Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, July 5, 2010

Polisi ajipiga risasi nne kituoni

WIMBI la askari wa Jeshi la Polisi kujiua, limeendelea kushika kasi baada ya askari wa kike WP Suzana, aliyekuwa amepangiwa kuzuia magari ili msafara wa Rais Jakaya Kikwete upite wilayani Tarime mkoani Mara kujiua.

Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, Sebastan Zakari alisema, Suzana alijiua majira ya saa 7.05 mchana ndani ya kituo cha polisi.

“Mimi niko kwenye msafara wa Rais, ni kweli nimepata taarifa kwamba kuna askari wetu wa kike amejiua, baada ya kutoka kwenye eneo lake (pointi), tuliyokuwa tumempangia baada ya msafara wa Rais kupita… sijajua chanzo gani kilichomsibu,” alisema Kamanda Zakaria.

Habari zilizopatikana kutoka Tarime zinasema WP Susana, baada ya kukosea kuelekeza msafara huo, alifuatwa na maafisa usalama wa taifa, ambao walimfokea kisha kuamuru akamatwe na kupelekwa mahabusu kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi.

Chanzo hicho, kinasema kitendo hicho, kilionekana kumkera na kuamua kuchukua bunduki na kujipiga risasi nne kifuani.

Watu walioshududia tuko hilo, walisema askari huyo alikosea kuelekeza magari ya kwanza yaliyokuwa kwenye msafara, ambayo yalitakiwa kwenda eneo la Bomani ambako Rais alitakwenda ili asome taarifa ya wilaya.

Ilidaiwa baada ya kukosea, ndipo alipokamatwa na wenzake kisha kupelekwa kituo kikuu cha polisi Tarime, na kwamba huko alipewa vitisho na wakubwa wake wa kazi kutokana na kosa hilo.

Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Charles Samson, alithibitisha kupokea mwili wa askari huyo na kueleza kuwa alijipiga maeneo ya kifuani na risasi kutokea mgongoni upande wa kushoto ambako ni eneo la moyo.

Tukio ni la pili, kutoka baada ya juzi asubuhi askari polisi ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Tanzania Polisi Academy, Konstebo Nole Paul Njega, kujipiga risasi na kufumua kichwa chake chote, mjini Dar es Salaam. Habari zaidi bofya Hapa

No comments:

Post a Comment