Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, May 3, 2010

Ubingwa wanukia kwa Chelsea!!!


Chelsea imekaribia kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya England baada ya kuichapa Liverpool kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Anfiled.

Kipindi cha pili kilianza taratibu, na dakika nane tu baada ya mapumziko hayo, Frank Lampard aliandika bao la pili na la ushindi.

Liverpool wakionekana kuchoka kutokana na mchezo wa ligi ya Europa dhidi ya Atletico Madrid, hawakuonesha dalili zozote za kuzinduka.

Obama atembelea eneo yanakovuja mafuta!!!


Rais Barack Obama wa Marekani ameelezea kuvuja kwa mafuta katika Ghuba ya Mexico ni janga kubwa la kimazingira ambalo halijawahi kutokea.

Akizungumza huko Louisiana, Bw Obama alisema serikali yake itafanya kila linalowezekana kuondoa mafuta hayo, na kuongeza kuwa BP inahusika na kuwajibika kwa gharama za usafishaji wa mazingira.

Alisema kazi ya muhimu kwa sasa ni kuzuia mafuta yasisambae zaidi katika pwani ya Ghuba.

BP inasema itachukua zaidi ya wiki moja kabla ya mipango ya dharura kuzuia uvujaji huo haijaanza kuzaa matunda.

Lakini huenda kazi ya kuchimba visima vya pembeni kusaidia kunyonya mafuta ikamalizika baada ya miezi kadhaa kumaliza kabisa tatizo hilo, Waziri wa mambo ya ndani, Ken Salazar alionya siku ya Jumapili.

Mtambo unaoendeshwa na BP wa kuchimbia mafuta ujulikanao kama Deepwater Horizon, ulizama tarehe 22 Aprili, siku mbili baada ya mlipuko kuua watu 11.

Chadema kutumia Sh 5 bilioni uchaguzi mkuu!!!


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimetuma salamu kwa Chama cha Mapinduzi(CCM), kuwa kitakigaragaza hama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa bajeti ya Sh 5 bilioni.


Chama hicho ambacho pia kimethibitisha kusimamisha mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kimetangaza ratiba ya kuanza kuchukua fomu kwa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani ambazo zinaanza kutolewa leo nchi nzima.

Vilevile chama hicho kimepanga kuwa Agosti 11 mwaka huu baraza la kuu la Chadema, litapendekeza majina ya wagombea urais, makamu wa rais muungano na rais wa Zanzibar na ilani ya chama, Agosti 12 utafanyika mkutano mkuu wa kuteua jina la mgombea urais na kuthibitisha ilani yao.

Katibu mkuu wa chama hicho Dk, Wilbroad Slaa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akitoa taarifa maalumu, kwa umma kuhusu mkutano mkuu wa halmashauri ya kuu ya Chadema uliofanyika Aprili 25 na 26 mwaka huu.

“Ni kwa kutumia fedha hizo tutawashinda CCM na mabilioni yao, sisi hatuwezi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya uchaguzi katika nchi masikini na inayokabiliwa na matatizo makubwa kama nchi yetu,”alisema Dk Slaa na kuongeza,

“Chadema tunaamini katika nchi masikini kama hii ambayo watu wake wanakabiliwa na shida mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wao kukosa masomo, wafanya kazi kukosa mishahara bora na huduma bora za jamii kwa ujumla Sh 5 bilioni zinatosha katika kuandaa vikao na kupiga kampeni kwa nafasi zote ikiwemo ya uraisi kutumia Helcopter,”.

Akitaja vyanzo vya fedha alisema chama hicho kinategemea michango ya wanachama, marafiki na kwamba kinaweza kikakopa kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

Sunday, May 2, 2010

CUF wamlalamikia Bujugo kuanza kampeni!!!



CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimelalamikia kitendo cha Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo (CCM) kwa kitendo cha kuitisha mikutano ya hadhara na kisha kuwaada wananchi wa Kata hiyo iliapate kuchaguliwa tena nafasi ya Udiwani.

Malalamiko hayo yalitolewa na baadhi ya wazee wa CUF katika kijiwe cha Shibam, wazee hao ambao hawakutaka kutaja majina yao gazetini walidai kuwa, kitendo cha Bujugo kuzunguka katika mitaa hiyo na wapambe wake ni kukiuka katiba ya Uchaguzi.

“Haiwezekani Bujugoo kuanza kuitisha mikutano ya adhara na kuongea mambo ya kujifagilia wakati hajasaidia chochote katika Kata hii” alisema Mzee huyo ambaye nji Kada wa CUF.

Mwingine alisema kuwa, kitendo cha kujisifia kuwa ameweza kujenga barabara kwa kiwango cha lami huo ni uongo, wakati akijua ukweli barabara hiyo imejengwa chini ya kiwango kwa mradi wa Manispaa ya Kinondoni na wala si yeye kama anavyojitangazia” alisema Mzee huyo.

Mwandishi wa Habari hizi ambaye alikuwepo katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, ambapo Diwani huyo alikuwa akinadiwa na Makada mbalimbali wa CCM wa Kata hiyo akiwemo Mwenyekiti Shaweji Mkungura, walidai kuwa kwa kuona diwani wao huyo kuleta maendeleo Kata ya Mamogeni wameamua kumchagua aendelee kugombea awamu nyingine.

“Jamani Diwani wetu ametujengea barabara na ameweza kushirikiana na sisi kwa kila jambo hivyo tunaomba muendelee kumpa kura zenu za udiwani katika uchaguzi hapo baadae’ alisikika akimnadi Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo baada ya kuwasiliana na Bujugo juu ya kushutimiwa kuanza kampeni mapema kabla ya wakati, hakuweza kupatikana baada ya simu yake kutokuwa hewani muda mrefu.

Je Wajua hii??


Pichani Mwanamuziki Wahu kutoka Nchini kenya katika moja ya Show zake...Je unajua kwamba Mwanadada huyu alikuwa Mwanamke wa Kwanza Afrika kutoka Kenya Kushika namba 1 kwenye mtihani wa Hesabu?Kama ulikuwa huji basi habari ndio hiyo,pia mwanadada huyu mbali na Usanii hapo alipo ana Stashahada ya Hesabu na hivi karibuni yuko mbioni kumalizia Degree yake ya masuala ya Communications.

Matokeo kidato cha sita: wasichana watamba!!!


JUMLA ya watahiniwa 55,764 sawa na asilimia 88.86 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Sita mwaka huu, wamefaulu ambapo idadi ya wasichana waliofaulu ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya wavulana.

Jumla ya wasichana 21,821 sawa na asilimia 90.39 ya wasichana waliofanya mtihani huo wamefaulu, wakati wavulana waliofaulu ni 33,943 sawa na asilimia 87.90 ya wavulana waliofanya mtihani huo.

Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk. Joyce Ndalichako alisema idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa 10,048 wakati asilimia ya ufaulu imepungua kwa asilimia 0.78 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2009 ambapo waliofaulu ni 45,716 sawa na asilimia 89.64.

Alisema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 45,217 , sawa na asilimia 93.76 ya waliofanya mtihani na watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 10,547 sawa na asilimia 74.57.

Mwaka 2009 watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu ni 9,244 sawa na asilimia 74.84 ya waliofaulu. Hivyo idadi ya waliofaulu imeongezeka kwa watahiniwa 1,300 ikilinganishwa na mwaka jana.

Ingawa wasichana wanawaburuza wavulana kwa idadi ya waliofaulu, kwa mujibu wa matokeo nafasi ya wanafunzi kumi bora kitaifa inashikiliwa na wavulana waliokuwa wanasoma shule za sekondari za wavulana ambapo Sekondari ya Mzumbe inang’ara kwa kutoa wanafunzi bora wanne kati ya 10.

Walioshika nafasi ya kwanza hadi ya kumi kitaifa na shule zao kwenye mabano ni Japhet John (Ilboru), Manyanda Chitimbo (Kibaha), Hassan Rajab (Minaki), Samuel Killewo (Feza Boys), Abdullah Tahel, Steven Elias na Paul Nolasco wote wa Mzumbe Sekondari, Alexander Marwa (Tabora Boys) Ephraim Swilla (Mzumbe) na Benedicto Nyato (Tabora Boys).

Mgambo waamua Kupiga Dili la Miamvuli


kulingana na hali ya hewa ya jiji kwa sasa kuwa ni ya mvua mvua za mara kwa mara,Mgambo wa jiji waamua kufanya biashara ya kuuza miamvuli kwa wakazi wa jiji.
Sasa sijui hii biashara ni ya kwao wenyewe au wameagizwa na mabosi wao??