Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, October 12, 2010

KIFAAA KINATAFUTA BWANAAAAA


mrembo ni Miss Temeke 2003/04, anaitwa Mariam Omary ambaye by now ni mkufunzi wa mashindano ya urembo hapa Bongo.
Huyu mto bana, amekaa chini na ku-discuss baadhi ya mwenendo wa life na kugudua kuwa anamisi kitu kimoja tu muhimu, yaani mwanaume.
So Mariam ni mtoto wa jijini pande za Mangomeni Morocco, ana age ya miaka 24, muonekano wake kiukweli mtoto ana shepu ya ki-miss na kwamba amelelewa katika mazingira sahihi ya Kitanzania. Hivyo basi, anatafuta mchumba mwenye umri wa kuanzia miaka 28 kuendelea mwenye sifa zifuatazo:
Mfanyakazi wa serikali au kampuni yoyote binafsi.
Awe na akili timamu.
Awe na Elimu ya kutosha.
Awe na uwezo wa kutunza familia na siyo Mariooo.
Awe tayari kupima ngoma.
Are you ready? Na je, una sifa zote hizo? Fanya fasta, mcheki kwa namba 0652-018355

Wednesday, September 29, 2010

Muswada wa Obama wa kudhibitiwa Internet nchini Marekani


Rais Barack Obama wa Marekani anajiandaa kuwasilisha muswada wa kudhibitiwa matumizi ya Intaneti nchini humo.
Kwa mujibu wa muswada huo, maelezo binafsi ya watumiaji wa Intaneti ikiwa ni pamoja na barua-pepe zao na mitandao ya kijamii zitakuwa zinawafikia moja kwa moja polisi wa FBI.

Gazeti la New York Times limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, kama muswada huo utapitishwa, basi maelezo ya wanachama wa mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Skype yatakuwa yanawafikia moja kwa moja polisi wa Marekani FBI itakapobidi.
Muswada huo unatarajiwa kuwasilishwa mbele ya Baraza la Congress la Marekani mwaka ujao wa 2011.

Maafisa usalama wa Marekani wanasema kuwa inabidi sheria na hatua mpya zichukuliwe kwa ajili ya kudhibiti na kuwekea mipaka matumizi na mawasiliano ya Intaneti nchini humo.
Lakini baadhi ya weledi wa mambo wameelezea wasiwasi wao kuwa hatua hizo mpya zitapelekea watu wenye nia mbaya kupenya ndani ya barua-pepe za watu binafsi na kufanya uhalifu na uharibifu.

Haramia wa kisomali akamatwa Tanzania


Jeshi la Tanzania limesema limemkamata mshukiwa mmoja wa Uharamia raia Somalia, kufuatia makabiliano makali ya ufyatulianaji wa risasi katika bahari ya Hindi.

Ripoti zinasema tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili iliyopita katika eneo la Kusini mwa pwani ya Tanzania, eneo ambalo meli ya kampuni ya kuchimba mafuta ya Ophir inafanya utafiti ili kubainisha ikiwa eneo hilo lina utajiri wa mafuta ya Petroli.

Msemaji wa jeshi la wanamaji nchini Tanzania, Steve Buyuya, amesema manuawari ya kijeshi ilishambuliwa kwa risasi na maharamia waliokuwa kwenye mashua ndogo.
Lakini baada ya ufyatulianaji wa risasi uliodumu kwa muda, maharamia kadhaa walifanikiwa kutoroka huku mmoja wao akikamatwa na wanamaji wake.

Andrew Chenge akamatwe haraka- Mahakama Yatoa Amri




BAADA ya kutoonekana mahakamani jana , Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni, Dar es Salaam imeamuru kukamatwa kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Chenge ambaye yuko nje kwa dhamana akikabiliwa na mashitaka ya kusababisha vifo vya watu wawili, jana hakufika mahakamani hapo wala mdhamini wake bila taarifa.
Amri hiyo ilitolewa mahakamani hapo na Hakimu Sundi Fimbo, baada ya mwendesha mashitaka, Richard Rweyongeza kusoma maelezo ya awali ya mashitaka yanayomkabili mshitakiwa.

“Haijalishi kuwa mshitakiwa yuko kwenye kampeni au wapi, Mahakama haitambui jambo lolote kuhusu kampeni, hivyo kwa kuwa hajahudhuria mahali hapa, inabidi akamatwe kwa kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama,” alisema Hakimu Fimbo.
Alifikia uamuzi huo baada ya masharti ya dhamana ambayo yanamtaka mshitakiwa kufika mahakamani siku ya kesi aliyopangiwa na bila hivyo atoe taarifa za kutofika kwake mahakamani.

Kwa niaba ya Hakimu Mkazi, Kwey Rusema, ambaye anasikiliza kesi hiyo, Hakimu Fimbo aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 5 mwaka huu itakaposikilizwa tena.
Ilidaiwa kuwa Machi 27, 2007 mshitakiwa akiendesha gari aina ya Toyota Hilux namba T 512 ACE alimgonga mwendesha pikipiki ya magurudumu matatu - bajaj jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya Beatrice Costantine na Victoria George.
Awali baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka, Mahakama ilisema Chenge ana kesi ya kujibu na alitakiwa kufika mahakamani jana kuanza kusikiliza utetezi wake.

Chenge ambaye anatetea ubunge Bariadi Magharibi alisema ataleta mashahidi wawili ambao ni yeye na shahidi mwingine ambaye hakutajwa mahakamani.
Aidha, katika kesi hiyo shahidi wa mwisho wa upande wa mashitaka, Raymond Njeje, alidai kuwa stika ya bima aliyokuwa akitumia Chenge si mali yake.
Njeje alidai kuwa, stika hiyo ni ya gari namba T 571 AKH aina ya Toyota RAV4 nyeusi na si ya Toyota Hilux iliyosajiliwa kwa namba T 513 ACE ambalo alikuwa akiendesha Chenge wakati anapata ajali.

Alidai stika hiyo namba 11919156 inamilikiwa na Evarist Ses iliyotolewa mwaka 2007 kwa ajili ya matumizi ya miezi mitatu kuanzia Juni 29 hadi Septemba 28.

Monday, September 27, 2010

Titus Bramble atuhumiwa kubaka!!


Mlinzi wa timu ya Sunderland Titus Bramble, amekamatwa baada ya mwanamke kubakwa kwenye hoteli moja mjini Newcastle.

Mchezaji huyo wa Ligi Kuu ya England amekamatwa pamoja na mtu mwengine katika hoteli ya Vermont mapema siku ya Jumatano na wanahojiwa na polisi.
Bramble mwenye umri wa miaka 29 amekamatwa kwa kushukiwa amebaka baada ya polisi kupigiwa simu na mwanamke mmoja.

Klabu ya Sunderland hadi sasa haijazungumza lolote kuhusiana na tuhuma hizo. Bramble alijiunga na klabu hiyo akitokea Wigan msimu huu.

Mwanamke mwenye matatizo ya akili anyongwa Marekani.


Teresa Lewis mwanamke mwenye umri wa miaka 41 mwenye matatizo ya akili amenyongwa leo nchini Marekani kwenye jimbo la Virginia, kwa kosa la kumuua mumewe na mjukuu wake wa Kambo.

Teresa ni mwanamke wa kwanza kuhukumiwa adhabu ya kifo nchini Marekani tangu mwaka 1912 na amesubiri kutekelezewa adhabu hiyo kwa muda wa miaka mitano.
Mwanamke huyo ameuawa kwa kudungwa sindano ya sumu. Maswali mengi yamejitokeza kuhusiana na uwezekano wa mama huyo aliyekuwa na kiwango cha akili cha IQ 72 kupanga na kutekeleza mauaji hayo ya watu wawili, ambaye pia imejulikana alikuwa na matatizo ya akili.

Mahakama kuu ya Marekani na Gavana wa jimbo la Virginia walikataa kuondoa adhabu hiyo ingawa wengi wametilia shaka kesi hiyo na maelfu ya watu walitaka iondolewe. Virginia ni jimbo la pili nchini Marekani linaloongoza katika utendaji vitendo vya jinai.

TAKUKURU yamsafisha Waziri Batilda Buriani!


TAASISI na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha imekenusha kuwashikiliwa baadhi ya wafuasi wa mgombea ubunge wa Arusha Mjini, Dk. Batilda Burian, ambao pia ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa tuhuma za kuhusishwa na rushwa katika uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Kamanda wa taasisi hiyo Mkoa wa Arusha, Ayubu Akida, alisema habari hizo zimetolewa pasipo kufanyiwa uchunguzi wa kina.

Kamanda Akida alisema ni kweli walipata taarifa ya kuwepo kwa kikao katika nyumba moja katika Kata ya Baraa jijini hapa, ambapo washiriki hao wangegawiwa fedha ili kuwashawishi wapiga kura kumpigia kura mgombea ubunge wa Arusha Mjini ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Burian.

Alibainisha kuwa maofisa wa Takukuru walifika katika nyumba hiyo jioni na kujichanganya na watu waliokuwamo ndani ya nyumba hiyo ambao baadaye walibainika kuwa wanavikundi na wanachama wa CCM waliokuwa na vikao vya ndani lakini hakukuwapo na tukio la utoaji wa fedha.

Alisema baada ya kubaini hilo maofisa wa Takukuru hawakuona sababu ya kuwakamata wanachama hao kwa kuwa CCM wana utaratibu wa kuwa na vikao vya ndani, ambavyo wao huviita kampeni za nyumba kwa nyumba ambapo mgombea hukutanishwa na wananchi ili kueleza sera zake.

“Unajua haya yanayosemwa ni njama za kunichafua kisiasa zaidi mbele ya wapiga kura ambao hata saa nane za usiku wapo tayari kuichagua CCM… mwanzo nilizushiwa kuhusu ndoa yangu, sasa wameona wakimbilie TAKUKURU na kunichafua katika vyombo vya habari, mimi ni mkomavu wa kisiasa, sina wasiwasi na haya,” alisema Dk. Batilda.