salaam, Juma Said, 35, ameieleza Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo kuwa ni heri aende jela kutumika kifungo cha miezi sita alichohukumiwa kutokana na kukosa Sh10,000 za kulipia faini.

Said alieleza hayo ijumaa wakati Hakimu Mwajuma Diwani kumuhukumu kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini ya Sh 10,000 baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kete moja ya bangi.

Hakimu Diwani alitoa hukumu hiyo ya kifungo baada ya mtuhumiwa huyo, aliyekuwa amefikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, kukiri kosa lake.

Wakati hukumu hiyo ikitolewa mara baada ya mshtakiwa huyo kukubali shitaka, Hakimu Diwani alisema kuwa Said hakutaka kuisumbua mahakama hivyo aliamuru alipe faini ya Sh 10,000 au kifungo cha miezi sita jela.

Hakimu huyo alimuuliza mshtakiwa huyo kama anacho kiasi hicho cha fedha alichotakiwa kulipa faini.

"Mama mimi sina hela hiyo ya kulipa ni bora niende gerazani," alisema Said ambaye sasa ataigharimu serikali angalau Sh270,000 za chakula kwa siku 180 atakazokuwa jela iwapo atagharimiwa Sh1,500 kwa mlo mmoja kwa siku.
Jibu hilo lilimfanya hakimu huyo aamuru akatumikie adhabu hiyo ya kifungo cha miezi sita jela.

Said alidaiwa mahakamani hapo kuwa Aprili 21, mwaka huu katika eneo la Upanga wilayani Ilala alikamatwa na ofisa wa polisi wa kituo cha Salender Bridge, Koplo Eustace akiwa na kete moja ya bangi wakati akijua kuwa hilo ni kosa la jinai.

Trafiki sasa kumwaga kadi kama Marefa Wa soka!!


Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dsm, imeanzisha mtindo wa kutoa kadi ya njano na nyekundu kama ilivyo kwa mchezo wa soka, kwa madereva wa daladala ikiwa ni njia ya kudhibiti uvunjaji wa sheria za barabarani.

Hadi sasa tayari madereva 70 wamepewa kadi za njano na wengine wanane wamepewa nyekundu ambapo wamenyang’anywa leseni zao kutokana na makosa hayo.

Hayo yalisemwa jana Dsm na Kamanda wa kikosi hicho cha usalama wa barabarani, Mohammed Mpinga.

“Tunatumia mtindo wa ‘yellow card’ na tayari tumeshazitoa kwa madereva 70 na wengine wanane tumewapa ‘red card’ hii ni katika kudhibiti vitendo vya kuvunja sheria za barabarani,” alisema Mpinga.

Pamoja na hayo, alikanusha madai ya madereva kuwa wakikamatwa kwa makosa ya barabarani hupelekwa moja kwa moja lupango kwa wiki mbili.

“Tunafuata sheria, akikamatwa dereva taratibu zipo za dhamana na hata akifikishwa mahakamani dhamana huwa wazi isipokuwa kwa wale ambao mahakama itakosa uaminifu kwao.”

Alisema hadi sasa madereva 21 wana kesi mahakamani na wengine 18 wamefungwa jela kwa muda wa miezi mitatu hadi sita kutokana na kuvunja sheria za barabarani ambazo ni kukatisha ruti na kutanua njia.

Kwa mujibu wa Mpinga, Polisi imejipanga kuhakikisha kuwa inadhibiti makosa ya barabarani na iko kwenye mchakato wa kuwa na kamera aina ya CCTV Dar es Salaam na barabara zote za mikoani.

“Kamera hizi zitasaidia sana kuona makosa ambayo kwa sasa tunashindwa kuyaona, hata ajali ikitokea mikoani kupitia kamera hizi tutakuwa na uwezo wa kurudisha mkanda nyuma na kuona tukio zima na hivyo kujua chanzo cha ajali hiyo bila shida,” alisema.

Wednesday, April 28, 2010

Niliowamwaga Kundini Ni Wavivu!


King wa Miondoko ya Kwaito Bongo, Juma Kassim Kiroboto a.k.a Nature ambaye juzikati aliwapa shiti washkaji zake waliokuwa wakiunda Crew ya Wanaume TMK Halisi, amewadisi jamaa hao aliowaacha yatima baada ya kula mkataba na Kampuni ya DLC ya nchini China.
Nature aliwachana jamaa hao alipokuwa akigonga interview na stesheni moja ya redio jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo mtu mzima alieleza chanzo cha kuwatosa kwenye shavu hilo.
“Tumewaacha kwa sababu ni wavivu wa kuandika na pia tulijua mwishoni watajiondoa wenyewe kundini. TMK Halisi hii mpya ni kazi kwa kwenda mbele, hatutaki tena watuma meseji,” alisema Nature bila kufafanua ni meseji za aina gani.

Wasanii wanaoendelea kuwakilisha TMK Halisi na Nature ni pamoja na Dolo, Baba Levo, JB wa Mabaga Fresh na KG Son. Waliotoswa ni Luteni Kalama, Mzimu, Malipo, D Chief, Bob Q, BK na Richie One ambaye alikuwa ni mshkaji wa karibu wa Nature.

Malaria yamdondosha Mfalme Sele


Mkali wa Rhymes Bongo, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ juzi Sunday ya Aprili 25,alipiga chini (alianguka) na kupoteza fahamu jukwaani wakati akipafomu kwenye tamasha la siku ya Malaria duniani, event ambayo ilifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Habari za kuaminika zinaeleza kuwa Mfalme Sele alikuwa akisumbuliwa na Malaria kali, na alikuwa amelazwa Hospitali, ila kwa kuwa alikuwa ameshalamba ‘mkwanja’ akalazimika kuhudhuria huku akiwa mgonjwa.
Ilikuwa ni kama muvi kali kwani sherehe zilikuwa ni za maadhimisho ya siku ya Malaria duniani, na Prezidaa alikuwa akiwahimiza Watanzania kujikinga na ugonjwa huo hatari, huku wasanii, akiwemo Afande Sele wakisaidia kuufikisha ujumbe kwa walengwa, kumbe tayari adui malaria alikuwa ndani ya mwili wa Afande. Mkali huyo wa Rhymes ambaye awali alikuwa amelazwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu, alipanda jukwani kwa kujikongoja.
Baada ya kudondoka, Mfalme Sele kwa msaada wa mabaunsa na wasanii wenzake akiwemo Joseph Haule ‘Profesa Jay,’ alikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala alikolazwa kwa mara ya pili na kuendelea kupata tiba ya uhakika ya malaria.

noriega Arudishwa Ufaransa


Aliyekuwa kiongozi wa Panama, Manuel Noriega, amesafirishwa hadi Ufaransa, baada ya kufungwa kwa zaidi ya miaka 20 jela nchini Marekani.

Waziri wa mashauri ya nje wa Marekani, Hillary Clinton, alitia saini waranti ya "kusalimu amri", baada ya kutokuwepo tena vipingamizi vya kisheria kumzuia nchini Marekani.

Noriega, pasipo kuwepo mahakamani, alihukumiwa nchini Ufaransa mwaka 1999, kutokana na ulanguzi wa fedha, na kuna uwezekano pia wa kufunguliwa kesi mpya.

Noriega sasa anatazamiwa kufikishwa mbele ya maafisa wa mashtaka, ambao watamjulisha kuhusu waranti iliyotolewa ya kumkamata.

Tuesday, April 27, 2010

Miaka 46 ya Uhuru Yaadhimishwa!!







Omar Al Bashir Kutangazwa mshindi??


Matokeo ya kwanza kufuatia uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi katika kipindi cha miaka 24 yanatazamiwa kutangazwa leo nchini Sudan.
Mwandishi wa BBC mjini Khartoum anasema Rais Omar al Bashir anatazamiwa kutangazwa mshindi.
Salva Kiir, aliyekuwa kiongozi wa waasi wa kusini, SPLM, ametangazwa mshindi, kama rais wa serikali ya kusini, ambayo kwa kiasi fulani ina madaraka ya uongozi.

Uchaguzi katika sehemu zote ulikuwa na malalamiko mengi ya udanganyifu, na pia vitisho kwa wagombea, huku wasimamizi wa kimataifa nao wakisema kwamba viwango vya uchaguzi huo kamwe havikubaliki.

Monday, April 26, 2010

ANATUA BONGO MAY 15


Haya sasa wazee wa burudani jamaa anatarajiwa kutua bongo tarehe 15 may na atatoa burudani katika kumbi mbalimbali hapa bongow

Dominic Mwita Hatunaye Tena!


Hayati Dominic Mwita.

Chumba cha habari cha Daily News na HabariLeo kimeghubikwa na majonzi kufuatia habari ya kifo cha Dominic Mwita (32), aliyewahi kuwa mwandishi wa habari kwenye makampuni hayo kabla ya kuhamia kitengo cha habari cha UNICEF jijini Dar.

Kifo chake kimesababishwa na ajali ya barabarani siku ya Ijumaa usiku wakati marehemu aliyekuwa anatoka harusini na gari yake aina ya RAV4 aliingia kwa nyuma semi-trela lenye namba T632 AGH lililokuwa limesimamishwa katikati ya barabara kiasi cha mita 100 hivi toka daraja la Mbezi Beach jijini Dar.

Kamanda wa polisi wa Kinondoni Elias Kalinga amethibitisha kutokea ajali hiyo na kusema uchunguzi unaendelea. Aliongezea kusema tela hilo lilisimamishwa katikati ya barabara bila wenyewe kuweka tahadhari ya traiengo ama ala ingine kwa watumia barabara wengine.

Msiba uko nyumbani kwa shemeji wa marehemu, Bw. Fred Mwita, huko Mbezi Makonde ambako mipango yote ya mazishi inafanyika.

Marehemu Dominic, ambaye amewahi kufanya kazi Posta na Nyanza bottling huko Mwanza, amefanya kazi Daily News kati ya mwaka 2003 na 2005 kabla ya kuhamia UNICEF.

Mola aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu

AMEN

Source www.issamichuzi.blogspot.com

TAARIFA MUHIMU KWA VYOMBO VYA HABARI!!



Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika.

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kuratibu Silaha ndogondogo hapa nchini, Jumanne Aprili 27, 2010 saa 2.00 asubuhi itakutana ili kupitia maazimio ya mapendekezo ya mshwaada wa kurekebishaji sheria za kumiliki silaha hapa nchini.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema kuwa Mkutano huo ambao utafanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kuanzia saa 2.00 asubuhi, utawashirikisha baadhi ya Maafisa wa Wizara na Idara za Serikili zinazojihusisha na masuala ya kiusalama pamoja na baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai utafunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Lawrence Masha.

Kutokana na umuhimu na uzito wa masuala yatakayozungumziwa siku hiyo, Wahariri mnaombwa kutuma waandishi na wapiga Picha kwa ajili tukio hilo.

Saturday, April 24, 2010

MOTO WAZUA KIZAAZAA BENKI YA NMB TAWI LA BANK HOUSE!!


Moshi uliozusha hofu kwa wateja na wafanyakazi wa banki ya NMB tawi la Bank House lililopo mtaa wa Samora, baada ya moto kulipuka katika benki hiyo , haikufahamika mara moja chanzo cha moto lakini upande uliolipuka moto ndiyo eneo lililokuwa likitumika mwanzo na benki hiyo kutoa huduma kwa wateja, hivi karibuni upande huo ulifungwa na wateja walihamiswa na kuendelea kupata huduma ghorofa ya tatu.
Upande huo unafanyiwa ukarabati na mafundi kitu ambacho kinasadikiwa kuwa huenda ndiyo chanzo cha moto huo katika benki hiyo, nilikuwepo katika benki hiyo nikipata huduma na nilipomaliza nilishuka chini, nilipofika kwa walinzi wa benki hiyo nikasikia wakisema kuna moto unawaka, mara nikasikia king'ora kikilia.
Walinzi walitoa taarifa kwa uongozi ndipo watu wakaaza kukimbia hovyo huku moshi ukiendelea kusaambaa katika jengo hilo, hata hivyo wafanyakazi wa kampuni inayofanya kazi ya kukarabati jengo hilo walijaribu kuudhibiti moto huo na kufanikiwa kwa kiasi fulani kabla ya kikosi cha Zimamoto waliokuwa wamechelewa sana kufika eneo la tukio na kuchukua hatua za kuuzima

Rais Wa Iran Atua Uganda!


Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, amewasili nchini Uganda, ambako suala la mpango wa nuclear la Teheran linatarajiwa kuwa agenda kubwa katika mazungumzo yake na Rais Museveni.

Kwa hivi sasa Uganda ni mwanachama katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Siku ya Ijumaa, katika siku yake ya pili ya ziara nchini Zimbabwe, Bw Ahmadinejad aliyashtumu mataifa ya magharibi kwa kujaribu kuangamiza uchumi wa Iran na Zimbabwe.

Akifungua maonyesho ya biashara mjini Bulawayo, Bw Ahmadinejad alisema nchi hizo mbili zilipitia wakati mgumu wa kuingiliwa kati na mataifa hayo ya magharibi.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameunga mkono mpango wa nuclear wa Iran.

Madini ya Vito Sasa Kuchimbwa na Wazalendo tu!!


Mswada wa Sheria ya Madini wa mwaka 2010 unaoendelea kujadiliwa Bungeni, umeweka kipengele kinachodhibiti uchimbaji wa madini ya vito kufanywa na Wantanzania peke yao.
Akichangia hoja hiyo miongoni mwa Wabunge wengine, Mbunge wa viti maalumu Bungeni kupitia CHADEMA Halima James Mdee, amesema madini hayo kama Tanzanite ya Mererani, safaya na mengine, hayahitaji nguvu ya teknolojia kubwa kutoka nje.

Amesema wenyeji wanaweza kutekeleza jukumu hilo hadi kuinua pato la Taifa iwapo watawezeshwa kwa kupelekewa viwanda, kuandaliwa soko na vifaa vingine pia kupewa miongozo na usimamizi thabiti.

Kadhalika sheria hiyo itatoa fursa ya ushirikiano baina ya wenyeji na wageni kutoka nje pale itakapobidi kwa makubaliano maalumu yatakayoridhiwa na pande zote mbili na kwa maslahi yanayotambulika kwa uwazi.

Aidha madini mengine kama Uranium, Copper, plutonium, mafuta na mengine yenye kuhitaji usimamizi mkubwa Serikali kutokana na umuhimu wake yatabakia kuwa chini ya uangalizi wa Serikali kama mdau mkuu na kupewa wawekezaji kwa mikataba ya wazi na Serikali.

Friday, April 23, 2010

Kimwana Manywele msagaji?


Kimwana Manywele namba (2) 2006-07, Husna Idd ‘Sajent’ hivi karibuni aliwashangaza wageni waalikwa katika sherehe ya kuzaliwa kwa Malkia wa Ngwasuma, Ketula Kihongosi pale alipowaacha watu wakisherehekea pati hiyo na kushughulika na vitendo vya kisagaji kwenye mwili wa mlengwa.

Kimwana huyo alionekana akichezea matiti ya mwenzake sambamba na kulishana keki kwa kutumia mdomo hadharani kitendo kilichowashtua wageni hao na kubaki wakijiuliza kulikoni Kimwana Manywele amekuwa na tabia za kisagaji?

Pamoja na watu kufurika katika sherehe hiyo iliyokuwa maalum kwa ajili ya kumpongeza malkia kwa kutimiza miaka kadhaa, Husna hakuwaogopa, alichukua muda mwingi kukaa karibu na aliyekuwa akisherehekewa na kuanza kumpapasa papasa na kumfanyia vitendo vya kisagaji huku picha zikichukuliwa na wanawake wengine wakimshangaa.

“Hivi kimwana siku hizi amekuwa msagaji? Ona anavyochezea kifua cha mwenzake, angalia alivyoshika matiti kama vile anamchezea mpenzi wake, huu si usagaji jamani?” Alisikika dada mmoja ambaye naye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa.

Aidha, kitendo cha Husna ‘Sajenti’ kuchukua muda mrefu na kutawala kwenye sherehe hiyo akionesha mapenzi makubwa kwa msichana mwenzake, kiliwashangaza wengi wakiwemo akina kaka waliokuwa karibu na malkia huku wakihoji kulikoni.

“Huenda hawa mabinti ni wasagaji, kwanini kila kona Sajent anakaa na malkia na hampi nafasi ya kuchati na wageni wengine… angalia kila mara anampiga mabusu,mh emu ninyamaze miye mambo haya ya mjini zaidi,” alisema kaka mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Issa.
Hata hivyo, mara baada ya sherehe hizo na wageni waalikwa wote kuondoka ‘Sajent’ alibaki ameganda hali iliyomfanya mwandishi wetu kumhoji.

Alipoulizwa sababu ya kutoondoka na kwanini alikuwa akifanya naye mambo yaliyotafsiriwa na watu kuwa ni ya kisagaji alijibu: “Hiki ndiyo kinakushangaza? Huyu ni rafiki yangu wa karibu sana hayo mambo ya kisagaji mimi sina na wala sijawahi kufikiria, ni tabia ambayo siipendi kabisa.
CHANZO GLOBALPUBLISHERS

UNGEKUWA WEWE UNGEENDESHA JE!!!!!


USAFIRI KAFIRI: kutokana na shida ya usafiri, watu wanalazimika kubeba mizigo yao katika mazingira ya hatari kama mkazi huyu wa Morogoro alivyonaswa na mpiga picha wetu mkoani humo jana. Baiskeli yake ina kitako, lakini kaamua kubeba tenga lake kichwani na kuendesha baiskeli kwa mkono mmoja...ungekuwa wewe ungeendeshaje na ukawa salama in case ikitokea rabsha kwenye road?

Mbunge Kimaro apatwa na kiharusi



MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), amepatwa na kiharusi akiwa bungeni mjini Dodoma na amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Spika wa Bunge, Samuel Sitta pamoja na uongozi wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma, wamethibitisha kuugua kwa mbunge huyo maarufu miongoni mwa kundi lililojipambanua kuwa linapambana na ufisadi.

Akizungumza jana jioni bungeni, Sitta alisema Kimaro alikuwa anajisikia vibaya tangu juzi na hivyo kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa Muhimbili jana.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Philemon Saigodi alisema Kimaro alifikishwa hospitalini hapo juzi usiku na Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM).

Dk. Saigodi, alisema kwa mujibu wa Kimaro, alipatwa na matatizo kwa kuishiwa na nguvu ghafla katika mkono wake wa kulia na mguu wakati akipata chakula cha usiku.

“Alisema wakati anakula usiku, aliishiwa nguvu mkono wa kulia na mguu wa kulia, hivyo akaletwa hospitali,” alisema Dk. Saigodi na kuongeza:

“Baada ya kumpokea, nilimwita daktari bingwa wa viungo, Dk. Chaula na kumchunguza na kugundua kuwa ana tatizo kubwa zaidi na anahitaji kulazwa. Hivyo akalazwa wodi ya Daraja la Kwanza.”

Aidha, Dk. Saigodi alisema licha ya uchunguzi kubaini kuwa ana tatizo kubwa zaidi, pia waligundua kuwa mapigo ya moyo yalikuwa juu ya kiwango cha kawaida.

Alisema kutokana na hali hiyo, jana asubuhi, mbunge huyo kutoka mkoani Kilimanjaro, ilibidi asafirishwe kwa gari la wagonjwa la Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kupelekwa Muhimbili.

Alisema msafara huo uliondoka jana saa 12 asubuhi ukiwa na wauguzi kadhaa wa hospitali hiyo ili kupelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Dk. Saigodi alisema uchunguzi huo utahusisha kuangalia athari za kiharusi hicho pamoja na tatizo kubwa wanaloliona ikiwamo uchunguzi wa kichwa chake.

Kimaro aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na katika siku za karibuni, amekuwa akisikika kuwa miongoni mwa baadhi ya wabunge wa CCM wanaopamba na ufisadi.

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, aliyetangaza nia ya kuwania Jimbo la Vunjo katika Uchaguzi Mkuu ujao, alimpa pole na kumwombea apate nafuu ya haraka mbunge huyo.

Lakini aliongeza kuwa “mimi wakati nikienda kutibiwa India, Kimaro aliwakusanya watu Vunjo na kueleza kwamba sitarudi, napenda ajue kuwa kila mtu ni mgonjwa mtarajiwa …namwombea apone tupambane Vunjo.”

MAJAMBAZI SUGU 18 MBARONI!!!


Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman H. Kova akionyesha waaandishi wa habari Ofisini kwake leo Silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi kwa msako maalum pamoja na kutaja orodha ya majambazi yaliyotiwa nguvuni na jeshi la polisi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata majambazi sugu 18 , kufuatia uchunguzi wa kikachelo wa muda mrefu kwa makosa ya mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha,ubakaji, uvunjaji wa migahawa na wizi wa kutumia nguvu.

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema ya jana asubuhi Kamanda wa jeshi hilo, Suleimani Kova alisema kati ya majambazi hao watano walikamatwa na silaha 3 ambazo ni bastola 2 na bunduki moja iliyotengenezwa kienyeji.

Bastola zilizokamatwa ni aina ya CESCA yenye NO.127159 iliyokuwa na risasi 4. nay a pili ilikuwa aina ya Chinese Pistol yenye NO. N001292 yenye risasi mbili.Pia bunduki iliyotengemnezwa kienyeji (Home made Gun) gobore iliyokutwa imeshindiliwa tayali kwa matumizi.

Kova aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni; Abdul Hamis Kinyunguza ambaye alikutwa na bastola aina ya CESCA. Ambaye ni mkazi wa Buza kanisani.

Said Athumani alikutwa na na Bastola aina ya CHINESE, ambaye ni mkazi wa Tanga mtaa wa maandazi, kwa upande wake Omari Abdul na wengineo walikutwa kwa makosa mbalimbali ya kujihusisha na uhalifu

Katika tukio la kujeruhi ambalo nilakusikitisha lililotokea jana tarehe 21.4.2010 majira ya saa 10 na dakika 50 jioni huko maeneo ya Mbagala Kingugi (W) Temeke Mtoto wa Kiume aliyetambulika kwa jina la Denatus Deminikus(4) mkazi wa Mbagala Kingungi aliyejeruhiwa kwa kuunguzwa na uji wa moto sehemu zake za siri na mapajani na shangazi yake aliyefahamika kwa jina la Bi.Deminata Theonest(29) mkazi wa Mbagala Kingugi ambaye ndiye alikuwa akiishi naye,Sababu ya kumuunguza motto huyo bado hajafahamika.Majeruhi amelazwa hospitali ya Temeke,Shangazi huyo alimchukua motto huyo toka Bukoba na kuja naye DSM kwa ajili ya kumlea na matokeo yake amekuwa akimfanyia vitendo vya ukatili Mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi unaendelea,alisema Kamanda Kova.

Thursday, April 22, 2010

AUNT EZEKIEL AKUTWA UKANDA WA MAKAHABA



Msanii mwenye nyota ya kung’ara katika tasnia ya muvi Bongo, Aunt Ezekiel Gryson ‘Gwantwa’ amenaswa na kamera ya paparazi wetu akiwa katika ukanda hatari kwa upatikanaji wa machangudoa, jijini Dar, Amani limekusanya albamu nzima.

Tukio hilo lilijiri ‘naiti’ ya Jumamosi pembezoni mwa baa maarufu ya Meridian iliyoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Aunt alitia timu eneo hilo majira ya saa saba usiku akiwa ndani ya kivazi cha Casino ambacho ni kipensi cha rangi ya bluu na singlendi ya rangi ya chungwa yenye maandishi mbele yakisomeka Trandy.

Baadhi ya wateja walioonekana kukolea kileo walianza kumjadili staa huyo wa filamu kutokana na mavazi yake hayo na maeneo aliyopo ambayo makahaba hupiga kambi kuwinda wateja wao.

Walisema vyema kama baada ya kufika eneo hilo na kampani yake wangetulia mahali kimya mpaka muda wa kutoka kuliko kutangatanga.


“La, si Aunt huyu? Mavazi gani sasa! Wenzake huvaa Casino kama Las Vegas, yeye anakuja nayo huku K’ndoni (Kinondoni) haoni kama anajijumuisha na ‘madadapoa’ wa barabara hii? Afadhali wangekaa mahali kimya mapaka wakati wa kutoka,” alisikika akihoji chapombe’ mmoja aliyekuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakimpiga chabo msanii huyo.

Mbali na Aunt, wenzake waliotimiza idadi ya watatu waliandamana naye na kulifanya eneo lote la baa hiyo kuwa na macho juu juu kwani walionekana kutoka kwenye kilevi kabla ya kupiga hema eneo hilo.

Ndipo paparazzi wetu mahiri aliposeti mtambo wake wa kamera yenye kuvuta picha kwa mbali na kuanza kuwafotoa ambapo walitawanyika huku na kule huku wakimkemea ‘fotografa’ huyo kwamba aache mara moja kitendo cha kuchukua picha zao kwa kuwa walivaa ‘kihasarahasara’.

Licha ya mafanikio ya kumpiga picha, Aunt aliweza kukimbia kila kona ya eneo hilo lengo likiwa kukwepa ‘lenzi’ ya kamera huku akiwa ameng’ang’ania kipochi kidogo kwa kukibana kwenye kwapa na simu aliyokuwa ameishika mkono wa kushoto.

Ilifika mahali Aunt aliamua ‘kama mmbwai mmbwai’ pale alipoamua kusimama na kumwambia paparazi, ananukuliwa: “Haya piga tani yako, we si unataka picha yangu nikiwa hivi, piga sasa!”

Usemi huo ambao huenda yeye alitegemea ungesitisha zoezi hilo ulimpa nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya mpiga picha wetu kwa kumlenga kisawa sawa kitendo kilichomfanya Aunt ajue kuwa, kumbe mshikakamera huyo alikuwa pale kikazi zaidi.


Wakati tafrani hilo likiendelea, wenzake walishasevu ishu hiyo kwa kwenda kuingia ndani ya gari na kumwacha ‘stering’ wao, Aunt akipambana na ‘adui’.

Mpaka mwisho wa mkanda, Aunt alikuwa amechoka kwa zoezi la kukimbiakimbia na sasa akabaki akitweta kama mwanariadha wa Ethiopia aliyeshiriki mbio za Marathon kwa mara ya kwanza.

Utafiti wa gazeti hili umegundua kuwa, asilimia sabini na tano ya machangu katika jiji la Dar wanapatikana wilaya ya Kinondoni hasa maeneo ya Makaburini, ukanda wa Mango Garden, MK na baa ya Meridian kuelekea Komakoma.

Sehemu nyingine ni Bamaga-Mwenge, barabara yote ya Shekilango, nje ya Club ya Sun Cirro, Magomeni ya Kwamacheni na kwenye Club maarufu wilayani humo ndiyo maana Aunt kuonekana kuzagaa eneo lile na mavazi yale kuliibua maswali kibao.

chanzo globalpublishers

HILI NDILO TAIFA LETU LA KESHO!!!


Kijana huyu hivi karibuni alinaswa na kamera yetu makutano ya barabara ya Bibi Titi Mohamed na Maktaba jijini Dar akiwa ameuchapa usingizi mzito kama anavyoonekana pichani. Hata hivyo haikufahamika mara moja sababu iliyomfanya kuuchapa usingizi eneo hilo.

Mtoto huyu ndio Taifa la kesho!!!???



Camera yetu ilikutana na mtoto huyu akiruka geti la nyumbani kwao maeneo ya Makumbusho Kijitonyama pengine hata sio kwao,Uzio wa Nyumba hiyo ukiwa umezungushiwa fensi ya umeme ambayo ingekuwa on ingeweza kusababisha madhara makubwa kwa huyu mtoto pengine hata kifo.


Hebu cheki dogo huyu alivyokuwa komando,unadhani hatma ya huyu mtoto ni nini?hapo baadaye?Wadau tunaomba maoni yenu.

LOVE YOUR JOB... NO MATTER WHAT YOU DO


Imetumwa na mdau wa umbea.com pia hata wewe waweza tuma habari yako na picha kupitia innolyimo24@yahoo.com.KARIBUNI SANA

TANESCO KUONGEZA MTANDAO WA EMEME MBINGA!!


Benjamin Sawe: Maelezo Dodoma
Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la umeme nchini imepanga kuongeza mtandao wa umeme mjini Mbinga kwa kujenga ujenzi wa njia ya kilometa moja ya msongo wa KV 11.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Adam Malima alisema ingawa Mbinga imeshapata umeme wa jenereta mbili zenye uwezo wa kuzalisha jumla ya MW2.5 bado kunahitajika umeme zaidi kulingana na shughuli za kiuchumi na jamii kuwa juu

Alisema Tanesco pia itafunga transoma yenye uwezo wa KVA 100 ikiwa ni pamoja na kujenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 2.0 ili kusambaza umeme maeneo ya Matika Tanki la maji mjini Mbinga.

Kwa mujibu wa Mheshimiwa Malima pia itafungwa transofoma yenye uwezo wa KVA 100 na kujenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 2.0 ili kusambaza umeme katika maeneo ya Matarawe Ruhuwiko

Aidha Mheshimiwa Malima alisema Serikali itajenga njia ndogo ya umeme yenye urefu wa kilometa 1.5 ili kusambaza umeme maeneo ya kiwandani Mbambi.

Alisema tatizo linalokwamisha upelekaji wa maeneo ya Maguu,Litembo,Matiri na Ruanda ni uwezo mdogo wa Serikali wa kutekeleza miradi ya kusambaza umeme nchi yote kwa pamoja kulingana na uwezo wa fedha.

AMWIK WATOA MAFUNZO YA HAKI ZA WANAWAKE NA WAJIBU WAO KWA SERIKALI NCHINI KENYA!!


Kina mama wa kabila la Kiturukana wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kupata mafunzo ya haki za wanawake. Chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Kenya (AMWIK) kimekuwa kikitoa mafunzo kwa kutumia Community Radio Listening Group kuwaelimisha wanawake hao ili wajue haki zao na wajibu wao kwa serikali.
(Picha na Anna Nkinda -Kenya)

Kundi kubwa la ngamia wakiwa wanakunywa maji katika mto Chicho Hoko ulioko wilayani Isiolo katika Mkoa wa North Estern nchini Kenya. Ngamia hao wanamilikiwa na wafugaji wa kabila la waborana.Hivi karibuni wilaya hiyo ilikumbwa na ukame uliosababisha kufa kwa mifugo mingi wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo lakini ngamia ni wanyama wanaostahimili hali ya ukame.

Mdau Lawrence Mureith akiwa amesimama nje ya moja ya nyumba ya kabila la waturukana ambao ni wafugaji wanaopatikana huko wilayini Isiolo mkoani Kenya.

Watoto wa kabila la kiturukana wakiwa na nyuso za furaha wakati wanapigwa picha.

Kina mama wa kabila la Kiturukana kutoka kundi la ANUPIT wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Kenya (AMWIK) mara baada ya mafunzo ya haki za wanawake na wajibu wao kwa serikali yanayotelewa na chama hicho kwa kutumia Community Radio Listening Group.

Wednesday, April 21, 2010

J....MARTINS AFANYA ONYESHO LA NGUVU JANA


Hili ndio jengo lenyewe lililozinduliwa jana kama taswira ya picha inavyoonyesha na stage yake kwa mbele ambapo ndipo j martins atakapo warusha wadau wake na kwa mujibu wa ratiba niliyopata kuwa mambo yalirushwa live na kituo cha ITV NA CHANNEL 5 huku kiingilio kikiwa ni miguu yako tu hahahhahahah.
picha na kachero wa umbea.com

KAMERA YA UMBEA.COM YAMBAMBA KANUMBA AKINUNUA MKANDA


kama mnavyonijua wadau wangu kwa umbea jana mida ya juaa kali nilimbamba msanii huyu akimuunga mkono kijana huyu kwa kununua mkanda kwa ajili ya suruale yake ambalo ni jambo zuri kwa kuwajali vijana hawa wanaouza vitu vidogo vidogo big up sana brother mie nimekuunga mkono

Vyeti Necta kuwekwa picha za mtahiniwa

KUTOKANA na vitendo vya udanganyifu kukithiri kwenye vyeti vya kidato cha nne na cha sita, Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limeanza kuweka picha katika vyeti vya matokeo ya ngazi hizo za elimu, ili kuwawezesha wadau kumtambua mmiliki halali wa cheti.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, aliliambia Bunge mjini Dodoma kuwa picha hizo huwekwa kwa kompyuta hivyo haziwezi kuondolewa kirahisi na mtu yeyote.

Uwekaji huo wa picha katika vyeti utaanza na vyeti vya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2008 ambavyo vitachapwa Mei 2010.

Naibu Waziri huyo alisema hati za matokeo ya mitihani ya kidato cha nne 2009 nazo zimetolewa zikiwa na picha.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde, Dk Ali Tarab Ali (CUF), aliyehoji kwa nini vyeti vya kidato cha nne na sita visiwekwe picha ya mtahiniwa husika kwa kutumia kompyuta ili kuondoa tatizo la udanganyifu.

Mbunge huyo katika maelezo yake alidai baadhi ya vyeti vya matokeo ya mtihani wa kitaifa ya kidato cha nne na sita kutoka Necta, vinatumiwa na watu wengine wasio watahiniwa kwa ajili ya kutafuta ajira au nafasi za masomo nje.

Katika kujibu swali hilo, Mahiza alikiri kuwa ni kweli kwamba baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu wamebainika kutumia vyeti vya matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne na sita visivyokuwa vyao, kwa ajili ya kutafuta ajira au nafasi za masomo ya juu, jambo ambalo ni kosa la jinai.

Alitoa mwito kwa wananchi wote kuacha mtindo wa kutumia vyeti visivyokuwa vyao kwani kufanya hivyo kunawanyima wenye vyeti stahili zao na ni kutenda kosa la jinai.

Katila swali lake la nyongeza, Mbunge huyo wa Konde alidai kuwa suala la mtu kutumia cheti ambacho sio chake mara nyingi linafanywa kwa makubaliano na mwenye cheti husika, hivyo alitaka kufahamu pia hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa wote walioshiriki kufanya udanganyifu huo.

Lakini kwenye majibu yake, Mahiza alisema kuwa kesi za kuuza cheti ni chache sana na mara nyingi kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wanapata kesi za watu kupotolewa na huwa wanazipeleka Polisi ili zishughulikiwe.

FIXTURE KILI TAIFA CUP - 2010 GROUP 'A' - DODOMA

(a) Dodoma
(b) Kigoma
(c) Singida
(d) U - 20

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Singida V/S U-20 14:00 HRS JAMHURI ST.
2. 5/8/2010 C/D Dodoma V/S Kigoma 16:00 HRS JAMHURI ST.
5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C U-20 V/S Dodoma 14:00 HRS JAMHURI ST.
4. 5/10/2010 D/A Kigoma V/S Singida16:00 HRS JAMHURI ST.

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Singida V/S Dodma 14:00 HRS JAMHURI ST.
6. 12-May-10 D/B Kigoma V/S U-20 16:00 HRS JAMHURI ST.
GROUP 'B' - TANGA
(a) Tanga
(b) Morogoro
(c) Pwani
(d) Temeke

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Tanga V/S Morogoro 14:00 HRS MKWAKWANI
2. 5/8/2010 C/D Pwani V/S Temeke 16:00 HRS MKWAKWANI

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Morogoro V/S Pwani 14:00 HRS MKWAKWANI
4. 5/10/2010 D/A Temeke V/S Tanga 16:00 HRS MKWAKWANI

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Tanga V/S Pwani 14:00 HRS MKWAKWANI
6. 12-May-10 D/B Temeke V/S Morogoro 16:00 HRS MKWAKWANI

GROUP 'C' - MWANZA
(a) Mwanza
(b) Kagera
(c) Shinyanga
(d) Tabora

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Shinyanga V/S Kagera 14:00 HRS C.C.M. KIRUMBA
2. 5/8/2010 C/D Mwanza V/S Tabora 16:00 HRS C.C.M. KIRUMBA

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Kagera vs Mwanza 14:00 HRS C.C.M. KIRUMBA
4. 5/10/2010 D/A Tabora vs Shinyanga 16:00 HRS C.C.M. KIRUMBA

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Shinyanga vs Mwanza 14:00 HRS C.C.M. KIRUMBA
6. 12-May-10 D/B Tabora V/S Kagera 16:00 HRS C.C.M. KIRUMBA

GROUP 'D' - ARUSHA
(a) Arusha
(b) Mara
(c) Manyara
(d) Kilimanjaro

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Mara V/S Kilimanjaro 14:00 HRS SHEKH AMRI ABED
2. 5/8/2010 C/D Manyara V/S Arusha 16:00 HRS SHEKH AMRI ABED

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Kilimanjaro V/S Manyara 14:00 HRS SHEKH AMRI ABED
4. 5/10/2010 D/A Arusha V/S Mara 16:00 HRS SHEKH AMRI ABED

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Mara V/S Manyara 14:00 HRS SHEKH AMRI ABED
6. 12-May-10 D/B Arusha V/S Kilimanjaro 16:00 HRS SHEKH AMRI ABED

GROUP 'E' - IRINGA
(a) Iringa
(b) Mbeya
(c) Rukwa
(d) Kinondoni

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Rukwa V/S Mbeya 14:00 HRS SAMORA ST.
2. 5/8/2010 C/D Iringa V/S Kinondoni 16:00 HRS SAMORA ST.

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Mbeya V/S Iringa 14:00 HRS SAMORA ST.
4. 5/10/2010 D/A Kinondoni V/S Rukwa 16:00 HRS SAMORA ST.

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Rukwa V/S Iringa 14:00 HRS SAMORA ST.
6. 12-May-10 D/B Kinondoni V/S Mbeya 16:00 HRS SAMORA ST.

GROUP 'F' - MTWARA
(a) Mtwara
(b) Lindi
(c) Ruvuma
(d) Ilala

SN - DATE - CODE - TEAMS - TIME - GROUND
1. 5/8/2010 A/B Lindi V/S Ruvuma 14:00 HRS NANGWANA ST.
2. 5/8/2010 C/D Mtwara V/S Ilala 16:00 HRS NANGWANA ST.

5/9/2010 REST DAY

3. 5/10/2010 B/C Ruvuma V/S Mtwara 14:00 HRS NANGWANA ST.
4. 5/10/2010 D/A Ilala V/S Lindi 16:00 HRS NANGWANA ST.

5/11/2010 REST DAY

5. 12-May A/C Lindi VS Mtwara 14:00 HRS NANGWANA ST.
6. 12-May-10 D/B Ilala VS Ruvuma 16:00 HRS NANGWANA ST.

FIXTURE KILI TAIFA CUP - 2010
QUARTER, SEMI FAINAL AND FAINAL
KILIMANJARO TAIFA CUP 2010
FROM 23 MAY, 2010 TO 29 MAY, 2010
UHURU STADIUM - DAR ES SALAAM

SN - DATE - TEAMS - TIME - GROUND
QUARTER FINAL

1. 23 May, 2010 WINNER GROUP 'A' V/s WINNER GROUP 'B' 14:00 HRS UHURU ST - DSM
2. 23 May, 2010 WINNER GROUP 'C' V/s WINNER GROUP 'D' 16:00 HRS UHURU ST - DSM
3. 24 May, 2010 WINNER GROUP 'E' V/s WINNER GROUP 'F' 14:00 HRS UHURU ST - DSM
4. 24 May, 2010 WINNER GROUP 'G' V/s WINNER GROUP 'H' 16:00 HRS UHURU ST - DSM

SEMI FAINAL

5. 25 May, 2010 WINNER GROUP 'A' V/s WINNER GROUP 'B' 16:00 HRS UHURU ST - DSM
6. 26 May, 2010 WINNER GROUP 'C' V/s WINNER GROUP 'D' 16:00 HRS UHURU ST - DSM

27 May, 2010 REST DAY

7. 28 May, 2010 LOOSER No. '5' V/s LOOSER No. '6' 16:00 HRS UHURU ST - DSM
8. 29 May, 2010 WINNER GROUP '5' V/s WINNER GROUP '6' 16:00 HRS UHURU ST - DSM

Tuesday, April 20, 2010

MIAKA HIYO……THOSE WERE THE DAYS! VERY INTERESTING

JIKUMBUSHE NA BARUA ENZI HIZO ZA KISHULE SHULE…LUGHA HAIPANDÄ°..HALAFU UNAILAZIMISHA IPANDE..BINTI AMEMWANDIKIA BARUA ‘BOIFLENDI’ WAKE..(pichani ndiyo binti)

Dear Sugar
Time and ability plus double capacity has forced my pen to dance automatically on this benedicted sheet of paper. Why! this miraculous thing happened is because papie I love you spontaneously and as I stand horizontal to the wall and perpendicular to the ground I only think of you, since you are a fantastic and fabulous guy.

Papie please Stop haranguing with the feelings in my heart because I love you more than a snake loves the rat. To me each day starts by thinking of you and ends by dreaming of you. Each time I see you, my metabolism suddenly stops and my peristalysis goes in reverse gear. My medula-oblangata also stops functioning.
Crazy crazy crazy you may say but this is true. If only you knew what is going on in my encephalon you would understand. That’s why I need to see you face to face with you, soon. I think I have to pen-off here because I still haven’t finished studying electrolysis and polymerization. Catch you Pa – later. Sleep tight and don’t let those bed bugs ever bite you coz you are too sweet a thing for them.
I have put my beautiful picture in the letter for you.

Yourz Ever,
Sugar nonoza..

BAADA YA YA ’BOIFLENDI’ KUPATA BARUA MAJIBU YAKAWA HIVI…..(pichani ndiyo BF mwenyewe)

Dear Honie
My Love, My Sugar, i was exasperated with pride to have received one from you, the lungs in my body flapped with joy when i have been reading your letter. Anyway by now you have reached the realisations to why i am jotting this small letter to you, yes it is to see if you are keeping with the sands of time.
How is everything on that other side of yours? Well here everything is just half lemon half sugar to make it schweppes. How is your schooling? How are you pulling the wagons of life? I am just pulling the schooling thing like a donkey pulling a cart.

My honie, i am missing you very much right now, my heart is perambulating with every word that i write, if it was not for these oceans that decided to flow between us then i would get on the next bus to come and see you, but until then i know that i will not hesitate to put this blue blood on this paper and write to you. I remember that day lovie, that one sweet day as Maria Curry sanged it, you know that it is my favorites song honie, the one day that we were boarding the combies and you escorted me to my home, walking with you just brought sweet dreams to me for the rest of my life honie.

If words of love could ride a bicycle I would be competing against Diego Maradona. Anyways, i will not stop you from reading the books that give you life and education so I will stop here for today.
Please always writing to me because I am missing you like sugar misses tea. You can see my foto in the letter. My dedications to you are : Maria Curry – One Sweet Day. Boys to Main – And of the Rod.

Keep well my mop of my heart,
Yours in flesh and in blood,
Ruise Sugar Baby.

P.S. Sorry about my english, I did not learn anymore

Stiggo thanks for the email!!!!

HAWA NDIO BAADHI YA WASANII WALIO UWAGA UKAPERA.


Mmoja wa member anayeunda kundi la Wakali Kwanza, Joseph Mapunda a.k.a Qj pichani akiwa na mkewe Bi Elizabeth na kwa sasa wameungana na kuwa kitu kimoja kama Mr and Mrs Joseph Mapunda hii ni juzi tu jamaa kavuta jiko safi.

Huyu ni Matonya siku ya harusi yake hapo akiwa na rafiki yake kipenzi Banana Zoro pamoja na mkewe.. Na kwa kudra zake mwenyezi mungu ndoa hiyo imeshaipa baraka kwa kupatikana mtoto.. Tonya pia ni moja kati ya wasanii wa bongo flava ambao tayari washauwaga ukapera.

Picha juu ni Juma Nature na mkewe Pili siku ya harusi yao .. Sir Juma Nature na mkewe wamebarikiwa kupata mtoto wa kike aliyezaliwa katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke.. Huyu ni Mwingine pia ambaye amesha watoroka wale wengi ambao bado hawajakamilisha hili.

Baada ya vikao vingi vya kukamilisha hili na kupanga jinsi ya kulikamilisha hatimaye siku ikafika na kijana kutoka TMK Wanaume Family kuuwaga rasmi ukapera na kutuletea shemejiiiii.....!!! Ilikuwa siku ya jumamosi baada ya kuchukuwa kifaa jumla, hii ilikuwa katika kanisa la Azania Front jijini Dar es salaam.

Judith Wambura alizaliwa mkoani Shinyanga tarehe 15 jun, 1979 kwa Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake. Inasemekana dada jide alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba, alianza kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi, bi shosti pia ni moja ya wasanii wa bongo flava wanaoishi kwenye ndoa kwa sasa.

Banana Zorro na Suzy Walele wakilishana keki siku ya harusi yao iliyofanyika katika ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar - es- salaam. Banana pia ni masanii wa bongo flava ambaye amesha sepa kwenye kundi la ukapera.

Na kwa sasa nadhani huyu ndio atakaye fata tunamuombea kila la kheri mungu ampe wepesi katika hilo Amin inshaallah.