Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, August 16, 2010

NAWATAKIA RAMADHANI NJEMA NDUGU ZANGU WAISLAM


Waislam duniani wameuanza mwezi mtukufu wa Ramadhan ikiwa ni mojawapo ya nguzo tano katika uislam.Nawatakia kila la kheri katika mwezi huu wa toba nawaombea kwa mungu wafunge salama na mungu awabariki sana. Ramadhan kareem

HAWA NDIO WALIOPEWA KUGOMBEA UBUNGE CCM!!!


Waliopitishwa CCM hadi sasa: TABORA i. Tabora Urban: Ismail RAGE ii. Tabora North: Sumar MAMLO iii. Urambo East: Samuel SITTA iv. Urambo West: Prof. Juma KAPUYA v. Igunga: Rostam AZIZ vi. Sikonge: Said NKUMBA vii. Igalula: Athuman MFUTAKAMBA viii. Bukene: Seleman ZEDI ix. Nzega: Hamis KIGWANGALA IRINGA i. Iringa Urban Monica MBEGA ii. Isimani: William LUKUVI iii. Kalenga: William MGIMWA iv. Kilolo: Prof. Peter MSOLLA v. Ludewa: Deo FILIKUNJOMBE vi. Makete: Dr. Binilith MAHENGE vii. Mufindi North: Mohamed MGIMWA viii. Mufindi South: Menrad KIGOLA ix. Njombe North: Deo SANGA (Jah People) x. Njombe South: Anne MAKINDA xi. Njombe West: Gerson LWENGE ARUSHA i. Arusha: Dr. Batilda BURIANI ii. Arumeru East: Jeremiah SUMARI iii. Arumeru West: Goodluck Ole MEDEYE iv. Karatu: Dr. Wilbald LORRI v. Longido: Michael LAIZER vi. Monduli: Edward LOWASSA vii. Ngorongoro: Saning’o Ole TELELE KAGERA i. Nkenge: Assumpter MSHAMA ii. Bukoba Urban: Khamis KAGASHEKI iii. Bukoba Rural: Jasson RWEIKIZA iv. Muleba North: Charles MWIJAGE v. Muleba South: Anna TIBAIJUKA vi. Chato: John MAGUFULI vii. Kyerwa: Eustace KATAGIRA viii. Karagwe: Gosbert BLANDES ix. Biharamulo: Oscar MUKASA x. Ngara: Deogratias NTUKAMAZINA IGOMA i. Kigoma Urban: Peter SERUKAMBA ii. Kigoma South: Gulam KIFU iii. Kasulu Urban: Neka NEKA iv. Kasulu Rural: Daniel NSANZUGWANKO v. Manyovu: Albert NTABALIBA vi. Buyungu: Christopher CHIZA vii. Muhambwe: Jamal TAMIMU viii. Kigoma North: Rabinson LEMBO KILIMANJARO i. Moshi Urban: Justin SALAKANA ii. Moshi Rural: Dr. Cyril CHAMI iii. Rombo: Basil MRAMBA iv. Same East: Anne MALECELA v. Same West: David DAVID vi. Hai: Fuya KIMBITA vii. Vunjo: Chrispin MEELA viii. Mwanga: Prof. Jumanne MAGHEMBE ix. Siha: Aggrey MWANRI MANYARA i. Babati Urban: Kisyeri CHAMBIRI ii. Babati Rural: Jitu SONI iii. Hanang: Dr. Mary NAGU iv. Kiteto: Benedict Ole NANGORO v. Mbulu: Philip MARMO vi. Simanjiro: Christopher Ole SENDEKA MARA i. Musoma Urban: Vedasto MATHAYO Manyinyi ii. Musoma Rural: Nimrod MKONO iii. Mwibara: Alphaxard LUGOLA iv. Bunda: Stephene WASSIRA v. Rorya: Lameck AIRO vi. Tarime: Nyambari NYANGWINE vii. Serengeti: Dr. Stephene KEBWE MBEYA i. Mbeya Urban: Benson MPESYA ii. Mbeya Rural: Luckson MWANJALA iii. Kyela: Dr. Harrison MWAKYEMBE iv. Mbarali: Dickson KILUFI v. Lupa: Victor MWAMBALASWA vi. Songwe: Philipo MULUGO vii. Rungwe East: Prof. Mark MWANDOSYA viii. Rungwe West Prof. David MWAKYUSA ix. Ileje: Aliko KIBONA x. Mbozi Mashariki: Godfrey ZAMBI xi. Mbozi West: Dr. Luka SIAME MOROGORO i. Morogoro Urban: Aziz ABOOD ii. Morogoro South East: Dr. Lucy NKYA iii. Morogoro South: Innocent KALOGERIS iv. Mvomero: Amos MAKALA v. Ulanga East: Celina KOMBANI vi. Ulanga West: Haji MPONDA vii. Gairo: Ahmed SHABIBY viii. Kilosa: Mustafa MKULO ix. Mikumi: Abdulsalaam SULEIMAN x. Kilombero: Abdul MTEKETA MTWARA i. Mtwara Urban: Murji MOHAMED ii. Mtwara Rural: Hawa GHASIA iii. Masasi: Mariam KASEMBE iv. Lulindi: Jerome BWANAUSI v. Tandahimba: Juma NJWAYO vi. Newala: George MKUCHIKA vii. Nanyumbu: Dunstan MKAPA MWANZA i. Ilemela: Anthony DIALLO ii. Nyamagana: Laurence MASHA iii. Busega: Dr. Kamani MLENGENYA iv. Magu: Dr. Festus Limba v. Kwimba: Sharif MANSOOR vi. Sumve: Richard NDASA vii. Geita: Donald MAX viii. Nyang’wale: Hussein AMAR ix. Sengerema: William NGELEJA x. Buchosa: Charles TIZEBA xi. Misungwi: Charles KITWANGA xii. Ukerewe: Getrude MONGELA. RUVUMA i. Songea Urban: Emmanuel NCHIMBI ii. Peramiho: Jenister MHAGAMA iii. Namtumbo: Vita KAWAWA iv. Tunduru South: Mtutura MTUTURA v. Tunduru North: Ramo MAKANI vi. Mbinga West: Capt. John KOMBA vii. Mbinga East:

Sunday, August 15, 2010

Mtoto Andrea Kipangula ni mtoto yatima kati ya watoto wanaosaidiwa vifaa vya shule na TAWLAE kwa msaada wa USAID/AED/ AGSP.

Ana miaka 10 (kumi) na anasoma darasa la nne (4) katika shule ya Kibao, wilaya ya Mufindi, kwa sasa, kwa masaa anayoweza kumudu anasoma shule ya msingi ya Makuburi, wilaya ya Kinondoni.

Mtoto huyu ana tatizo la kutopata choo kwa muda mrefu kwa vile njia yake ya haja kubwa

inahitilafu. Madaktari wamemfanyia upasuaji mara saba hosipitali ya rufaa ya Muhimbili ili kurekebisha hali yake.

Kwa sasa imebidi atumie utumbo mkubwa kutolea choo ambao upo nje ya tumbo lake, hali ni ngumu kwa mtoto huyu.

Bibi yake ambaye ni mzee sana pamoja na shangazi yake ambaye ni mjane, hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu na maisha.

Wale watakaopenda kusaidia kwa njia ya benki, tafadhali weka katika akaunti namba

0121030000838 ya NBC Samora Branch Dar-es-salaam, ukishaweka tuarifu kupitia simu namba 0754-360215 begin_of_the_skype_highlighting 0754-360215 end_of_the_skype_highlighting au +255(22)2700085 begin_of_the_skype_highlighting +255(22)2700085 end_of_the_skype_highlighting au fax pay in slip ya benki kwenye namba +255(22)2700090 begin_of_the_skype_highlighting +255(22)2700090 end_of_the_skype_highlighting. Vinginevyo tuletee msaada kwenye ofisi zetu zilizopo MARI-MIKOCHENI Plot namba 24 “b” Sam Nujoma Road kuelekea kiwanda cha Cocacola,

Tafadhali tunaomba msaada wako ili kumsaidia.

Aksante.

Mary Liwa

Mkurugenzi wa Miradi

MATUKIO NA HABARI ZA KIPOLISI TOKA JIJINI DAR ES SALAAM

WATU watatu wamelipotiwa kufa katika matukio tofauti yaliyotokea juzi jijini Dar es Salaam likiwemoo la mwanamke wa (75) kujinyonga kwa kutumia mtandio
Akiongea na waandishi wa Habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema tukio la kujinyonga lilitokea jana majira ya saa tatu na nusu asubuhi huko Kitunda Machimbo, mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Paulina Nyambega(75) akiwa bafuni amejinyonga kwa kutumia mtandio aliyoutundika kwenye dali la bufu hiyo.
Aidha inadaiwa marehemu alifika nyumbani hapo kwa mkwewe Christine Julius(33) akitokea Tarime miezi miwili iliyopita, hata hivyo awali inadaiwa marehemu aliwahi kutamka kua amebakiza siku chache za kuishi hivyo anataka kugawa urithi kwa watoto wake wote.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Amana na sababu za kupelekea kujinyonga hazijafahamika. Katika tukio jingine, Kamanda Shilogile alisema gari aina la Fuso namba T433ABY aina ya Benz Truck lilimkanyaga kichwa mzoa takataka na kusababisha kifo chake papo hapo.
Akielezea ajali hiyo, Shilogile alisema kua tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku, wakati gari hilo linafanya shughuli za kubeba takataka Manispaa ya Ilala, likiendeshwa na Moses Peter(38) lilipofika barabara ya Morogoro kuelekea Kigogo Sambusa, ghafla mtu mmoja mwanaume ambaye bado hajafahamika kwa jina anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka (20-25) alidondoka chini ya tairi na kukanyagwa kichwa na matairi ya gari hilo na kupelekea kifo chake.
Shilogile alisema kua marehemu alivaa kaptula ya jinsi,fulana nyeusi na raba nyeupe, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Muhimbili na dereva amekamatwa. Mbali na tukio hilo, Kamanda Shilogile alisema mpita njia mwamke aliyefahamika kwa jina la Honolinda Kimbavala (49), alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari aina ya Scania yenye namba T 567 ACE, iliyokua na trela namba T 227 ABU iliyokua ikiendeshwa na Thomas Isack (26).
Shilogile alisema kua ajali hiyo ilitokea majira ya saa tatu asubuhi katika barabara ya Nyerere eneo la Tazara, Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Temeke na dereva amekamatwa. Katika tukio jingine, mtoto wa siku moja aliokotwa akiwa ndani ya mfuko wa kaki huko maeneo ya Kigamboni magongoni akiwa ametupwa na mwanamke asiyejulikana.
Akiongea na waandishi wa habari, Kamamnda wa Polisi mkoa wa Temeke David Msiime alisema kua tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nne na nusu asubuhi, kichanga hicho kiliokotwa na wapiti njia. Kamanda Msiime alisema kichanga hicho kimehifadhiwa Hospitali ya Muhimbili na hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri. na upelelezi wa kumsaka mwanamke aliyefanya tukio hilo unaendelea.

Friday, August 13, 2010

BRAZAMEN ACHANGAMKIA UKOKO WA PILAU KWENYE MAULID


Brazamen Haji (kushoto) akiwa anapakuliwa pilau ambalo baadaye lilitua kwenye Rambo lake.
Na Dunstan Shekidele, Morogoro
KIJANA mmoja smati aliyefahamika kwa jina moja la Haji mkazi wa maeneo ya Nunge mjini hapa, aliwashangaza watu waliohudhuria sherehe ya Maulid ya kumtoa mtoto kufuatia kitendo chake cha kwenda jikoni akiwa na mfuko wa ‘Rambo’ na kuomba atiliwe pilau pamoja na matandu yake ili aende navyo nyumbani kama “take away”.

Paparazi wetu ambaye alikuwa mmoja wa waalikwa mashuhuri hapo alistaajabu kuona kundi la kina mama wakiangua kicheko baada ya kumwona Brazamen huyo akichomoa mfuko wake wa Rambo aliokuwa ameuhifadhi kwenye ‘jeans’ lake na kuomba atiliwe pilau hilo kwenye mfuko huo.

Kijana huyo ambaye alikata mshipa wa aibu alipofika kwenye sufulia la pilau hilo, alimshawishi mpishi amjazie msosi, na mpishi huyo baada ya kuona macho mengi ya watu yakielekezwa kwake, aliamua kutumia ‘Uislamu’ na kumjazia Braza huyo pilau kama wanavyoonekana pichani.

Kocha wa Timu ya Taifa ya Pool kutoka Nchini Zambia Bw. Dennis Lungu atua dar


Kocha wa Timu ya Taifa ya Pool kutoka Nchini Zambia Bw. Dennis Lungu akisalimiana na afisa habari kutoka kampuni ya Integreted Bw. Innocebt Mellek walipokutana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye kijiji cha makumbusho leo katikati ni Mwambata wa Biashara na Masoko katika Ubalozi wa Zambia Nchini Bw Sunday Chikoti.
BAADA ya kilio cha muda mrefu kuhusiana na kocha wa timu za Taifa za Pool table nchini, hatimaye kilio hicho kimesikika baada ya wadhamini wa mchezo huo nchini Safari Lager kukisikia na kuamua kusaidia ujio wa kocha kutoka nchini Zambia.
Kocha huyo kijana Denis Lungu ambaye ana umri wa miaka 27, amesaini mkataba wa miaka miwili ambao umeanza rasmi Agosti Mosi mwaka huu hadi Julai 28 mwaka 2012 huku akihaidi kuibadilisha Tanzania na kuifikisha katika medani za kimataifa kwenye mchezo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha kocha huyo katika mkutano uliofanyika kijiji cha Makumbushi jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TAPA, Amos Kafwinga alisema uamuzi wao wa kumleta kocha huyo unatokana na jukumu walilonalo kama chama ni kuhakikisha wanafanya kila jitihada kuuinua mchezo huo na mojawapo ni kuwa na kocha wa uhakika.
“Lengo la kumleta kocha huyu ni kama inavyoeleza katiba yetu kuwa chama kitasimamia na kuendeleza mchezo wa Pool, hivyo kutokana na jukumu hili ni lazima tuwe na kocha wa uhakika mwenye uwezo mzuri wa kutufikisha kule tunakohitaji.
“ Na kama haitoshi, ni azma ya chama chetu kuhakikisha mchezo huu unachezwa kwa kufuata sheria na viwango vinavyoeleweka ili uwe na ladha hata mtazamaji afurahie kuangalia ili kutekeleza vema azma ya mdhamini wetu bia ya Safari Lager ya kuleta mapinduzi ya kweli na mafanikio makubwa katika mchezo wa Pool nchini” alisema Amos.
Akizungumzia mikakato yake katika kuundeleza mchezo huo nchini, Denis alisema atahakikisha anatumia uwezo wake wa hali ya juu ya kuucheza mchezo huo wa takribani miaka 15 kuhakikisha anaibadilisha Tanzania na kutamba katika medani za kimataifa.
“Matamanio yangu ni kuusogeza mbele na siku za usoni Tanzania itambulike kwenye ramani ya Dunia ya mchezo huo si kwa kuwa washiriki, bali wachezaji wake waweze kuucheza kwa kufuata sheria, kanuni na viwango vya hali ya juu” alisema Denis.Hata hivyo aliwataka viongozi wa mchezo huo na Serikali kwa ujumla kuhakikisha mchezo huo unaasisiwa zaidi shuleni ili watoto waanze kujifunza huko na si kusubiri vijana wa umri wa kati ambao wanatuhusiwa kwenda baa ndio wajifunze maana ndipo meza za mchezo huo zinapopatikana jambo lililochangia mchezo huo kushindwa kupiga hatua za haraka

Wednesday, August 11, 2010

HASHEEM ATUA TENA BONGO



Mchezaji wa Mpira wa kikapu nchini Marekani NBA anayechezea timu ya Memphis Grizzlies, Hasheem Thabeet (pichani) akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kuanza kwa programu ya Basketball Clinic itakayoanza tarehe 12 Agosti kwenye viwanja vya Don Bosco.

Watoto zaidi ya 400 wanatarajiwa kukutana kwenye clinic hiyo ambapo TBF kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Phares Magesa amesema wanatakiwa kujiandikisha katika shule zote zenye vilabu vya Basketball nchini kote.

Lakini pia Hasheem Thabeet ameeleza kwamba katika nchi za Afrika ameshafanya Basketball Clinic kama hizo katika nchi za Nigeria, Senegal, Ivory Coast pamoja na Tanzania kwa sasa, kwa nchi za Asia amefanya programu kama hiyo na mchezaji mwenzake Yao Ming kwa nchi za HongKong, Quatar. Taipei, kulia katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa TBF Phares Magesa.


PICHA: HISANI YA FULL SHANGWE