Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, April 2, 2010

mpango mzima wa pasaka ndio kama hivi

NGWEA KUCHINJA MBUZI VINGUNGUTI PASAKA


Msanii wa Kizazi Kipya Albart Mangwea (Ngwea), katika kusherehekea Siku kuu ya Pasaka, Jumatatu ya Pasaka patakuwa apatoshi katika Ukumbi wa Mpya na kisasa wa Mashujaa Pub, Uliopo Vingunguti Kiembe Mbuzi, ambapo kutakuwa na Shoo Kabambe itakayoambatana na Disco Kali litakaloshushwa na Madj wa siku nyingi(Wakongwe) –Dj Dullah, na Dj Say Dou.
Mratibu wa Shamrashamra hizo Said Salum alisema kuwa pia amewaandalia shindano la kukuza vipaji wasanii chipukizi( underground), katika muziki wa kizazi kipya ususani wakazi wa Vingunguti na maeneo ya jirani, Buguruni, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, na Tabata ambayo zawadi mbalimbali itatolewa kwa atakayeonyesha kipaji kuzidi wengine.


Alisema kuwa maonyesho hayo yataanza mapema ambapo zawadi ya kwanza itakuwa kwa mteja atakayekuwa wa kwanza kukata tiketi kuwa atapatiwa furana ya Mashujaa Musica ikiwa kama kumbukumbu ya Ukumbi wa Mashujaa Hall ambao ndiyo walezi wa Bendi hiyo.



Kiingilio kwa mujibu wa Said kitakuwa ni cha chini ili kukidhi uwezo wa vijana ambacho kimepangwa kuwa shilingi 3000 kwa wakubwa na 1000 kwa Disco Toto litakaloanza mapema saa kumi jioni hadi mbili usiku ambapo baadaye kitafuata Ngwea kuwapa raha mashabiki wake(kukimbiza kisanii) kabla ya kupisha Disco kwa watu wote kuserebuka.



Wakazi wa maeneo ya Vingunguti na majirani mmekaribishwa kufika siku hiyo kusherehekea Siku kuu ya Pasaka inayosherehekewa Takribani Dunia nzima ikiwa ni kukumbuka kuzaliwa kwa Kristo. Ulinzi kwa ajili ya mazingira Said alisema kuwa umeandaliwa wa kutosha Mwisho.

HIA ENDI ZEA


WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU JIJINI MWANZA.


Hawa ni watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Jijini Mwanza - Tanzania. Wadau wa haki za watoto mnasemaje hapa?

USA Yafikiria Kutuma Ndege Za kivita Kusaidia Serikali Ya Somalia

Marekani inafikiria kutuma ndege zake za kipelelezi zijulikanazo kama "drones" pamoja na vifaa vingine vya kivita nchini Somalia ili kuisaidia serikali ya nchi hiyo katika vita vyake na wapiganaji wa Al-Shabaab wanaosadikiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda.
Ndege hizi za drones huongozwa na marubani ambao hubakia ardhini; na pamoja na mafanikio yake makubwa katika vita vya Iraq, Afghanistan na Pakistan, mara nyingi pia zimekosea shabaha na kusababisha maafa makubwa kwa raia.
Inavyoonekana Wamarekani hawataki kupeleka wanajeshi wao katika uwanja wa mapambano huko Mogadishu. Pengine bado wanakumbuka kisa cha mwaka 1993 ambapo wanajeshi wake 18 waliuawa na hatimaye kuwafanya wafungashe virago kwa haraka haraka na kuondoka.
Naamini kwamba tatizo la Somalia ni letu Waafrika na kama kweli tungekuwa na nia ya dhati la kulitatua tungeweza

Rubani aliyeko ardhini akiwa anaendesha ndege hizo

Thursday, April 1, 2010

BREKING NYUUUUUZZZZZ: ZE FULANAZZZZ KWISHNEI


BAADA YA KUENDELEZA LIBENEKE KWA TAKRIBAN MIAKA MINNE MFULILIZO BILA KUCHOKA, HATIMAYE LEO ZE FULANAZZZ YA GLOBU YA JAMII IMECHUKULIWA RASMI KUTOKA KWA ANKAL NA KUWEKWA PEMBENI TAYARI KWA KUPIGWA MNADA ILI KUCHANGISHA PESA ZA MAENDELEO YA WADAU.

KAMPUNI YA USAFIRISHAJI MIZIGO YA HILLVIEW FAMILY COMPANY LIMITED ILIYOKO READING, UINGEREZA, IMEINUNUA ZE FULANAZZZ KWA PAUNI 1,000 ILI KUINADI NA KUCHANGIA MABLOGA KUENDELEZA LIBENEKE KWA UFANISI ZAIDI.
SIKU YA MNADA UTAOFANYIKA ONLINE ITATAJWA KARIBUNI, NA MABLOGA WANAOTAKA KUNUFAIKA NA LIBENEKE LA MNADA WA ZE FULANAZZZZ WANATAKIWA WALETE MAOMBI YA MSAADA NA EMAIL ADDRESS ZAO KUPITIA issamichuzi@gmail.com ILI KUWEZA KUFIKIRIWA NA JOPO LA GLOBU YA JAMII NA WATAALAMU WA HILLVIEW FAMILY COMPANY.
JUMLA YA MABLOGA WACHANGA 10 WATANUFAIKA NA MPANGO HUU AMBAPO WATAPATIWA LAPTOPS, MODEM ZA INTERNET PAMOJA NA PESA ZA AIRTIME YA INTERNET YA MIEZI MITATU ILI KUWAWEZESHA KUANZIA KAZI. MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI APRILI 10, 2010. MPANGO HUU UNAMHUSU BLOGA YEYOTE MCHANGA POPOTE ALIPO DUNIANI.

PICHANI ANAONEKANA ANKAL AKIKABIDHI ZE FULANAZZZ KWA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HILLVIEW FAMILY BW. HASSAN ABDULLAH JIONI HII HUKO READING BAADA YA KUTOA KIASI HICHO CHA PESA HUKU WAKISHUHUDIWA NA WADAU GARDOL NA MAALIM ABDULLAH AMBAYE NI MWEKA FEDHA YA KAMPUNI.

PAMOJA NA KUSIKITIKA KWA KUIKOSA ZE FULANAZZZ AMBAYO IMEKUWA KAMA NEMBO KUU YA GLOBU YA JAMII, ANKAL AMEISHUKURU HILLVIEW FAMILY COMPANY LIMITED KWA KUJITOLEA KUSAIDIA MAENDELEO YA LIBENEKE NDANI NA NJE YA TANZANIA.

HILLVIEW COMPANY NI KAMPUNI INAYOSAFIRISHA MIZIGO YA AINA YOYOTE DUNIANI KUTOKA UK KWA MIAKA 15 SASA. INAPATIKANA:
UNIT 13,
ACCESS STORAGE CENTRE
62 PORTMAN ROAD
READING
BERKSHIRE
RG30
1EA

SIMU NAMBA: 0118 957 6667
FAX: 0118 907 6241
WEB: http://www.hillviewfamilycompany.com/

--------------------------------------------

Napenda kuchukua nafasi hii kutuma maombi yangu kama mmoja wa Mablogga wachanga wanaotaka kunufaika na mpango uliofadhiliwa na HILLVIEW FAMILY kwa kushirikiana na BLOG YA JAMII. Kama ujuavyo sisi mablogga wachanga moja ya changamoto tunayopata ni ukosefu wa vitendea kazi kama Computer, Modem na hata wakati mwingine pesa ya kuweka balance kwa ajili ya kutuma post za kila siku. Hii inapelekea Mablogga wengi kushindwa kuendeleza Blog matokeo yake Libeneke kuishia njiani au kutuma post moaj kwa wiki hata wakati mwingine kwa mwezi kutokana na hali ngumu.
Hivyo mpango huu wa kusaidia mablogga wachanga ambao umefadhiliwa na HILLVIEW FAMILY na BLOG YA JAMII ni sehemu ya kuleta maendeleo kwetu sisi mablogga ili kuendeleza libeneke la kukuza sekta ya habari na mawasiliano.
Ni matumaini yangu kuwa ombi langu litasikilizwa.

Wako katika kuendeleza libeneke
teknohabari webmaster

KALLEY PANDUKIZI

http://teknohabari.blogspot.com/

-----------------------------------------

kwa wadau wote wa Glob ya Jamii.
Maombi yangu ni kwamba hii fulanazi ya jamii ambayo Issa alikuwa ana ivaa ipelekwe makumbusho ya Taifa kwa kuweka kumbukumbu katika jamii kuhusu mchango mkubwa wa Issa Michuzi katika jamii ya kitanzania. Iwekwe na kuambatanishwa na historia ya maisha yake tangu michuzi alipoanzia na kufika hapa alipo. ni watu wachache sana ambao wameweza kuwaunganisha watanzania wote kwa kutumia mtandao kama huu. Michuzi ni mtu ambaye jamii ya Kitanzania hasa ya Diaspora haita msahau hata kidogo. Ametufanya tufamiane kama tuna kaa nchi moja. Leo hii jambo linatokea Tanzania au Japan tayati tuna jua na kuona picha na video. huu ni mchango mkubwa sana. Na vile vile bila kusahau roho ya unyenyekevu wa michuzi aliyo nayo kwa watu wote na ukaribu wake wa watu wa hali zote. Naomba hii " the fulanazi" ipelekwe makumbusho ya taifa.

Mdau
USA.

Makamba, Mkuchika Waitema CCM na kurukia CCJ!



Siku Mbili baada ya Mbunge wa Kishapu Fredy Mpendazoe kutangaza kuhamia CCJ, Viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Yusuf Makamba ambaye ni Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake George Huruma Mkuchika wamekihama chama hicho na kufuata upinzani.

Hatua hiyo ya kukihama CCM wameifika jana kwa nyakati tofauti na kuahidi kuleta maendeleo makubwa huko walipo.
leo siku ya wajinga.

Kufuatia hali hiyo lile ambalo lilisemwa na CCJ kuwa vigogo wengi wa CCM watahamia huko limeanza kudhhirika rasmi.