WATU watatu wamelipotiwa kufa katika matukio tofauti yaliyotokea juzi jijini Dar es Salaam likiwemoo la mwanamke wa (75) kujinyonga kwa kutumia mtandio
Akiongea na waandishi wa Habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema tukio la kujinyonga lilitokea jana majira ya saa tatu na nusu asubuhi huko Kitunda Machimbo, mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Paulina Nyambega(75) akiwa bafuni amejinyonga kwa kutumia mtandio aliyoutundika kwenye dali la bufu hiyo.
Aidha inadaiwa marehemu alifika nyumbani hapo kwa mkwewe Christine Julius(33) akitokea Tarime miezi miwili iliyopita, hata hivyo awali inadaiwa marehemu aliwahi kutamka kua amebakiza siku chache za kuishi hivyo anataka kugawa urithi kwa watoto wake wote.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Amana na sababu za kupelekea kujinyonga hazijafahamika. Katika tukio jingine, Kamanda Shilogile alisema gari aina la Fuso namba T433ABY aina ya Benz Truck lilimkanyaga kichwa mzoa takataka na kusababisha kifo chake papo hapo.
Akielezea ajali hiyo, Shilogile alisema kua tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku, wakati gari hilo linafanya shughuli za kubeba takataka Manispaa ya Ilala, likiendeshwa na Moses Peter(38) lilipofika barabara ya Morogoro kuelekea Kigogo Sambusa, ghafla mtu mmoja mwanaume ambaye bado hajafahamika kwa jina anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka (20-25) alidondoka chini ya tairi na kukanyagwa kichwa na matairi ya gari hilo na kupelekea kifo chake.
Shilogile alisema kua marehemu alivaa kaptula ya jinsi,fulana nyeusi na raba nyeupe, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili na dereva amekamatwa. Mbali na tukio hilo, Kamanda Shilogile alisema mpita njia mwamke aliyefahamika kwa jina la Honolinda Kimbavala (49), alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari aina ya Scania yenye namba T 567 ACE, iliyokua na trela namba T 227 ABU iliyokua ikiendeshwa na Thomas Isack (26).
Shilogile alisema kua ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu asubuhi katika barabara ya Nyerere eneo la Tazara, Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Temeke na dereva amekamatwa. Katika tukio jingine, mtoto wa siku moja aliokotwa akiwa ndani ya mfuko wa kaki huko maeneo ya Kigamboni magongoni akiwa ametupwa na mwanamke asiyejulikana.
Akiongea na waandishi wa habari, Kamamnda wa Polisi mkoa wa Temeke David Msiime alisema kua tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nne na nusu asubuhi, kichanga hicho kiliokotwa na wapiti njia. Kamanda Msiime alisema kichanga hicho kimehifadhiwa Hospitali ya Muhimbili na hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri. na upelelezi wa kumsaka mwanamke aliyefanya tukio hilo unaendelea.
Habari mbalimbali toka pande za bongo bila kusahau matukio mbalimbali yanayorindima pande zote za dunia
Psquare Ft. J.Martins- E No Easy
Sunday, August 15, 2010
Friday, August 13, 2010
BRAZAMEN ACHANGAMKIA UKOKO WA PILAU KWENYE MAULID

Brazamen Haji (kushoto) akiwa anapakuliwa pilau ambalo baadaye lilitua kwenye Rambo lake.
Na Dunstan Shekidele, Morogoro
KIJANA mmoja smati aliyefahamika kwa jina moja la Haji mkazi wa maeneo ya Nunge mjini hapa, aliwashangaza watu waliohudhuria sherehe ya Maulid ya kumtoa mtoto kufuatia kitendo chake cha kwenda jikoni akiwa na mfuko wa ‘Rambo’ na kuomba atiliwe pilau pamoja na matandu yake ili aende navyo nyumbani kama “take away”.
Paparazi wetu ambaye alikuwa mmoja wa waalikwa mashuhuri hapo alistaajabu kuona kundi la kina mama wakiangua kicheko baada ya kumwona Brazamen huyo akichomoa mfuko wake wa Rambo aliokuwa ameuhifadhi kwenye ‘jeans’ lake na kuomba atiliwe pilau hilo kwenye mfuko huo.
Kijana huyo ambaye alikata mshipa wa aibu alipofika kwenye sufulia la pilau hilo, alimshawishi mpishi amjazie msosi, na mpishi huyo baada ya kuona macho mengi ya watu yakielekezwa kwake, aliamua kutumia ‘Uislamu’ na kumjazia Braza huyo pilau kama wanavyoonekana pichani.
Kocha wa Timu ya Taifa ya Pool kutoka Nchini Zambia Bw. Dennis Lungu atua dar
Kocha wa Timu ya Taifa ya Pool kutoka Nchini Zambia Bw. Dennis Lungu akisalimiana na afisa habari kutoka kampuni ya Integreted Bw. Innocebt Mellek walipokutana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye kijiji cha makumbusho leo katikati ni Mwambata wa Biashara na Masoko katika Ubalozi wa Zambia Nchini Bw Sunday Chikoti.
BAADA ya kilio cha muda mrefu kuhusiana na kocha wa timu za Taifa za Pool table nchini, hatimaye kilio hicho kimesikika baada ya wadhamini wa mchezo huo nchini Safari Lager kukisikia na kuamua kusaidia ujio wa kocha kutoka nchini Zambia.
Kocha huyo kijana Denis Lungu ambaye ana umri wa miaka 27, amesaini mkataba wa miaka miwili ambao umeanza rasmi Agosti Mosi mwaka huu hadi Julai 28 mwaka 2012 huku akihaidi kuibadilisha Tanzania na kuifikisha katika medani za kimataifa kwenye mchezo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha kocha huyo katika mkutano uliofanyika kijiji cha Makumbushi jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TAPA, Amos Kafwinga alisema uamuzi wao wa kumleta kocha huyo unatokana na jukumu walilonalo kama chama ni kuhakikisha wanafanya kila jitihada kuuinua mchezo huo na mojawapo ni kuwa na kocha wa uhakika.
“Lengo la kumleta kocha huyu ni kama inavyoeleza katiba yetu kuwa chama kitasimamia na kuendeleza mchezo wa Pool, hivyo kutokana na jukumu hili ni lazima tuwe na kocha wa uhakika mwenye uwezo mzuri wa kutufikisha kule tunakohitaji.
“ Na kama haitoshi, ni azma ya chama chetu kuhakikisha mchezo huu unachezwa kwa kufuata sheria na viwango vinavyoeleweka ili uwe na ladha hata mtazamaji afurahie kuangalia ili kutekeleza vema azma ya mdhamini wetu bia ya Safari Lager ya kuleta mapinduzi ya kweli na mafanikio makubwa katika mchezo wa Pool nchini” alisema Amos.
Akizungumzia mikakato yake katika kuundeleza mchezo huo nchini, Denis alisema atahakikisha anatumia uwezo wake wa hali ya juu ya kuucheza mchezo huo wa takribani miaka 15 kuhakikisha anaibadilisha Tanzania na kutamba katika medani za kimataifa.
“Matamanio yangu ni kuusogeza mbele na siku za usoni Tanzania itambulike kwenye ramani ya Dunia ya mchezo huo si kwa kuwa washiriki, bali wachezaji wake waweze kuucheza kwa kufuata sheria, kanuni na viwango vya hali ya juu” alisema Denis.Hata hivyo aliwataka viongozi wa mchezo huo na Serikali kwa ujumla kuhakikisha mchezo huo unaasisiwa zaidi shuleni ili watoto waanze kujifunza huko na si kusubiri vijana wa umri wa kati ambao wanatuhusiwa kwenda baa ndio wajifunze maana ndipo meza za mchezo huo zinapopatikana jambo lililochangia mchezo huo kushindwa kupiga hatua za haraka
Wednesday, August 11, 2010
HASHEEM ATUA TENA BONGO
Mchezaji wa Mpira wa kikapu nchini Marekani NBA anayechezea timu ya Memphis Grizzlies, Hasheem Thabeet (pichani) akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kuanza kwa programu ya Basketball Clinic itakayoanza tarehe 12 Agosti kwenye viwanja vya Don Bosco.
Watoto zaidi ya 400 wanatarajiwa kukutana kwenye clinic hiyo ambapo TBF kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Phares Magesa amesema wanatakiwa kujiandikisha katika shule zote zenye vilabu vya Basketball nchini kote.
Lakini pia Hasheem Thabeet ameeleza kwamba katika nchi za Afrika ameshafanya Basketball Clinic kama hizo katika nchi za Nigeria, Senegal, Ivory Coast pamoja na Tanzania kwa sasa, kwa nchi za Asia amefanya programu kama hiyo na mchezaji mwenzake Yao Ming kwa nchi za HongKong, Quatar. Taipei, kulia katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa TBF Phares Magesa.
PICHA: HISANI YA FULL SHANGWE
Sunday, August 8, 2010
Eti-profesa-umechana-kadi-za-wanaccm-walokupotezea.

Wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ludewa wamesikitishwa na kitendo kilichofanywa na mbunge wa zamani wa Jimbo la Ludewa (CCM) Prof. Raphael Mwalyosi wilayani Ludewa cha kuzichana chana kadi za CCM hivi karibuni.
Akishirikiana na wapambe wake - Bw. Boscow Thobias Lingala Lingala, Bw. Obote Msemakweli, Bw. Aulerian Mhagama (Amca) na Bw. Florian Mtweve (Mvanginye) - Prof. Mwalyosi alichana kadi za wanachama wa CCM kata za Ludewa Mjini, Manda na Nkomang’ombe.
Siku mbili kabla ya kura za maoni wapambe wa Prof. Mwalyosi walikuwa wakienda kwenye zile Kata asizokubalika Profesa wakinunua kadi moja ya CCM kwa shilingi 10,000/= mpaka 20,000/= toka kwa wana CCM na kuzichana ili kuwafanya wanachama hao wasipige kura wakihofia kuwa wakifanya hivyo watawapigia wagombea wengine.
Wakati kadi zilizochanwa Manda zilitupwa chooni kadi zilizochanwa Ludewa Mjini zilitupwa kwenye jalala la kilabu cha Pombe za Kienyeji cha Henry kilichopo Ludewa Mjini.
Mtandao huu uliviona vipande vipande vya kadi za CCM viingine vikiwa vimeunguzwa na moto jalalani hapo na vingine vikiwa vimetapakaa pembeni ya jalala hilo.
Wagombea wengine walioshiriki kwenye mchakato wa kura za maoni Jimboni Ludewa ni Injinia Zebadiah Chaula, Bw. Deo Filikunjombe – Kamanda wa Vijana UVCCM (W) na Bw. James Mgaya.
Bw. Allen Ngingo, Katibu Kata wa Kata ya Ludewa Mjini ambako kadi za CCM pia zilichanwa amelaani kitendo kilichofanywa na Mbunge huyo wa zamani (Prof. Mwaloysi).
“Hatukutegemea kama Profesa anaweza kuchana kadi za Chama kilichomweka madarakani kwa miaka mitano,” alilalamika Katibu Kata huyo akiongeza kuwa “Sisi tumekitafsiri kitendo hicho kama ni mbinu mahsusi za kutaka kukihujumu Chama Cha Mapinduzi, kwa maslahi binafsi.”
Lakini pia sisi tumesikitishwa zaidi kuona kuwa baadhi ya walioshiriki kuzichana kadi hizo za CCM ni watumishi wa serikali,” alisema kwa uchungu mwana CCM mwingine mkongwe, Andrew Nyilawila, 75. “Sielewi kabisa; mtumishi wa serikali anawezaje kuchana kadi ya chama tawala?” alihoji Bw. Nyilawila.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ludewa, Mama Magreth Chusi, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa swala hilo linashughulikiwa kiChama ndani ya CCM na kwamba hatua stahiki zitachukuliwa kwa waliofanya hivyo. “Tumelifikisha swala hilo kwenye vyombo husika,” alisema mama Chusi.
ie hupenda kusema, 'siasa si hasa bali visa na mikasa' na ndicho ninachoendelea kukisoma kila kukicha katika vyombo kadha wa kadha vya habari kuhusiana na harakati za uchaguzi mkuu mwaka huu. Pengine utaelewa usemi wangu huo ukishakisoma kisa kilichoandikwa
Katibu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Mary Tesha naye amekiri kuzipokea taarifa za kuchanwa chanwa kwa kadi za CCM jimboni Ludewa.
“Taarifa ambazo nimezipata zimenistua na zimenisonesha sana,” alisema Mary Tesha huku akiongeza kuwa uchunguzi makini unaendelea ili kuwabaini wale waliohusika na vitendo hivyo na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa watakao bainika kuihujumu CCM.
Prof. Raphael Mwalyosi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa (CCM) toka mwaka 2005 hadi 2010 amedondoshwa kwenye kura za maoni na mwandishi wa habari, Bw. Deo Filikunjombe aliyepata ushindi wa kura 7175 huku Prof. Mwalyosi Raphael (6,652), James Mgaya (588) na Chaula Daniel (461).
credit source: http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz0vzy26eJJ
Saturday, August 7, 2010
Lulu ateswa na msururu

Ni supastaa mwenye ‘eji’ ndogo ndani ya Bongo Movies Industry, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amevunja ukimya na kueleza kile kinachoutesa moyo wake, yaani msururu wa midume inayotaka kufaidi penzi lake bila kujali kuwa ni ‘sidanganyiki’, Risasi Jumamosi lina ‘full data’.
Katika mahojiano maalum na ‘pepa’ hili ndani ya ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar, juzi, Lulu aliweka kweupe kwamba, amekuwa akipokea simu za wanaume kati ya 30 hadi 50 kwa siku za kawaida zikimtaka kimapenzi bila kujali kuwa ni siku za kuwa darasani.
“Hiyo ni kwa siku za kawaida yaani Jumatatu hadi Ijumaa, wikiendi ndiyo kabisa kwani simu zinafika hata 60,” alisema Lulu anayetisha katika kiwanda cha filamu Bongo.
Akimiminika bila nukta, koma wala mkato, Lulu alisema kwamba katika maisha yake anahisi ‘usupastaa’ alionao unaelekea kumtokea puani kwani unataka kumvurugia maisha yake ya shule.
Aliliambia Risasi Jumamosi kuwa kinachomshangaza zaidi ni kwamba miongoni mwa midume inayomtongoza ni waume za watu ambao anawafahamu fika kuwa ni wamiliki wa familia.
Alisema: “Jamani naomba nisiwataje kwa majina ili kuwafichia aibu, lakini wengine ni wazee kabisa na mimi ni mjukuu wao. Kwa kweli wanakera na wanatesa.”
Kufuatia hali hiyo, Lulu alisema kuwa analazimika kutotumia lugha chafu ili kutohatarisha maisha yake kwakuwa wanaume hao ni watu wenye uwezo kifedha wanaoweza kumfanyia kitu mbaya na hata kumteka.
Lulu alidai kwamba njia pekee ya kujihami ni kuwa makini na vishawishi vya wanaume hao wapenda ngono.
Mcheza filamu huyo aliyewika na Kundi la Kaole anasema kwamba, mazingira hayo ya kusumbuliwa na wanaume kila anapokatiza yamekuwa yakimpa wakati mgumu ‘boyfriend’ ambaye hakuwa tayari kumwanika hadi atakaporejea mwana wa Mungu kuchukua walio hai na wafu.
Lulu alimalizia kwa kuwaomba wanaume wanaomsumbua kutokana na umaarufu wake waache mara moja ili siku moja wasije wakajikuta wanaangukia pabaya kwakuwa hadi sasa bado ni mwanafuzi a.k.a Sidanganyiki.
Subscribe to:
Posts (Atom)
