Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, September 6, 2010

SINA WATOTO,ILA MAPENZI YANGU YOTE NAYAPELEKA KWA PAKA HAWA...HAWA NI WANANGU.Anaitwa Bi Fatu Shah,mkazi wa hapa Dar es salaam maeneo ya Temeke mtaa wa Mpole.Bibi huyu amenivuta sana mpaka kuamua kumuweka hapa ni lifestyle yake.Bibi anafuga paka 20 na kuku 16 ambao wote anawalea kama watoto wake.Bibi huyu ana umri wa miaka 84 lakini hakubahatika kupata mtoto hata wa dawa.Hivyo akaamua mapenzi yake kuyaamishia kwa paka na kuku.Bibi anasema paka wana mapenzi sana na wanamfariji na anawapenda kama watoto wake na kuufanya uzee wake uwe na faraja.Anasema kabla hajaanza kufuga hao paka sababu ya mawazo ya kukosa watoto alikuwa mtu mkali na mkorofi mpaka akapachikwa hina la Bi Mkali lakini toka alipoanza kufuga akajikuta anakuwa mtu mwenye amani ndani ya nafsi yake.

Bibi anasema ana mali kibao ana nyumba nyingi tu hapa Dar na pesa,sasa pesa yake kuliko awahudumie binadamu wasio na fadhila ni bora awalee wanyama hao ambao anawaona wanamapenzi na yeye,mchana kutwa akikaa wanakuja kulala miguu kwake kila anakoenda wanamfuata binadamu hawawezi kumfanyia upendo huo.
Anasema hali hiyo imemfanya watu wamfikirie yeye mchawi lakini yeye si mchawi ndivyo alivyoamua kuishi.
Bi Fatu akiwapa chakula paka wake,anasema anahakikisha wamekula wao kwanza ndio yeye ale...kila siku anawapa ugali na samaki au wali na samaki,wakiumwa anajua anawatibu kwa kuwapa panadol,wakiumia anawafunga vidonda.Kuku anao wafuga yeye hata aje mgeni gani hachinjwi anawafuga kwa upendo na si kwa dhumuni la kula nyama.Ikitokea mmoja kafariki kwake ni msiba na anawazika kama binadamu kwa kuchimba shimo nakumfukia.


Paka wamenona hao na wana afya tele duuuuuuuuuuh kila mtu huishi apendavyo ili mradi nafsi yake ina amani na hamkeri wala kumbugudhi mtu.Niliposoma hii story kwenye Mwananchi la ijumaa ya tarehe 23 iliyokuwa imeandikwa na Bi Florence Majani nikavutiwa sana kujua zaidi.Asante sana Florence kwa ushirikiano wako mwenyezi mungu akujaalie katika kazi zako na pilikapilika zako za kutafuta habari.

No comments:

Post a Comment