Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, March 22, 2010

HAKUNA HELA MBOVU, ATAYEIKATAA KUSHITAKIWA!!



Serikali imewasihi na kuwaomba radhi baadhi ya wananchi kuacha kukataa baadhi ya fedha halali zilizoko kwenye mzunguko kwa madai kuwa hazifai kwasababu ya uchakavu wake.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa wizara ya uchumi na fedha, Ramadhani Kijah, hakuna sheria inayomruhusu mwananchi kuzikataa fedha hizo.
Alisema ingawa kuna malalamiko ya uchakavu wa koini za sh 100, alisema hiyo siyo sababu ya kuzikataa kwani zinatambulika na sheria.
"Fedha hizo zitumike hadi hapo zitapofika benki amabako ndiko zitakuwa mwisho wake kwani kule kuna watu maalumu waliojariwa kuteketeza pesa mbovu na hata hela chafu," alisema Kijah.
Kijah alisema kwa yeyote atakayepinga kupokea fedha hizo basi atambue kuwa anapingana na sheria zilizowekwa na serikali hivyo atakuwa anajijengea mazingira ya kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Saturday, March 20, 2010

“MO KUMSIMIKA KAMANDA WA UVCCM MAGU-MWANZA LEO”


Mh.Mohammed Dewji.

Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida mjini,ameondoka Dar es Salaam jana,kuelekea Mkoani Mwanza kwa ajili ya Sherehe za Kumsimika Ukamanda Mbunge wa jimbo Busega,Mh.Raphael Chegeni,Sherehe hizo zitafanyika katika Wilaya ya Magu,Mkoani Mwanza,Mh Dewji pia atashiriki katika Harambee ya Amani SACCOS katika kijiji cha Lamadi jimbo la Busega.

Hon. Lawrence Maasha Minister of Home Affairs hosted Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia at his office at the Ministry on 19 March, 2010 where he


Hon. Lawrence Maasha Minister of Home Affairs hosted Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia at his office at the Ministry on 19 March, 2010 where he handed her The Tanzanian Flag as She represents for the First Time TANZANIA at the 19 Miss India Worldwide Pageant to be Held in Durban South Africa on March 27, 2010.

Friday, March 19, 2010

KIBAKA AKILA KICHAPO TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI!


Kibaka anachukua kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali huko mitaa ya Posta....USHAURI WA BUREjamni acheni wewe mmoja watu wenge mtajapoteza maisha kwa kichapo
picha na inno lyimo!

KWELI BONGO MISHEMISHE!

Ama kweli bongo misheshe kamera yetu ya UMBEA.COM ilikuwa mitaani kama kawaida yake ya huku na kule na bahati nzuri ilikutana na huyu kijana akifanya biashara ya kuuza kahawa maeeneo ya kariakoo sokoni huku akiwa vutia wateja wake kwa alivyo vaa na utani ndani yake!big up sana kaka uko creative kinoma
Picha na inno lyimo

BABA NA MWANA MGONGONI.....................................


Mdau huyu alibabwa na kamera yetu siku za hivi karibuni. Ni mkaka tu wa kawaida, kajibebea mwanae mgongoni, anadunda mtaa kwa mtaa, shida hataki!
SWALI:
wababa wangapi mnaweza kubeba watoto wenu mgongoni mkapita nao mtaani kama hivi?
Piccha na inno lyimo!

Adhabu hizi zinafundisha au udhalilishaji?



Wengi tiliosoma Saint Government aka St. Mchangani tushashika masikio kwa style hii sana tu!
Ukiona kama mchezo, ila unaumia, acha tu, miguu inakosa nguvu kabisa, afu kama una ugonjwa wa kutoka damu puani, au kusikia kizunguzungu inakua balaa!
Afu kuna ya kuita juu, mkiwa wengi mtu anaweza kudhani mnafanya choreography, maana inapendeza, kumbe mnateseka, ila fimbo ndio kiboko ya wote!
Ingawa siku hizi watoto wengi wanasoma St Private aka English Academy, no fimbo, no adhabu kali, je adhabu hizi zilikua zinasaidia?
picha na inno lyimo