Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, September 19, 2010

PRESIDENT JAKAYA AMPIGA TAFU LOWASSA MONDULI


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Monduli mkoani Arusha, Edward Lowasa, kwa wapiga kura wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa kampeni jana jioni.


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dr.Jakaya Kikwete, akihutubia wananchi wa jimbo la Monduli mkoani Arusha jana jioni.

Friday, September 17, 2010

mtangazaji wa radio free afrika avamiwa,ajeruhiwa vibaya.!


MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRIKA AMBAYE VILEVILE YU PRODUCER WA KUREKODI MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NDANI YA TETEMESHA PRODUCTION SANDU GEORGE MPANDA MAARUFU KWA JINA LA KID BWAY AMEVEMIWA NA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI.

TAARIFA ZINASEMA KUWA KID BWAY AKIWA NYUMBANI KWAKE LUMALA JIJINI MWANZA, JAMAA ALIYEMVANIA ALIFIKA NYUMBANI HAPO MAJIRA YA SAA 2:30 USIKU NA KUJITAMBULISHA KAMA MSANII AKIHITAJI KUFANYA RECORDING, BAADA YA MAZUNGUMZO NA KUJITAMBULISHA ALIKARIBISHWA NDANI HADI CHUMBA CHA KUREKODIA STUDIO.

NYUMBANI KWA MTANGAZAJI HUYO ANAISHI NA JAMAA ZAKE WAWILI AMBAO WAKATI KID AKIMKARIBISHA MTENDA UHALIFU HUO NYUMBANI HAPO JAMAA HAO WALIMWONA KIJANA HUYO KISHA KILA MMOJA AKAINGIA CHUMBANI KWAKE. DAKIKA KADHAA WAKASIKIA KWA KIPINDI KIREFU SPIKA ZA STUDIO ZIKIKOROMA ISIVYO KAWAIDA NA KUANZA KUDADISI HUKU WAKIMWITA KID BWAY KUWA INAKUWAJE! WAKAITA NA KUITA NDIPO WALIPO AMUA KUINGIA STUDIO NA KUMKUTA SAKAFUNI KAANGUKA DABU ZIKIMTOKA MASIKIONI, PUANI NA KWENYE MAJERAHA SEHEMU ZA KICHWA.

KWA HIVI SASA KID YUPO HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO AKIWA HOI HAJITAMBUI YAANI KAPOTEZA FAHAMU, ALITUNDIKIWA DRIPU YA MAJI IKIWA NI HUDUMA YA KWANZA AMBAYO AMEPATIWA JANA MARA BAADA YA KUFIKA HOSPITALINI HAPO AKISUBIRI KIPIMO CHA T SCAN KUONA KWA UNDANI ZAIDI SEHEMU ALIZODHURIKA. HAKUNA TAARIFA YOYOTE YA UPOTEVU WA MALI HALI INAYOPELEKEA WADADISI WA MAMBO KUDHANI KUWA YAWEZEKANA KULIKUWA NA VITA YA KICHINI CHINI AKA BIFU(AMBAYO HAIJAFAHAMIKA).

UCHUNGUZI KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI UNAENDELEA KUJUA NINI SABABU ZA UVAMIZI HUO.

TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUKUJULISHA.
TWAMWOMBA MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU BROTHER UPATE KUPONA.


Habari hii ni kwa hisani ya mdau G Sengo.

NIACHENI JAMANI NIMECHOKA


Jamaa huyu amenaswa na kamera yetu maeneo ya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam akiuchapa usingizi mchana wa leo kama ambavyo anaonekana baada ya mihangaiko ya hapa na pale ya kutafuta maisha.

Nakaaya Sumari aikacha CHADEMA, ajiunga CCM!


Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini ambaye alikuwa Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha, Nakaaya Sumari, jioni hii ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nakaaya katangaza hayo jioni hii mbele ya mgombea urais wa CCM,Dr. Jakaya Kikwete katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati wa mkutano wa kampeni za Wilaya ya Arumeru

Wednesday, September 15, 2010

LULU ALEWA CHAKARI SIKU YA IDD MOSI!!




Awali wawili hao walikutwa na kamera yetu ndani ya Ukumbi wa Sun Sirro uliopo Shekilango Ubungo jijini Dar ambapo kulikuwa na uzinduzi wa kundi la Tip Top Connection na baadaye kuibukia katika Klabu Billicanas.

Akiwa ‘Bills’ na ‘shosti’ wake walizidi kugida bia na kadri muda ulivyozidi kusogea mbele ndani ya ukumbi huo, ndivyo Lulu alivyokuwa akionekana kulemewa kimtindo.





Kati ya watu waliokuwa karibu yao ni ‘Pedeshee’ mmoja mwenye asili ya Kihindi ambaye alijipendekeza kwa Lulu kwa kulipia vinywani na vilaji akiwa na lengo la kuondoka na msanii huyo kwenda naye anakokujua yeye.

Hata hivyo, ilifika mahali Lulu alzidiwa na pombe hizo na kuonekana kama vile alikuwa akitaka ‘kuangusha gari’


Ilifikia hatua Lulu aliamua kutafuta sehemu ya kuegemea kutokanana kuzidiwa na pombe na kuinamisha kichwa kulala huku ‘Kanjibai’ huyo akiwa anemmezea mate pembeni yake.

Baadaye msanii huyo aliyekuwa mguu kwa mguu na shostito wake walishtukia mtego wa Pedeshee huyo wa Kihindi na kumtoka kiaina wakimwmabia wanatoka kidogo



Mdosi baada ya kubaini kwamba ameachwa ‘njia panda’ alionekana akizagaazagaa huku na kule kumsaka msanii huyo na shoga yake lakini bila ya mafanikio kwani kwa wakati huo ilishatimu saa kumi na moja kasoro robo alfaajiri ambapo Lulu na shoga yake walichomoka na kuelekea pande za Sinza Makaburini.


‘Shosti’ wake Lulu.

Kamera yetu ilipowakimbiza pande hizo iliwakuta wamepiga kambi kwenye hoteli moja (jina tunalo) na baadaye kuelekea makwao huku wakiwa katika gari aina ya Hiace nyekundu iliyokuwa na wanaume wanne kama mabaunsa wao.

Sunday, September 12, 2010

COCO BEACH YAFURIKA,UANGALIZI WA WATOTO HAUKO MAKINI


Ni katika moja na mbili watu walikuwa wamepozi kwenye mapango wanabadilishana mawazo!hii ni siku ya idd mosi cocobeach

HATA KAMA NI NIA HAITANGAZWI HIVI!!!:::::::


...raha ikizidi jamani ni balaa!...