Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, August 15, 2010

Mtoto Andrea Kipangula ni mtoto yatima kati ya watoto wanaosaidiwa vifaa vya shule na TAWLAE kwa msaada wa USAID/AED/ AGSP.

Ana miaka 10 (kumi) na anasoma darasa la nne (4) katika shule ya Kibao, wilaya ya Mufindi, kwa sasa, kwa masaa anayoweza kumudu anasoma shule ya msingi ya Makuburi, wilaya ya Kinondoni.

Mtoto huyu ana tatizo la kutopata choo kwa muda mrefu kwa vile njia yake ya haja kubwa

inahitilafu. Madaktari wamemfanyia upasuaji mara saba hosipitali ya rufaa ya Muhimbili ili kurekebisha hali yake.

Kwa sasa imebidi atumie utumbo mkubwa kutolea choo ambao upo nje ya tumbo lake, hali ni ngumu kwa mtoto huyu.

Bibi yake ambaye ni mzee sana pamoja na shangazi yake ambaye ni mjane, hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu na maisha.

Wale watakaopenda kusaidia kwa njia ya benki, tafadhali weka katika akaunti namba

0121030000838 ya NBC Samora Branch Dar-es-salaam, ukishaweka tuarifu kupitia simu namba 0754-360215 begin_of_the_skype_highlighting 0754-360215 end_of_the_skype_highlighting au +255(22)2700085 begin_of_the_skype_highlighting +255(22)2700085 end_of_the_skype_highlighting au fax pay in slip ya benki kwenye namba +255(22)2700090 begin_of_the_skype_highlighting +255(22)2700090 end_of_the_skype_highlighting. Vinginevyo tuletee msaada kwenye ofisi zetu zilizopo MARI-MIKOCHENI Plot namba 24 “b” Sam Nujoma Road kuelekea kiwanda cha Cocacola,

Tafadhali tunaomba msaada wako ili kumsaidia.

Aksante.

Mary Liwa

Mkurugenzi wa Miradi

No comments:

Post a Comment