Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, October 20, 2010

Zitto anadi gwanda, achangisha 800,000/- papo hapo!



Kampeni za Naibu Katika Mkuu wa CHADEMA Taifa, Zitto kabwe, katika jimbo la Sumbawanga mjini zimeendelea kuiweka pabaya CCM kutokana na kampeni zake kuwachambua kinagaubaga.
Watu zaidi ya 2,000 walifanya maandamano ya furaha kwa kumsindikiza mgombea ubunge wa jimbo hilo Mwalimu Norbert Yasembo. Pia, walitumia mkutano wa kampeni za CHADEMA kumchangia mgombea huyo fedha za kuwalipa mawakala wake kiasi cha shilingi zaidi ya 800,000/- katika harambee iliyoendeshwa na Zitto ambaye pia alijitolea kuchangia kampeni hizo kwa kuuza kombati yake kiasi cha shilingi 200,000/

Akihutubia katika mwendelezo wa mikutano ya kampeni ya CHADEMA mkoani Rukwa katika viwanja vya Rukwa High School jana, mbali ya kukataa kata kata dua za wananchi hao kumwombea kuwa Spika wa bunge lijalo la Muungano wa Tanzania, Kabwe alisema kuwa lazima CCM itambue kuwa hatua ya wananchi kuchangia kiasi hicho cha fedha ni mwisho mbaya kwake na kuwa itegemee kushinda kwa miujiza jimbo hilo.

“Nasema napongeza sana kwa mapokezi haya makubwa ambayo mmeonyesha kwangu na huu ni ushadidi kuwa mgombea wa CCM katika jimbo hili Aesha Hillary si chaguo halisi la wana jimbo la Sumbawanga mjini hivyo si vizuri kwa wachache waliobaki kupoteza kura zao kwa kumpa mgombea ambaye hatakiwi “

Alisema kuwa mkoa wa Rukwa, Kigoma na Tabora ni mikoa ambayo makao makuu yake bado hadi sasa hajaunganisha na lami hali ambayo inahitaji kuwapata wabungemakini watakaoweza kutetea wananchi wa mikoa hiyo kuwa ni sehemu ya wananchi wa mikoa ya Tanzania ambayo kwa sasa imeunganishwa kwa lami .

“Ndugu zangu, Tanzania ni moja na mikoa yote ya Tanzania wananchi wake ni walipaji wakubwa wa kodi, hivyo kitendo cha Serikali ya CCM kuendelea kuwabagua wananchi wa mikoa hiyo ni sawa na kuwaona kuwa hawafai kupewa huduma hiyo na dawa pekee ni wananchi wa mikoa hiyo kuunga na kuwanyima kura wagombea ubunge wa CCM na kuwapa wale wa CHADEMA ambao kupitia Rais mpya wa awamu ya tano kwa Tanzania Dk Wilbrod Slaa, wananchi wa mikoa hiyo wanapewa haki yao ya lami”

Kabwe alisema kuwa wananchi wa Tabora, Kigoma na Rukwa wasipokubali kuunganisha nguvu zao katika kuchagua wabunge wa CHADEMA, bado CCM itaendelea kuwafanya kuonekana kuwa wanyonge. Aliongeza kuwa, katika mkoa wa Kigoma kwa bunge lililopita mbunge wa upinzani alikuwa ni mmoja pekee huku katika mkoa wa Rukwa pia kulikuwa na mbunge moja hivyo ni vizuri Oktoba 31 wakaongeza idadi zaidi ili kuwe na idadi kubwa ya wabunge.

Hata hivyo, alisema kuwa kwa upande wake hana tatizo la jimboni kwake kwani tayari ameshinda na anasubiri kuapishwa na Rais wake Dk Slaa.

Katika hatua nyingine, Kabwe ameshangawa na hatua ya ulinzi mkali aliowekewa katika jimbo hilo la Sumbawanga mjini ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha askari polisi, askari magereza, pamoja na mgambo kufika kulinda mkutano jambo ambalo hajapata kuona askari magereza wakifika katika mikutano ya kampeni kama jimbo hilo la Sumbawanga mjini na kuwa yawezekana katika mkutano wake huo, wafungwa pia wamefunguliwa ili kujakusikiliza sera za CHADEMA.

Katika mkutano huo uliomalizaka kabla ya muda wa kampeni kuisha, wananchi walifanya maandamano makubwa huku biashara zao zikisimama kwa muda kwa ajili ya kusukuma gari la Zitto Kabwe pamoja na ile ya mgombea ubunge wa CHADEMA huku wakiimba kuwa wanataka mbunge Msomi wa CHADEMA sio CCM. Hatua hiyo ilionyesha kuwapa wakati mgumu askari polisi magereza na wale wa jeshi la polisi nchini kuwatuliza wananchi hao na kuwaomba viongozi wa CHADEMA kuwatuliza na kuwatawanya wananchi hao zaidi ya 2,000 kabla ya mgombea ubunge wa CHADEMA kuamua kuwatoroka viongozi wenzake ofisini ili waandamanaji hao watawanyike.

from: http://www.wavuti.com/4/post/2010/10/zitto-anadi-gwanda-mkutanoni-achangisha-800000-papo.html#ixzz12sZxXuaZ

4 comments: