Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, March 1, 2010

Habari zilonifikia hivi punde! JUU YA AJALI YA NDEGE YA AIR TANZANIA



PICHA ZOTE ZIKIONYESHA NDEGE HIYO ILIVYOKUWA
Habari kutoka Mwanza zinasema kuwa ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege Tanzania imepasuka matairi mawili ya mbele na kusababisha kizaaa kikubwa kwa abiria wapatao 36 na wafanyakazi 7 waliokuwamo ndani ya ndege hiyo, mapema leo asubuhi. Hali hiyo ilitokea wakati ndege hiyo ikijaribu kutua huku hali ya hewa ikiwa mbaya kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha karibu nchi nzima. Inaelezwa kuwa baada ya matariri ya mbele kupasuka, ndege ilitembelea tumbo kwa mita kadhaa kabla ya kufanikiwa kusimama na abiria pamoja na wafanyakazi wake kutoka salama. Safari za ndege kubwa zimesimamishwa kwa muda uwanjani hapo.
Picha zote na mwandishi wetu jijini mwanza kader adara!

HALI ILIVYOKUWA TETE HUKO LONDON!




JOHN MAKINI NA G NAKO WAVAMIWA NA MAJAMBAZI!


Wasanii wawili wa bongo usiku wakuamkia leo jamaa walikuwa na kazi ya ziada kupambana na majambazi ili kuokoa maisha yao. Majambazi hao walifika eneo la tukio na kuanza kazi zao na hatimae wakachukua simu za hawa majamaa, deki, tv, hela nyingi tu na vingine vingi.
Nilipata nafasi yakuongea na Gnako na Joh Makini ili kujua afya zao na wako poa ila wameniambia lilikuwa kama picha la Rambo aiseee.
Poleni sana ndugu zangu....bora mko poa nashukuru tutachapa kazi na vitu vitarudi kwenye hali yake

Wanafunzi IFM wadakwa na mirungi


POLISI wamewatia mbaroni wanafunzi wawili wa Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Dar es Salaam, kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa na mabunda saba ya mirungi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga amesema, watuhumiwa hao walikamatwa juzi saa 11:30 jioni katika eneo la Coco Beach, Oysterbay.

Aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Mohamed Abdullah (27) na Abdulatif Jabir (27).

Amesema, wanafunzi hao ni wakazi wa Bungoni Ilala, na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Wakati huohuo, mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Chanika, Amani Mwera (12), amekufa baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara.

Mtoto huyo aligongwa juzi saa 12:40 jioni katika barabara ya Mvuti – Chanika, Ilala.

Gari lililomgonga lina namba za usajili T775 BDF Nissan Caravan, lilikuwa likiendeshwa na Shaban Juma (22), mkazi wa Buguruni,alikuwa anatoka Chanika kwenda Mvuti.

Polisi wamemkamata dereva huyo, maiti ya mtoto imehifadhiwa katika Hospitali ya Amana, Dar es Salaam.

MANUNITED YATWAA KOMBE LA CARLING



Manchester United a.k.a The Red Devils ilifanikiwa kutwaa kombe la Carling hapo jana baada ya kuilaza timu ya Aston Villa kwa mabao 2-1. Aston villa walianza kwa kasi nakufanikiwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya tano kupitia kwa mchezaji wake Milner. Hata hivyo bao hilo halikudumu sana kwani katika dakika ya 12 manutd walisawazisha bao hilo kupitia mkongwe Michael Owen. Dakika 16 kabla ya mchezo kumalizika uper striker wa manchester, Wayne Rooney aliingia na kufanya mambo yake na kufanikiwa kupachika bao la pili na la ushindi kwa timu yake. Hongera Manchester United.

MAMBO YA MZALENDO PUB HAYOOOO!!






Walahi ilikuwa uhondo mtupu.Ringi lilikolea,yaani hapo ni full kuduarika bila kusahau mangoma ya uhakika kutoka pande zote za dunia.

HAYA NDO MAMBO YA MAULIDI DAY




haya ndio mambo ya usiku wakati kichwa kiko poa tayari,hii kitu imetokea usiku wa kuamkia leo pale kwenye ile kona matata sana mbele kidogo ya Rose Garden,jijini Dar.katika ajali hii hakudhurika mtu yeyote. Pichani ni Gari dogo aina ya Mitsubishi Pajero,yenye nambari za usajiri T 849 AXC ikiwa imekula mweleka ndani ya mtaro mara baada ya kumzidi ubavu suka wake.