Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, August 11, 2010

HASHEEM ATUA TENA BONGOMchezaji wa Mpira wa kikapu nchini Marekani NBA anayechezea timu ya Memphis Grizzlies, Hasheem Thabeet (pichani) akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kuanza kwa programu ya Basketball Clinic itakayoanza tarehe 12 Agosti kwenye viwanja vya Don Bosco.

Watoto zaidi ya 400 wanatarajiwa kukutana kwenye clinic hiyo ambapo TBF kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Phares Magesa amesema wanatakiwa kujiandikisha katika shule zote zenye vilabu vya Basketball nchini kote.

Lakini pia Hasheem Thabeet ameeleza kwamba katika nchi za Afrika ameshafanya Basketball Clinic kama hizo katika nchi za Nigeria, Senegal, Ivory Coast pamoja na Tanzania kwa sasa, kwa nchi za Asia amefanya programu kama hiyo na mchezaji mwenzake Yao Ming kwa nchi za HongKong, Quatar. Taipei, kulia katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa TBF Phares Magesa.


PICHA: HISANI YA FULL SHANGWE

No comments:

Post a Comment