Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, July 5, 2010

waliokuwa katika moto wazikwa congo!


Miili ya watu waliofariki baada ya mlipuko wa trela iliyokuwa imebeba mafuta kuanzisha moto mkubwa katika kijiji kimoja Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imezikwa leo katika makaburi mawili makubwa.
Watu wasiopungua 230 walikufa walikufa baada ya trela hiyo kupinduka na kulipuka, na moto mkubwa kutokea katika kijiji cha Sange.
Baadhi ya wale waliokufa ni watu waliokuwa wakichota mafuta. Lakini wengine waliteketea walipojipata katika mtego, wasiweze kutoka katika majumba, ikiwa ni pamoja na ukumbi mmoja wa filamu ulioshika moto.
Wanajeshi wa kudumisha amani wa Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wa mashirika ya misaada, wamekuwa wakijaribu kuwasaidia waliojeruhiwa katika moto huo.
Kulingana na shirika la habari la Associated Press, siku ya Jumamosi wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu waliibeba miili katika mifuko ya plastiki, hadi katika makaburi mawili makubwa, nje kidogo ya kijiji cha Sange.
Jean-Claude Kibala, gavana wa Kivu ya Kusini, amesema yaliyotokea katika kijiji hicho ni mambo ya kutisha.
"Kuna miili kila mahali barabarani. Wakaazi wote wamo katika hali ya mshituko, hakuna aliye katika hali ya kulia wala kuzungumza kuhusu mkasa huo." Ajali hiyo ilitokea usiku wa Ijumaa.
Kijiji cha Sange kipo mwendo wa kilomita 70 kusini mwa mji wa Bukavu, katika Kivu ya Kusini, karibu na mpaka wa Burundi.
www.bbcswahili.com

No comments:

Post a Comment