Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, April 1, 2010

BREKING NYUUUUUZZZZZ: ZE FULANAZZZZ KWISHNEI


BAADA YA KUENDELEZA LIBENEKE KWA TAKRIBAN MIAKA MINNE MFULILIZO BILA KUCHOKA, HATIMAYE LEO ZE FULANAZZZ YA GLOBU YA JAMII IMECHUKULIWA RASMI KUTOKA KWA ANKAL NA KUWEKWA PEMBENI TAYARI KWA KUPIGWA MNADA ILI KUCHANGISHA PESA ZA MAENDELEO YA WADAU.

KAMPUNI YA USAFIRISHAJI MIZIGO YA HILLVIEW FAMILY COMPANY LIMITED ILIYOKO READING, UINGEREZA, IMEINUNUA ZE FULANAZZZ KWA PAUNI 1,000 ILI KUINADI NA KUCHANGIA MABLOGA KUENDELEZA LIBENEKE KWA UFANISI ZAIDI.
SIKU YA MNADA UTAOFANYIKA ONLINE ITATAJWA KARIBUNI, NA MABLOGA WANAOTAKA KUNUFAIKA NA LIBENEKE LA MNADA WA ZE FULANAZZZZ WANATAKIWA WALETE MAOMBI YA MSAADA NA EMAIL ADDRESS ZAO KUPITIA issamichuzi@gmail.com ILI KUWEZA KUFIKIRIWA NA JOPO LA GLOBU YA JAMII NA WATAALAMU WA HILLVIEW FAMILY COMPANY.
JUMLA YA MABLOGA WACHANGA 10 WATANUFAIKA NA MPANGO HUU AMBAPO WATAPATIWA LAPTOPS, MODEM ZA INTERNET PAMOJA NA PESA ZA AIRTIME YA INTERNET YA MIEZI MITATU ILI KUWAWEZESHA KUANZIA KAZI. MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI APRILI 10, 2010. MPANGO HUU UNAMHUSU BLOGA YEYOTE MCHANGA POPOTE ALIPO DUNIANI.

PICHANI ANAONEKANA ANKAL AKIKABIDHI ZE FULANAZZZ KWA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HILLVIEW FAMILY BW. HASSAN ABDULLAH JIONI HII HUKO READING BAADA YA KUTOA KIASI HICHO CHA PESA HUKU WAKISHUHUDIWA NA WADAU GARDOL NA MAALIM ABDULLAH AMBAYE NI MWEKA FEDHA YA KAMPUNI.

PAMOJA NA KUSIKITIKA KWA KUIKOSA ZE FULANAZZZ AMBAYO IMEKUWA KAMA NEMBO KUU YA GLOBU YA JAMII, ANKAL AMEISHUKURU HILLVIEW FAMILY COMPANY LIMITED KWA KUJITOLEA KUSAIDIA MAENDELEO YA LIBENEKE NDANI NA NJE YA TANZANIA.

HILLVIEW COMPANY NI KAMPUNI INAYOSAFIRISHA MIZIGO YA AINA YOYOTE DUNIANI KUTOKA UK KWA MIAKA 15 SASA. INAPATIKANA:
UNIT 13,
ACCESS STORAGE CENTRE
62 PORTMAN ROAD
READING
BERKSHIRE
RG30
1EA

SIMU NAMBA: 0118 957 6667
FAX: 0118 907 6241
WEB: http://www.hillviewfamilycompany.com/

--------------------------------------------

Napenda kuchukua nafasi hii kutuma maombi yangu kama mmoja wa Mablogga wachanga wanaotaka kunufaika na mpango uliofadhiliwa na HILLVIEW FAMILY kwa kushirikiana na BLOG YA JAMII. Kama ujuavyo sisi mablogga wachanga moja ya changamoto tunayopata ni ukosefu wa vitendea kazi kama Computer, Modem na hata wakati mwingine pesa ya kuweka balance kwa ajili ya kutuma post za kila siku. Hii inapelekea Mablogga wengi kushindwa kuendeleza Blog matokeo yake Libeneke kuishia njiani au kutuma post moaj kwa wiki hata wakati mwingine kwa mwezi kutokana na hali ngumu.
Hivyo mpango huu wa kusaidia mablogga wachanga ambao umefadhiliwa na HILLVIEW FAMILY na BLOG YA JAMII ni sehemu ya kuleta maendeleo kwetu sisi mablogga ili kuendeleza libeneke la kukuza sekta ya habari na mawasiliano.
Ni matumaini yangu kuwa ombi langu litasikilizwa.

Wako katika kuendeleza libeneke
teknohabari webmaster

KALLEY PANDUKIZI

http://teknohabari.blogspot.com/

-----------------------------------------

kwa wadau wote wa Glob ya Jamii.
Maombi yangu ni kwamba hii fulanazi ya jamii ambayo Issa alikuwa ana ivaa ipelekwe makumbusho ya Taifa kwa kuweka kumbukumbu katika jamii kuhusu mchango mkubwa wa Issa Michuzi katika jamii ya kitanzania. Iwekwe na kuambatanishwa na historia ya maisha yake tangu michuzi alipoanzia na kufika hapa alipo. ni watu wachache sana ambao wameweza kuwaunganisha watanzania wote kwa kutumia mtandao kama huu. Michuzi ni mtu ambaye jamii ya Kitanzania hasa ya Diaspora haita msahau hata kidogo. Ametufanya tufamiane kama tuna kaa nchi moja. Leo hii jambo linatokea Tanzania au Japan tayati tuna jua na kuona picha na video. huu ni mchango mkubwa sana. Na vile vile bila kusahau roho ya unyenyekevu wa michuzi aliyo nayo kwa watu wote na ukaribu wake wa watu wa hali zote. Naomba hii " the fulanazi" ipelekwe makumbusho ya taifa.

Mdau
USA.

No comments:

Post a Comment