Habari mbalimbali toka pande za bongo bila kusahau matukio mbalimbali yanayorindima pande zote za dunia
Psquare Ft. J.Martins- E No Easy
Wednesday, September 8, 2010
CHADEMA yaazimia kuishitaki CCM kwa Wapiga Kura

L-R: Mabere Marando | Prof. Mwesiga Baregu | John Mnyika
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kampeni ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Prof. Mwesiga Baregu akiwa na viongozi wengine wa chama hicho, leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam amezungumzia maamuzi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini kutupilia mbali malalamiko ya chama hicho dhidi ya mgombea wa Uraisi kupitia CCM, Jakaya Kikwete.
Amesema CHADEMA imeweka wazi kuwa haitaweza kwenda mahakamani kutaka mgombea Uraise kupitia CCM, Jakaya Kikwete, aenguliwe kushiriki uchaguzi na badala yake watawashawishi wananchi wasimpigie kura mgombea huyo wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Uamuzi CHADEMA unakuja baada ya wakili wa chama hicho ambaye pia ni mjumbe wa timu ya Taifa ya kuratibu kampeni za uchaguzi, Mabere Marando, kutoa ushauri wa aina mbili ambao ni, kwenda Mahakama kuu kuomba marejeo ya maamuzi ya Tendwa ili mahakama hiyo itoe maamuzi ya haraka ya kumuondoka Rais Kikwete kugombea Uraisi au; Kushitaki kwa kutumia sheria ya gharanma za uchaguzi.
credit source: http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz0yvXkVguQ
Nimemaliza Shule!

BAADHI ya watahiniwa katika shule ya Msingi, Miburani, Temeke, Dar es Salaam wakishangilia baada ya mtihani wa mwisho wa kuhitimu Elimu ya Msingi. (photo: Bashir Nkoromo).
Vijana hawa wananikumbusha siku tuliyokuwa tukiisubiri kwa hamu kubwa sana, 'kumaliza shule' tukiamini ati baada ya kuondokana na adha ya kudamka alfajiri, kushikana mashati na 'konda', kuwahi 'namba' na 'mstarini'... yaani ndoto za kila aina alimradi kujiaminisha usumbufu utakuwa umekwisha kabisa.
Tulijiona sisi ndiyo 'top' hakuna mwingine duniani kama sisi. Hisia za 'kumaliza shule' na kubaki nyumbani wakati wengine wanaamka asubuhi wakiwa na heka heka za ama kwenda shuleni au kazini, zilitutawala.
Siku hizi, tofauti na zamani nilipomwona 'madha mnoko', huwa najivuna sana kuwa na Mama asiye na longolongo wala 'kukopesha maneno' kwani, aliponisikia nikijitapa eti 'nimemaliza shule' siku moja aliniambia,
"...wewe, umemaliza shule ipi? Subi, hujamaliza shule. Umehitimu Elimu ya Msingi tu. Umeimalizaje shule wakati hujafika hata Sekondari? Umesahau methali mlizofundishwa, Elimu ni bahari; Elimu haina mwisho? au ulidhani ukishakariri na kuandika kwenye daftari ukafunga na ulichofundishwa kimefungwa kwenye mkoba? Yaani mwalimu akishafuta ubao na kwenye akili yako vinafutika? (kichwani mwangu nawaza, 'kwani si ndiyo kazi ya shule? unaandika, mnakusanya madaftari, mwalimu anatia 'pata' kama hesabu umekosea fanya masahihisho tu, basi').
Umevuka madarasa ya shule ya awali, sababu ya kuitwa 'msingi' ni kwa kuwa umeweka msingi wa elimu na maisha yako. Ni sawa na kujenga nyumba. Ili iweze kusimama imara, lazima msingi uwepo, tena uwe ni msingi ulio imara. Msingi ndiyo kigezo cha uimara wa nyumba. Umeweka msingi, bado kuta, madirisha, paa, na fenicha na vifaa vingine vya ndani. Lakini la muhimu ni msingi. Ikiwa uliweka msingi imara, nyumba yako itakuwa imara, utaweza kujenga nyumba kuuuubwa au hata orofa, inategemea na uimara wa msingi wake."
Ni baada ya kwenda kwa Bibi na kuwatembelea ndugu, ninarejelewa kauli ya Mama, 'hujamaliza shule' nhe he, ndipo nilipotia akilini, kumbe tulichokuwa tukifurahia 'standadi seven kumaliza shule' ilikuwa ni furaha ya muda tu, tena ya kitoto, bado ilikuwepo kazi kubwa mbele yetu; Kuna kusaidia kazi za nyumbani sasa zaidi ya wengine na; Kuna kuchukua fomu za shule za "private" tena kujaza zaidi ya moja, na kwa ambaye matokeo ya maendeleo yake shuleni kila mhula hayakuwa mazuri, hali kwake ilikuwa ni mbaya, yaani atazijaza fomu za 'private school' hata tano ili walao abahatishe moja ikiwa atakataliwa kwingineko. Nakumbuka nilizijaza mbili, Majengo Secondary na Uru Seminary. Kisha kuna kufanya tena mtihani wa kuomba kujiunga na shule hizo na, ni lazima ufaulu, la sivyo uaibike kwa kuzurura mtaani na kufanya kazi nyumbani wakati wenzio wanaongozana kwenda na kutoka shuleni! Shabash! Hakuna kumaliza shule!
Naam, huo ndiyo wakati nilipoanza kufahamu kuwa ninayahama maisha ya utoto na kuingia ujanani.
Hongereni vijana mliohitimu elimu ya msingi, shule bado hamjaimaliza. Elimu haina mwisho
Msuba. Ganja. Bangi. Marijuana. Jani. Hashish. Charas.
Cpl Ryan Belgrave with the Canadian Army's 1st Battalion, The Royal Canadian Regiment Battle Group, walks through a field of marijuana plants during a patrol near the village of Salavat, in the Panjway district west of Kandahar on August 4, 2010. (REUTERS/Bob Strong)
Picha, hii inawakilisha sehemu ndogo sana tu ya mashamba yote ya bangi yaliyomo nchini Afghanistan.
Ukitaka kusoma matumizi ya bangi kwa ajili ya matibabu,
Hayo ni majina kadhaa yaliyopewa mmea wa 'bangi' ambao unahesabiwa kuwa mojawapo ya madawa ya kulevya ingawaje wengine husema kuwa majani yake ni mboga ya kawaida tu kwa ugali isiyo na madhara.
Hadi kufikia mwezi Machi 2010, takwimu zilizoripotiwa na Umoja wa Mataifa zinasema kuwa Afghanistan ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kilimo na uzalishaji wa mmea wa bangi ambapo nusu ya majibo yote 34 ya nchini humo hujishughulisha na kilimo cha mmea huo ambapo inakadiriwa kuwa hekta moja huzalisha kilo 145 ya bangi tofauti na kilo 40 zinazozalishwa kwa ukubwa wa eneo ilo hilo huko Morocco. Inakadiriwa pia kuwa kiasi cha dola za Kimarekani $3,900 hupatikana katika mauzo ya hekta moja ya bangi.
Mrema azungumzia kazi ya kubeba zege

Mgombea ubunge kupitia tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Agustine Lyatonga Mrema.
MGOMBEA ubunge kupitia tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Agustine Lyatonga Mrema katika jimbo la Vunjo Moshi Vijijini, amesema kwamba kazi ya ubunge siyo sawa na kazi ya kubeba zege ambayo itawahitaji vijana na siyo watu wazima kama yeye.
Mgombea huyo aliyasema hayo katika kipindi cha Mchakato Jimboni kinachorushwa na Runinga ya TBC1 kilichofanyika Chuo cha Ualimu Marangu hivi karibuni ambapo Mrema aliulizwa swali na mwananchi mmoja aliyetaka kujua kutokana na umri wake mkubwa na madai kwamba ni mgonjwa, je ataweza mikikimikiki ya kuwahudimia wananchi hao vyema kama wakimpa nafasi ya kuwa mbunge.
“Bungeni hatuendi kubeba zege,” alianza kujibu Mrema na kuwafanya watu waliohudhuria mdahalo huo kulipuka kwa vicheko na kuendelea kutamba kwa kusema kwamba yeye anaijua kazi hiyo vizuri sana tofauti na wagombea wengine kwa kuwa aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 10 hivyo anapaswa kupewa kura za wananchi wa jimbo hilo la Vunjo.
“Watu wanasema sijui Mrema anaumwa, mtu huwezi kukwepa kuumwa hata Dk. Slaa (Dkt. Willibrod Slaa mgombea urais wa Chadema) aliumwa pale alipoanguka bafuni na kuumia mkono, sijui nini si mnaniona au kama mnaona mimi ni mgonjwa muulizeni mke wangu kama kweli mimi ni mzima au mgonjwa…” alisema Mrema na kumfanya mwendesha kipindi hicho Shaaban Kissu kumkatisha kwa kumwambia kuwa inatosha.
Mbali na Mrema wagombea wengine waliojitokeza katika mdahalo huo ni pamoja na John Mrema wa Chadema na Crispine Robert Meela wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao nao kama ilivyokuwa kwa Mrema walipata fursa ya kutangaza ilani za vyama vyao.
BREKING NYUZZZZZ:DR. SLAA AFUNGULIWA MASHTAKA MAHAKAMA KUU JANA

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa (pichani), amefunguliwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaami, akidaiwa fidia y ash. bilioni moja kwa madai ya kunyang’anya mke wa mtu.
Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010, ilifunguliwa leo mahakamani hapo na Aminiel Mahimbo kwa kupitia ofisi ya mawakili ya Amicus.
Mahimbo anadai kuwa, Dk. Slaa kamnyang’anya mkewe wa ndoa Josephine Mushumbusi.
Kwa kupitia nakala ya hati ya madai, Mahimbo anadai fidia ya sh. milioni 200 kutokana na hasara alizozipata baada ya mdaiwa huyo, kumtangaza mkewe wa ndoa Josephine kuwa mchumba wake na sh. milioni 800 ikiwa ni hasara ya jumla aliyopata.
Mlalamikaji huyo, anadai Septemba 7, 2002 alifunga ndoa na mwanamke huyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama na kuishi maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara, Baruti, Dar es Salaam.
Pia anadai katika maisha yao ya ndoa wamebahatika kuwa na watoto wawili ambao ni Upendo aliyezaliwa Mei Mosi, 2003 na Precious aliyezaliwa Machi 14, 2007.
Mahimbo alidai, ndoa kati yake na Josephine haijavunjwa na chombo chochote na kwamba, bado ni mke wake halali.
Kwa mujibu wa hati hiyo, Mahimbo alidai hivi karibuni, mkewe alikuwa na safari za mara kwa mara na aliamini ni za kikazi. Josephine ni mfanyabiashara ambaye anaendesha kampuni iitwayo Green World Clinic.
Alidai katika tarehe na mahali tofauti, Dk. Slaa alimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, suala ambalo si kweli.
Mlalamikaji huyo alidai, uhusiano uliopo kati ya watu hao wawili umemfanya adhalilike na kunyanyasika katika jamii na anaiomba mahakama kumzuia Dk. Slaa kuendelea kujihusisha kimahusiano na mkewe.
Anaiomba mahakama kumwamuru Dk. Slaa kumlipa bilioni moja na kulipa gharama za kuendeshea kesi.
Mahimbo amedai ameambatanisha na cheti cha ndoa na Josephine, picha za harusi, vyeti vya kuzaliwa vya watoto na nakala za vipande vya magazeti zilizopigwa wakati Dk. Slaa akimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe.
Tuesday, September 7, 2010
Upendo Nkone Kufunga Ndoa Tarehe 17 October 2010

Muimbaji wa Injili Upendo Nkone atategemea Kufunga ndoa tarehe 17 October 2010 na Mchungaji John Mbeyela ambaye pia ni mjane mwenye watoto watatu, ndoa hiyo itafungwa katika kanisa la Naioth kwa Mchungaji Mwasota.
Akiongea na Strictly Gospel Upendo Anasema “Ninafurahi sana na ninaomba Mungu akamfute machozi kila mjane, haijalishi umekaa miaka mingapi. Mungu yupo atakukumbuka”
Bi. Nkone ambaye ameishi maisha ya ujane kwa miaka 9, ana jumla ya album tatu ambazo ni Mungu Baba, Hapa Nilipo na Zipo faida.
Tunamtakia kila la heri katika maandalizi yote mpaka harusi
Subscribe to:
Posts (Atom)