Habari mbalimbali toka pande za bongo bila kusahau matukio mbalimbali yanayorindima pande zote za dunia
Psquare Ft. J.Martins- E No Easy
Friday, June 18, 2010
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA RIADHA VIJANA KANDA YA TANO AFRIKA!!

Timu ya taifa ya riadha ya vijana chini ya umri wa miaka 20 yafanyiwa mchujo.
Mchujo wa kutafuta timu ya taifa ya riadha ya vijana chini ya umri wa miaka 20 watakaoshiriki mashindano ya riadha ya Afrika kanda ya tano yametimua vumbi leo hii kwenye uwanja wa taifa jijini DSM.
Akizungumuza wakati wa mchujo huo katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania (RT) SULEIMAN NYAMBUI amesema Tanzania watakuwa wenyeji wa mashindano hayo na wao watayatumia kwa ajili ya kuunda timu ya taifa ya vijana ambayo baadhi ya wachezaji wake watashiriki katika michezo ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika mjini NEW DELH nchini INDIA MWEZI OKTOBA mwaka huu.
Nao wanariadha waliobuka kidedea katika mbio za mita mia nne, mshindi wa kwanza MOHAM,ED CHARLES wa ARUSHA na mshindi wa pili JOSEPH MSILA wa DSM wamesema watafanya vyema katika mashindano hayo ya vijana ya Afrika kwani wamejiandaa vyema kuibuka na ushindi.
Mashindano ya riadha ya kanda ya tano kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 yampepangwa kufanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 kwenye uwanja wa Taifa na yatashirikisha wanariadha kutoka nchi za MISRI, ETHIOPIA, ERITREA, KENYA, UNGANDA,BURUNDI,RWANDA na wenyeji TANZANIA. Habari na picha kwa hisani ya www.janejohn.blogspot.com
FEDHA ZA SERIKALI ZITUMIKE KWA MALENGO!!

Wabunge wameishauri Serikali kutumia vizuri fedha za barabara ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa fedha zote zinazopelekwa Wilayani kwa ajili ya ujenzi wa barabara zinatumika kwa utaratibu uliopangwa.
Wakichangia hotuba ya Waziri Mkuu Wabunge hao pia wameiomba Serikali kutoa mafungu ya fedha mikoani kwa uwiano unaoweza kuwasaidia wananchi.
Akitoa mchango wake, Mbunge wa Lindi Viti Maalum, Mhe. Riziki Said Lulida amesema, Serikali haina budi kuwa macho na watu wanaoingia hapa nchini kwa kivuli cha wawekezaji kwani wengine huja nchini hata bila mtaji wa kutosha badala yake waletwe wawekezaji wenye uwezo wa uwekezaji.
Mbunge wa Mafia, Mhe. Abdulkarim Shah ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mifugo kuweka utaratibu wa kuwapatia wavuvi nyezo bora katika shguhuli ya uvuvi ili kuinua kiwango chao katika uvuvi.
Wabunge hao pia wameitaka Serikali kuendelea na utaratibu wake wa kutoa mbolea ya ruzuku kwa wakati kwa nchi nzima ili mkulima aweze kuongeza uzalishaji na tija
Wednesday, June 16, 2010
MWAKALEBELA AELEZA MIKAKATI YAKE YA KIMAENDELEO IWAPO ATAMPOKEA MBEGA UBUNGE JIMBO LA IRINGA
KATIBU mkuu wa shirikisho la soka Tanzania Frederick Mwakalebela asema anagombea ubunge jimbo la Iringa mjini ili kumpokea mbunge wa sasa Monica Mbega(CCM) katika mchakato wa kufanikisha maendeleo ya jimbo hilo kama nilivyo fanya ndani ya TFF kwa kipindi kifupi cha uongozi wangu .
Mwakalebela aliyasema hayo leo nyumbani kwake Wilolesi mjini Iringa wakati akitangaza azma yake na sababu za yeye kugombea ubunge jimbo hilo mbele ya waandishi wa habari na wazee wa mji wa Iringa .
Alisema kuwa katika kampeni zake za kuwania nafasi hiyo kamwe hatajaribu kumsema vibaya mgombea mwenzake ndani ya CCM na nje ya CCM kwani amedai kuwa lengo la wagombea wote wa CCM na wale wa upinzani ni kujenga nyumba imara ndani ya jimbo hilo hivyo haoni sababu ya kugombea fito ama kuendesha kampeni chafu za kupakana matope.
Zaidi soma Tanzania Daima kesho ama tembelea http://www.matukiodaima.blogspot.com/ na http://www.mtotobaraka.blogspot.com/
HUJAFA HUJAUMBIKA BADO,HUYU NI MTOTO YATIMA ANATESEKA KWA KUKOSA MSAADA WA MATIBABU
SAKATA LA OFISI KUCHOMWA MOTO MTANDAO HUU WABAINI SIRI NZITO,VIONGOZI WATATA WAKAMATWA
IMEBAINIKA kuwa ukimya wa tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarita Kalalu kuchunguza tuhuma za viongozi wa serikali ya kijiji cha Igowole wilayani humo juu ya ufujaji wa mali za kijiji ndio uliopelekea hujuma kuchomwa moto kwa ofisi hiyo ya na nyaraka zote
Kuchomwa moto kwa ofisi hiyo ya serikali kunadaiwa ni kutokana na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarita Kalalu kuchewesha majibu ya tume aliyokuwa ameiunda kwa ajili ya kuchunguza ufisadi uliokuwa umefanyika katika kijiji hicho na viongozi wa serikali ya kijiji kwa kuuza miti ya kijiji kinyemela na fedha kuzitumia wao katika matumizi binafsi
Akizungumza namtandao huu juu ya tukio hilo mwenyekiti wa tume ya mkuu wa wilaya kijijini hapa Hosea Kyando alisema kuwa kabla ya watu hao wasiofahamika kuchoma moto ofisi ya kijiji juzi usiku mchana waliweka vipande vya sabuni katika mlango wa ofisi ya kaimu afisa mtendaji wa kijiji hicho ambaye ana wiki moja pekee toka aripoti kijijini hapo
Alisema kuwa kutokana na wananchi wa kijiji hicho kuukataa uongozi wa kijiji chini ya mwenyekiti wake Idphonce Kafuka ,mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi alituma wakaguzi kwa ajili ya kukagua hesabu za kijiji hicho ambazo zilikuwa zikilalamikiwa na wananchi hao kiasi cha kufanya maandamano makubwa kuwataka viongozi wote wa kijiji kujiuzulu.
Hata hivyo viongozi hao hawakuweza kujiuzulu zaidi ya mkuu wa wilaya hiyo kuingilia kati suala hilo kwa kuunda tume ya kuchunguza malalamiko ya wananchi tume ambayo iliwasilisha ripoti yake ndani ya muda uliopangwa japo hadi sasa ni siku 14 zimepita bila mkuu wa wilaya kufika na kutoa ripoti ya uchunguzi wa tume hiyo kama alivyoahidi.
Hivyo alisema kuchelewa kutolewa kwa majibu ya tume hiyo ndiko kulikowakwaza zaidi wananchi hao ambao walilazimika kufunga safari hadi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Mohamed Abdulaziz kufikisha malalamiko yao na kuomba tume ya mkuu wa wilaya kutoa majibu yake.
"Hapa kuna mawili yawezekana ni viongozi wanaotuhumiwa wameamua kufanya hujuma ya ofisi ili kupoteza ushahidi...ama yawezekana ni wananchi wameamua kuchoma moto ofisi baada ya kuchukizwa na ukimya wa mkuu wa wilaya dhidi ya tume yake"
Pia alisema wakati moto huo ukiteketeza ofisi juzi usiku kegere iligongwa na wananchi wote waliweza kufika kuzima moto huo ila viongozi hao wa serikali ya kijiji ambao wamekuwa wakipingwa na wananchi hawakuweza kufika hata mmoja .
Mwenyekiti huyo alisema kuwa hadi sasa tayari askari polisi wamefika katika kijiji hicho kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo japo na viongozi watatu akiwemo mwenyekiti na afisa mtendaji wamekamatwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bibi Kalalu alipoulizwa na mwandishi wa habari hii juu ya tume hiyo kuundwa na kushindwa kutolewa majibu kwa wakati alisema kuwa kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam kwa matibabu na hawezi kulizungumzia zaidi suala hilo kutokana na matatizo ya kifanya yanayomsumbua huku mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ya Mufindi Limbaksye Shimwela hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.
Subscribe to:
Posts (Atom)