Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, September 6, 2010

Nguvu kwenye Kampeni, watu wenyewe walemavu!
Pengine walemavu hawa wametaka kumwona Raisi kwa muda mrefu na kutokana na msururu wa ngazi za kupitia hadi kumwona imeshindikana, basi wakaona hapa ndipo penyewe pa kufikisha yaliyowajaa moyoni. Ni kweli kuwa si kila mtu anayetaka kumwona Raisi atafanikiwa kufanya hivyo, lakini wapo wachache ambao hupewa kipaumbele, inategemea na uzito wa hitaji lao, lakini pia hali yao kimaumbile ni kipaumbele.

Mbona wapo wengi tu wenye ulemavu wamemwona Raisi na kupewa misaada kama vile baiskeli na pikipiki? Basi na hawa wangesaidiwa hivyo, lakini si kuwanyanyua vile kama vifaa bwana, wakati wao binadamu tena wanaohitaji msaada kutokana na ulemavu wao. Imenisikitisha!

Wakati mwingine vyanzo vya machafuko na ugomvi katika jamii vimelalamikiwa sana kuwa vyatokana na matumizi makubwa ya silaha na nguvu zisizowiana na tatizo lenyewe. Punguzeni 'madoido' na 'kujidai' walao kidogo. Katika mafunzo yenu nadhani mnapitia kozi ya saikolojia, basi fahamuni kuwa saikolojia ya wananchi kwa wakati huu wa kampeni na kuchagua viongozi wao, wananchi kidogo 'wamecharuka' lakini haijafikia kiwango kisichodhibitiwa (an unmanagable level) hivyo msiwatibue zaidi mwishowe mkazusha majibizano.

No comments:

Post a Comment