Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, September 27, 2010

TAKUKURU yamsafisha Waziri Batilda Buriani!


TAASISI na Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Arusha imekenusha kuwashikiliwa baadhi ya wafuasi wa mgombea ubunge wa Arusha Mjini, Dk. Batilda Burian, ambao pia ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa tuhuma za kuhusishwa na rushwa katika uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Kamanda wa taasisi hiyo Mkoa wa Arusha, Ayubu Akida, alisema habari hizo zimetolewa pasipo kufanyiwa uchunguzi wa kina.

Kamanda Akida alisema ni kweli walipata taarifa ya kuwepo kwa kikao katika nyumba moja katika Kata ya Baraa jijini hapa, ambapo washiriki hao wangegawiwa fedha ili kuwashawishi wapiga kura kumpigia kura mgombea ubunge wa Arusha Mjini ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Burian.

Alibainisha kuwa maofisa wa Takukuru walifika katika nyumba hiyo jioni na kujichanganya na watu waliokuwamo ndani ya nyumba hiyo ambao baadaye walibainika kuwa wanavikundi na wanachama wa CCM waliokuwa na vikao vya ndani lakini hakukuwapo na tukio la utoaji wa fedha.

Alisema baada ya kubaini hilo maofisa wa Takukuru hawakuona sababu ya kuwakamata wanachama hao kwa kuwa CCM wana utaratibu wa kuwa na vikao vya ndani, ambavyo wao huviita kampeni za nyumba kwa nyumba ambapo mgombea hukutanishwa na wananchi ili kueleza sera zake.

“Unajua haya yanayosemwa ni njama za kunichafua kisiasa zaidi mbele ya wapiga kura ambao hata saa nane za usiku wapo tayari kuichagua CCM… mwanzo nilizushiwa kuhusu ndoa yangu, sasa wameona wakimbilie TAKUKURU na kunichafua katika vyombo vya habari, mimi ni mkomavu wa kisiasa, sina wasiwasi na haya,” alisema Dk. Batilda.

No comments:

Post a Comment