Habari mbalimbali toka pande za bongo bila kusahau matukio mbalimbali yanayorindima pande zote za dunia
Psquare Ft. J.Martins- E No Easy
Monday, September 6, 2010
SINA WATOTO,ILA MAPENZI YANGU YOTE NAYAPELEKA KWA PAKA HAWA...HAWA NI WANANGU.
Anaitwa Bi Fatu Shah,mkazi wa hapa Dar es salaam maeneo ya Temeke mtaa wa Mpole.Bibi huyu amenivuta sana mpaka kuamua kumuweka hapa ni lifestyle yake.Bibi anafuga paka 20 na kuku 16 ambao wote anawalea kama watoto wake.Bibi huyu ana umri wa miaka 84 lakini hakubahatika kupata mtoto hata wa dawa.Hivyo akaamua mapenzi yake kuyaamishia kwa paka na kuku.Bibi anasema paka wana mapenzi sana na wanamfariji na anawapenda kama watoto wake na kuufanya uzee wake uwe na faraja.Anasema kabla hajaanza kufuga hao paka sababu ya mawazo ya kukosa watoto alikuwa mtu mkali na mkorofi mpaka akapachikwa hina la Bi Mkali lakini toka alipoanza kufuga akajikuta anakuwa mtu mwenye amani ndani ya nafsi yake.
Bibi anasema ana mali kibao ana nyumba nyingi tu hapa Dar na pesa,sasa pesa yake kuliko awahudumie binadamu wasio na fadhila ni bora awalee wanyama hao ambao anawaona wanamapenzi na yeye,mchana kutwa akikaa wanakuja kulala miguu kwake kila anakoenda wanamfuata binadamu hawawezi kumfanyia upendo huo.
Anasema hali hiyo imemfanya watu wamfikirie yeye mchawi lakini yeye si mchawi ndivyo alivyoamua kuishi.
Bi Fatu akiwapa chakula paka wake,anasema anahakikisha wamekula wao kwanza ndio yeye ale...kila siku anawapa ugali na samaki au wali na samaki,wakiumwa anajua anawatibu kwa kuwapa panadol,wakiumia anawafunga vidonda.Kuku anao wafuga yeye hata aje mgeni gani hachinjwi anawafuga kwa upendo na si kwa dhumuni la kula nyama.Ikitokea mmoja kafariki kwake ni msiba na anawazika kama binadamu kwa kuchimba shimo nakumfukia.
Paka wamenona hao na wana afya tele duuuuuuuuuuh kila mtu huishi apendavyo ili mradi nafsi yake ina amani na hamkeri wala kumbugudhi mtu.Niliposoma hii story kwenye Mwananchi la ijumaa ya tarehe 23 iliyokuwa imeandikwa na Bi Florence Majani nikavutiwa sana kujua zaidi.Asante sana Florence kwa ushirikiano wako mwenyezi mungu akujaalie katika kazi zako na pilikapilika zako za kutafuta habari.
Hali ni shwari Msumbiji baada ya ghasia

Taarifa kutoka Msumbiji zinasema sehemu kubwa katika mji mkuu, Maputo, kwa sasa ni shwari baada ya ghasia za wiki iliyopita ambazo zilisababisha watu kumi kufariki na wengine takriban mia tatu kujeruhiwa.
Ghasia hizo zilitokana na maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mkate na bidhaa nyinginezo kwa kiwango kikubwa.
Katika baadhi ya matukio, polisi walitumia risasi za mpira dhidi ya waandamanaji.
Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu katika mji mkuu, Americo Ubisse, alisema kuna wasiwasi wa ghasia kuzuka tena siku ya Jumatatu, wakati ujumbe wa simu za mkononi ukisambazwa kwa watu ili wafanye mgomo
Ujumbe kama huo ulitumiwa kabla ya kuzuka kwa ghasia za juma lililopita.
HII NDIYO SURA HALISI YA AFRIKA

AFRIKA ni bara linaloongoza kwa kuwa na sura za umaskini hasa ule unaowafanya binadamu kukosa kile alichokiita Abraham Maslow haki za msingi yaani chakula, malazi na mavazi. Nimepita hapa na kukuta taarifa na picha hii ambayo kwangu haijanifurahisha.
Haki chakula ni jambo ambalo nimekuwa nikilizungumza sana na ninatamai siku moja kila mwananchi kwa kuanza na Tanzania apate haki hii ya msingi. Kama tukikubali kurejesha sera za vitendo katika kilimo bila shaka tutamudu kuwezesha watu wetu kupata chakula wakati wote.
tunafahamu kuwa wakishapata chakula kiasi cha kushiba ni jukumu la pili kusisitiza juu ya chakula bora. Wimbo wa chakula bra hauwezi sasa kuimbw ana serikali yetu kwa kuwa hata haki ya chakula tu kwa wananchi bado ni kitendawili. Kuna waziri wa Kilimo nchini anaitwa Wassira, ni maarufu sana kwa maneno matamu lakini utendaji wa wizara hiyo katika kutibu tatizo la upatikanaji wa chakula bado ni ndoto takayohukua siku nyingi kupata jibu. Tunasubiri sijui aje nani ili kuhamaisha kilimo cha chakula katika Afrika? Inakera na kuumiza sana!
Nguvu kwenye Kampeni, watu wenyewe walemavu!


Pengine walemavu hawa wametaka kumwona Raisi kwa muda mrefu na kutokana na msururu wa ngazi za kupitia hadi kumwona imeshindikana, basi wakaona hapa ndipo penyewe pa kufikisha yaliyowajaa moyoni. Ni kweli kuwa si kila mtu anayetaka kumwona Raisi atafanikiwa kufanya hivyo, lakini wapo wachache ambao hupewa kipaumbele, inategemea na uzito wa hitaji lao, lakini pia hali yao kimaumbile ni kipaumbele.
Mbona wapo wengi tu wenye ulemavu wamemwona Raisi na kupewa misaada kama vile baiskeli na pikipiki? Basi na hawa wangesaidiwa hivyo, lakini si kuwanyanyua vile kama vifaa bwana, wakati wao binadamu tena wanaohitaji msaada kutokana na ulemavu wao. Imenisikitisha!
Wakati mwingine vyanzo vya machafuko na ugomvi katika jamii vimelalamikiwa sana kuwa vyatokana na matumizi makubwa ya silaha na nguvu zisizowiana na tatizo lenyewe. Punguzeni 'madoido' na 'kujidai' walao kidogo. Katika mafunzo yenu nadhani mnapitia kozi ya saikolojia, basi fahamuni kuwa saikolojia ya wananchi kwa wakati huu wa kampeni na kuchagua viongozi wao, wananchi kidogo 'wamecharuka' lakini haijafikia kiwango kisichodhibitiwa (an unmanagable level) hivyo msiwatibue zaidi mwishowe mkazusha majibizano.
Subscribe to:
Posts (Atom)

