Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Showing posts with label Umbea.com.. Show all posts
Showing posts with label Umbea.com.. Show all posts

Monday, April 19, 2010

KIBAKA ANVYOKOSA KOSA KULA KIPONDO


Haya sasa mambo yanapokuwa si mambo pale unapokutwa live na mwenye mali ukitaka kumuibia ukaanza kula kichapo na kwa bahati nzuri unapata msaada wa polisi kama hivi ambapo safari yako ya kituo cha polisi inakuwa rahisi!kijana pichani alijaribu au kuiba kiio cha gari moja halipo pichani ndipo mwenye gari alipotokea na kuanza kumuita mwizi nakula kichapo cha rasha rasha kabla ya kumvaa polisi kama anavyoonekana pichani

Wednesday, April 14, 2010

wachimbaji 8 wahofiwa kufa mgodini


Mwanaharakati wa haki za binadamu wametoa wito wa kumpatia msaada wa haraka mwanaume mmoja anayehjihusisha na mapenzi ya jinsia, aliye gerezani nchini Malawi anayeelezewa kuumwa sana.

Mwanaharakati Peter Tatchell amesema amepokea taarifa kutoka gereza la Chichiri kwamba Steven Monjeza anayeendelea na kesi ya uhusiano wake wa kimapenzi na mwanaume mwenzake, hajatibiwa na amekuwa akitapika na kulalamika maumivu ya kifua kwa zaidi ya siku kumi.

Taarifa zaidi zimesema anazuiliwa katika jela yenye msongamano mkubwa na ni chafu.

Monjeza na mpenzi wake Tiwonge Chimbalanga, wanashtakiwa kwa kuikuka sheria iliyowekwa nchini Malawi inayopiga marufuku ndo za watu wa jinsia moja .

Wapenzi hao walifanya sherehe ya ndoa yao mwezi wa Desemba na wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha mika kumi na minne jela ikiwa watapatikana na hatia.

Tuesday, April 13, 2010

SAFU YA VIBURUDISHO!

WADAU WA UMBEA.COM HII NI SAFU MPYA KABISA KWA BLOGU HII NA IKIWA NI YA KWANZA KWA KUTOA FURSA YA WADAU WAKE KUCHAGUA NYIMBO WANAYOTAKA WAWEKEWE KWA BLOGU BILA YA MALIPO YOYOTE YALE!HIVYO BASI WEWE UKIWA KAMA MDAU WA UMBEA.COM NAULIPENDA UEKEWE NYIMBO YAKO UNAYOIPENDA KWA BLOGU IWE NI YA AINA YOYOTE ILE TUMA EMAIL KWA innolyimo24@yahoo.com ukinipa jina la nyimbo!

IMETOLEWA NA UMBEA.COM!

Exclusive Akamatwa Live Gesti na Denti wake!



Mwalimu wa Shule ya Sekondari Muhanga, iliyopo Tabata Kinyerezi, Dar, Lucas Yusuph a.k.a Ticha Leizer, juzi alijikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kukutwa ndani ya gesti akiwa na mwanafunzi wake wa kidato cha tatu (Jina linahifadhiwa).

Ijumaa Wikienda a.k.a the Biggest IQ Paper ndilo pekee lenye kuthubutu kuwa la kwanza kulianika tukio hilo ambalo lilichukua nafasi Ijumaa iliyopita (Aprili 9, 2010) ndani ya kuta za Mori Guest, Sinza, Dar na kusindikizwa na timbwili zito.


.....jamani nilikuwa namfundisha hesabu za square...square..!!

Awali, gazeti hili lilipata malalamiko kutoka kwa familia ya mwanafunzi huyo kuwa binti yao amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa walimu mbalimbali, hali inayomsababishia aathirike kisaikolojia na kushindwa kufanya vizuri katika masomo yake.

Walisema kuwa, kutokana na mazingira hayo wamekuwa wakilazimika kumhamisha kutoka shule moja hadi nyingine lakini haikuweza kumsaidia kwani hata alipofika katika shule Muhanga, aliendelea kupata usumbufu kutoka kwa walimu wakware.

“Kwakweli tumechoshwa na usumbufu ambao umekuwa akipata binti yetu kutoka kwa walimu wakimtaka kimapenzi. Tumekuwa tukimgharamia pesa nyingi ili aweze kusoma lakini walimu wamekuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo yake.

“Wanamchapa na kumpa adhabu nzito ikiwa ni pamoja na kumfelisha kwa makusudi kwenye mitihani yake. Hilo lilitokea kwenye shule aliyokuwa akisoma awali, tukamhamishia katika shule hii ya Muhanga ambako nako mambo yamekuwa ni yale yale,” alisema kaka wa binti huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake na kuongeza:
“Kuhusu hili la Mwalimu Leizer, huyu binti yetu amekuwa akimlalamikia kwa muda mrefu akieleza kuwa, amekuwa akimsumbua akimtaka kimapenzi. Licha ya kumkatalia mwalimu huyu amekuwa akimlazimisha na leo amemwambia wakutane katika gesti ya Mori, eti kuna mambo anataka kumwambia, tunaomba mtusaidie ili tuweze kumnasa fataki huyu.”

Kufuatia maelezo hayo, waandishi wetu kwa kushirikiana na wazazi wa binti huyo pamoja Polisi wa Kituo cha Alimaua A, Tandale waliweka mtego ambapo Ijumaa majira ya saa 11 jioni walifanikiwa kumnasa Ticha huyo ‘live’ akiwa na mwanafunzi wake ndani ya chumba namba 1 cha gesti hiyo.

Baada ya fumanizi hilo, mwalimu huyo alijitetea kuwa hakuwa na lengo baya na denti wake na kudai kuwa, walikutana pale ili amfundishe mwanafunzi wake somo la Hisababti.

Hata hivyo, Ticha huyo alipobanwa kuhusu kondomu zilizokuwa kitandani, alishindwa kutoa majibu ya kueleweka.

Vijana wa Mwema ambao wakati huo walikuwa eneo la tukio, walimchukua mwalimu huyo pamoja na mwanafunzi wake hadi Kituo cha Polisi cha Alimaua kwa ajili ya mahojiano.

Ticha Leizer wakati akijieleza, aliruka kimanga kwa kudai kwamba yeye siyo mwalimu na kuongeza kuwa hata binti huyo aliyekuwa naye gesti hakujua ni denti.
Hata hivyo, Ticha huyo alipobanwa kuhusu kondomu zilizokuwa kitandani, alishindwa kutoa majibu ya kueleweka.

Vijana wa Mwema ambao wakati huo walikuwa eneo la tukio, walimchukua mwalimu huyo pamoja na mwanafunzi wake hadi Kituo cha Polisi cha Alimaua kwa ajili ya mahojiano.

Ticha Leizer wakati akijieleza, aliruka kimanga kwa kudai kwamba yeye siyo mwalimu na kuongeza kuwa hata binti huyo aliyekuwa naye gesti hakujua ni denti.
linakemea vikali tabia ya walimu kuwatongoza wanafunzi wao na linaomba taasisi husika kuhakikisha walimu kama hao wanashughulikiwa ipasavyo kwani wamekuwa ni chanzo cha baadhi ya wanafunzi wa kike kufeli katika masomo yao.

Monday, April 12, 2010

RPC anusurika kutekwa Mwanza

KAMANDA wa Polisi mkoani Mwanza, Simon Siro jana amenusurika kutekwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi ambao walikuwa wamemtegea mawe barabarani.

Mtego huo uliwekwa usiku wa kuamkia juzi majira ya saa sita wakati Kamanda huyo alipokuwa katika doria ya usiku akitokea wilayani Sengerema kwenda katika kivuko cha Busisi.

Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio katika kijiji cha Nyitundu kata na tarafa ya Busisi, zimeeleza kwamba baada ya Kamanda Siro kukuta mtego huo alilazimika kushirikiana na askari aliokuwa nao kuyatoa mawe hayo.

“Baada ya kuyakuta mawe hayo walishuka kutoka kwenye gari na kuamua kuyasogeza mawe hayo pembeni mwa barabara na kuendelea na safari yao, lakini inavyoonekana alipatwa na wasiwasi mkubwa,” kilisema chanzo chetu cha habari kutoka katika eneo la tukio.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, baada ya kufika umbali wa kilometa mbili hivi, Kamanda Siro aliwaamuru askari wote kurudi eneo lililokuwa na mtego huo.

“Walipofika katika eneo hilo walikuta mawe waliyoyatoa barabarani yakiwa yamerejeshwa huku wakiwepo watu wawili wenye mapanga, lakini baada ya kuwaona askari walitimua mbio na askari wakiongozwa na Kamanda Siro waliwakimbiza kwa miguu na kufanikiwa kumkamata mmoja wao.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu kutoka wilayani Magu ambako anahudhuria kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamanda Siro alithibitisha kukutana na mtego huo na kuahidi kupambana na wahalifu kwa kila kona ya Mkoa wa Mwanza.

‘Ni kweli ilitokea jana usiku (juzi) kwenye saa sita hivi…..nilikuwa wilayani Sengerema sasa nikaamua kuwachukua vijana wangu ili tufanye doria, nikapita hiyo barabara ya kwenda kwenye kivuko cha Busisi ambapo nina taarifa kwamba kuna eneo moja ambalo majambazi wanapenda sana kuteka magari pamoja na raia,” alisema Kamanda Siro.

“Cha ajabu baada ya kufika kwenye kijiji kimoja kinachoitwa Nyitundu ambapo kuna matengenezo ya barabara ya lami ambayo haijakamilika, tukakuta mawe barabarani, dereva wangu akasimamisha gari tukashuka tukayatoa, ni mawe makubwa,’’ alisema.

Alifafanua kwamba baada ya kwenda umbali kama wa kilometa mbili hivi, alimuamuru dereva wake kusimamisha gari na wakarejea katika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia hali ya usalama.

“Nilichotaka ni kuthibitisha kama kweli yale mawe yalikuwa yamewekwa pale na majambazi, na kweli Mungu si Athumani, tulipofika tu tukakuta yale mawe yamerejeshwa barabarani na kwa bahati nzuri zaidi kukawepo watu wawili kwenye eneo lile.

“Nikaona tayari tumepata kazi ya kufanya, nikawaamuru vijana kufanya kazi ambapo nilishirikiana nao kuwakimbiza watuhumiwa hao na kufanikiwa kumkamata mmoja wao, mwingine alituponyoka,’’ alifafanua Kamanda Siro.

Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, walianza operesheni usiku huo huo katika kijiji hicho kutokana na maelekezo ya mtuhumiwa ambaye walifanikiwa kumkamata ambayo yalifanikisha kuwakamata watuhumiwa wengine wanane ambao wanaendelea kuhojiwa.

Kamanda Siro ametangaza vita na watuhumiwa wote wa ujambazi katika eneo hilo ambalo linasifika kwa matukio ya utekaji wa magari ya abiria na mizigo, na amewataka watuhumiwa kujisalimisha mapema kabla ya msako mkali kuanza katika eneo hilo.

Eneo hilo limekuwa na matukio mengi ya utekaji wa magari ya abiria na yale ya mizigo na hasa malori yanayokwenda nje ya nchi kama vile Burundi, Rwanda na DRC, ambapo mara kadhaa watu wameporwa mali na fedha zao.

Tangu alipohamia mkoani Mwanza, Kamanda Siro ambaye amekuwa akiendesha operesheni za kusaka wahalifu yeye mwenyewe, amekuwa na mikakati kadhaa ya kupambana na uhalifu ambao umekithiri mkoani Mwanza na hasa ujambazi wa kutumia silaha.

Sunday, April 11, 2010

Abiria akosa nauli, amwomba dereva wa teksi “kumla uroda” mkewe



REVA wa teksi wa Bolton, Uingereza, aliambiwa na abiria wake kutoka Poland kwenda “kulala” na mkewe ili kufidia nauli ya Paundi 10.50 ambazo alikuwa anadaiwa, lakini alipokataa ombi hilo, abiria huyo alimfukuza akiwa na panga akitaka kumdhuru.

Dereva huyo mwenye umri wa miaka 38 aliachwa akiwa amepagawa kwa woga wakati abiria wake huyo alipomwamuru kufanya hivyo.
“Nauli ilikuwa ni Paundi 10.50,” alisema dereva huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake na kuongeza, kuwa “jamaa badala ya kulipa aliniambia niingie ndani nyumbani kwake kwenda kulala na mkewe.”

“Katika miaka kumi ya kazi ya udereva, hii ni mara ya kwanza abiria kunipa mkewe nifanye naye mapenzi badala ya kunilipa nauli,” alisema dereva huyo ambaye alikuwa amewachukua abiria wake hao nje ya baa moja huko Bolton, Ijumaa.

Dereva huyo ambaye alishituka kuambiwa hivyo na kisha kupiga king’ora na simu ya kuwaita madereva wengine, alibaini kwamba mwanamume huyo ambaye aliamini ni mtu wa Poland, alikuwa amekimbilia ndani ya nyumba yake na kurejea akiwa na panga lenye urefu wa sentimita 45.

“Aliniijia moja kwa moja na panga lake, ikabidi nichomoke mbio haraka,” alisema dereva huyo aliyekimbia na kumwacha mshambuliaji wake huyo ambapo alipiga simu polisi ambao walifika na kumtia mbaroni mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 37.

Tuesday, March 23, 2010

Msaada tutani jamani!

Wizi kupitia mtandao watinga nchini




Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Afande Abdallah Mssika


JESHI LA POLISI HALINA TAARIFA ZA KUIBWA KWA SHILINGI BILIONI 300 KUTOKA KATIKA MABENKI MBALIMBALI HAPA NCHINI

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limesema halina taarifa za wizi wa shilingi Bilioni 300 zinazodaiwa kuibwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kutoka katika mabenki mbalimbali yaliyounganishwa na mtandao huo hapa nchini.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema jana kuwa taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na wizi huo hazijafikishwa Polisi.

Kamanda Mssika amesema kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Ma
kosa ya Jinai Kamishna Robert Manumba, aliyedaiwa kukaririwa na chombo hicho cha habari, amesema kuwa hana taarifa ya tukio la wizi wa shilingi Bilioni 300.

Kamishna Manumba amesema kuwa mawasiliano kati yake yeye na Mwandishi wa taarifa hiyo kwa upande wake binafsi yalihusu tukio la wizi wa fedha katika benki ya NMB Tawi la Bank House Jijini Dar es Salaam ambapo mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu, ambapo Jeshi la Polisi lilibaini kuibwa kwa shilingi milioni 360 kwa njia ya mtandao wa kompyuta fedha ambazo zilihamishiwa katika tawi moja wapo la benki hiyo lililopo mkoani Shinyanga.
Kamanda Mssika amefafanua kuwa, mara baada ya fedha hizo kufika Mkoani Shinyanga, zilitawanywa kutoka katika tawi hilo na kupelekwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kwenda katika akaunti mbalimbali za watu binafsi kwenye matawi mengine ya benki hiyo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Kutokana na wizi huo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Benki ya NMB limeshafanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 319 kati ya shilingi milioni 360 zilizoibwa na kwamba tayari baadhi ya watuhumiwa waliohusika katika wizi huo wakiwemo watumishi watano wa benki wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu shitaka lao.
Hata hivyo Kamanda Mssika amesema kutokana na taarifa za kuibwa kwa shilingi bilioni 300, kama ilivyoandikwa, ametoa wito kwa Makampuni ama Taasisi za Kifedha zinazoweza kuwa zimefanyiwa hujuma hiyo ya wizi na iwapo rasimu zao za ndani kiuchunguzi zimekamilika, basi wawasiliane na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, ili hatua za uchunguzi ipasavyo kwa kuvishirikisha vyombo vya dola ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Friday, March 19, 2010

UMBEA.COM LEO IKO KAZINI TENA KUWALETEA MAANDALIZI YA UCHAGUZI YANAVYOENDELEA NCHINI TANZANIA,KWA BAHATI NZURI NILIKUTANA NA MBUNGE WA CHUNYA {MH. VICTOR MWAMBALASWA} KULE KWA WANYAKYUSA KUPITIA TIKETI YA C.C.M NA KUFANYA NAE MAHOJIANO MAFUPI JUU YA MKAKATI WAKE NA JINSI GANI ALIVYOJIPANGA JUU YA UCHAGUZI HUU UNAOTARAJIA KUFANYIKA OKTOBA MWAKA HUU!IFUATAYO NI SEHEMU TU YA MAHOJIANO HAYO

UMBEA.COM MZEE ASLAAM ALYEKUM!
MH.MBUNGE,ALYEKUM MUISLAM HABARI YAKO KIJANA

Wednesday, March 17, 2010

KUMBE PENDO ALIKUWA NA MIMBA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mpenzi wa Madee aliyefariki juzi na kuzika jana kule kwao Moshi kumbe amefariki akiwa na mimba ya miezi miwili tumboni. Madee ameniambia hivyo baada yakunipa shukrani zake kwa watu wote waliokuwa na yeye kwa kipindi hiki chote,

Napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru ndugu jamaa na marafiki zangu kwa kujitolea kwao kwa hali na mali katika wakati mgumu niliokua nao. Nashukuru kwa ukaribu wenu kwangu na kunitia moyo sana nakuombea uwe na moyo uwo kila siku.
Tumuombeeni Pendo wangu alale pema pepon, mimi nilimpenda but mungu kampenda zaidi.
Madee.
NA INNO LYIMO

HII NDIO BONGO DAR ES SAALAAM!




Hii ndio Bongo Daslam bwana yaani unachoona hakiwezekani sehemu nyingine,basi hapa kinawezekana .hebu cheki picha hii halafu utapata jibu na kujua nini ninachokiongea.eneo hili silitaji jina wala nini maana najua kabisa kuwa wanafahamu eneo hili.

Thursday, March 4, 2010

AMA KWELI POMBE SIO CHAI!


Kamera yetu imekuta kituko hiki jana majira ya saa 10:00 usiku katika kituo cha mabasi cha Palm beach hotel karibu na daraja la manyoya ambapo kijana huyu alikuwa amepanda basi la Kivukoni kuelekea Mwananyamala,alipokuwa ndani ya basi hilo alikuwa akifanya fujo kutokana na kulewa kupita kiasi ndipo dereva pamoja na kondakta wa basi hilo kuamua kumshusha katika kituo cha mabasi cha palm beach karibu kabisa na tukio la manyoya ili kuondoa kero kwa abiria wengine waliokuwa kwenye basi hilo.




Askari polisi wa kituo cha Salender wakijiandaa kumbeba kijana huyo na kumpeleka hospitalini akiwa hajitambui,UMBEA.COM haikuweza kupata jina la kijana huyo.


Kama kuna mtu yoyote anamfahamu kijana huyu aidha ni ndugu wa kijana huyu aende katika kituo cha polisi cha daraja la Salender atapata taarifa za ndugu yake alipo!

Wednesday, March 3, 2010

THE NORTHERN HIGHLANDS SECONDARY SCHOOL

Hii ni shule ya kutwa na bweni iliyoko mkoani kilimanjaro inatangaza nafasi

SERA YA KILIMO YASHINDIKANA TANZANIA!

Utekelezaji wa dhana ya kilimo kwanza haya ndiyo matunda yenyewe.









Sera Ya kilimo kwanza yashindikana Tanzania kutokana na imani za kishirikina Maeneo yanayo lalamikiwa zaidi ni Tanga na sumbawanga, Serekali yapoteza mabilioni ya fedha na kupata bidhaa zisizokubalika soko la dunia.




Tuesday, March 2, 2010

Ruge mutahaba afafanua madai ya mr ii kuhusu mradi wa zinduka na malaria

Pichani ni mabasi yanayotoa huduma kati ya usafiri katika Kituo kikuu cha Mabasi na Train cha KL Central kwenda uwanja wa ndege wa LCCT hapa Malaysia.

Air Asia ni wadhamini wa Manchester United na mabasi yao yote yamepambwa na picha za Manchester.

Changamoto kwenu watoaji huduma za usafiri Bongo!

BONGO TUTAFIKA LINI LEVEL HII??

Pichani ni mabasi yanayotoa huduma kati ya usafiri katika Kituo kikuu cha Mabasi na Train cha KL Central kwenda uwanja wa ndege wa LCCT hapa Malaysia.

Air Asia ni wadhamini wa Manchester United na mabasi yao yote yamepambwa na picha za Manchester.

Changamoto kwenu watoaji huduma za usafiri Bongo!