Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, August 7, 2010

Lulu ateswa na msururu


Ni supastaa mwenye ‘eji’ ndogo ndani ya Bongo Movies Industry, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amevunja ukimya na kueleza kile kinachoutesa moyo wake, yaani msururu wa midume inayotaka kufaidi penzi lake bila kujali kuwa ni ‘sidanganyiki’, Risasi Jumamosi lina ‘full data’.

Katika mahojiano maalum na ‘pepa’ hili ndani ya ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar, juzi, Lulu aliweka kweupe kwamba, amekuwa akipokea simu za wanaume kati ya 30 hadi 50 kwa siku za kawaida zikimtaka kimapenzi bila kujali kuwa ni siku za kuwa darasani.

“Hiyo ni kwa siku za kawaida yaani Jumatatu hadi Ijumaa, wikiendi ndiyo kabisa kwani simu zinafika hata 60,” alisema Lulu anayetisha katika kiwanda cha filamu Bongo.
Akimiminika bila nukta, koma wala mkato, Lulu alisema kwamba katika maisha yake anahisi ‘usupastaa’ alionao unaelekea kumtokea puani kwani unataka kumvurugia maisha yake ya shule.

Aliliambia Risasi Jumamosi kuwa kinachomshangaza zaidi ni kwamba miongoni mwa midume inayomtongoza ni waume za watu ambao anawafahamu fika kuwa ni wamiliki wa familia.
Alisema: “Jamani naomba nisiwataje kwa majina ili kuwafichia aibu, lakini wengine ni wazee kabisa na mimi ni mjukuu wao. Kwa kweli wanakera na wanatesa.”


Kufuatia hali hiyo, Lulu alisema kuwa analazimika kutotumia lugha chafu ili kutohatarisha maisha yake kwakuwa wanaume hao ni watu wenye uwezo kifedha wanaoweza kumfanyia kitu mbaya na hata kumteka.
Lulu alidai kwamba njia pekee ya kujihami ni kuwa makini na vishawishi vya wanaume hao wapenda ngono.

Mcheza filamu huyo aliyewika na Kundi la Kaole anasema kwamba, mazingira hayo ya kusumbuliwa na wanaume kila anapokatiza yamekuwa yakimpa wakati mgumu ‘boyfriend’ ambaye hakuwa tayari kumwanika hadi atakaporejea mwana wa Mungu kuchukua walio hai na wafu.

Lulu alimalizia kwa kuwaomba wanaume wanaomsumbua kutokana na umaarufu wake waache mara moja ili siku moja wasije wakajikuta wanaangukia pabaya kwakuwa hadi sasa bado ni mwanafuzi a.k.a Sidanganyiki.

1 comment:

  1. mimi nawaza kwampa wanaweza kumusameya Alikiba ao basi wamupunguzie malipizi yake juu Elizabeth yeye mwenyewe anasema kama hakumushika kwanguvu. Atakama hakingali na miaka chini ya 18. yeye mwenyewe kutaka kwake natena anasema kama ana hakili awezikudanganyika, neno ilo linamaanisha kama chochote kile afanyacho anakijua ndio maana mimi nazungumzia ivo, ila mimi niwazo langu tuu.Mimi napenda sana kufuatilia Habari za Great lakes, sana sana Tanzania na Congo. Haaya nashukuru sana kwa Habari zenu. Mungu atubariki. Naomba munitumie Ukulaso wa 1,2 na 3. Naomba munitumie Number mahalumu ile niweze kupata informations zote. Asanteni sana.

    ReplyDelete