Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, May 3, 2010

Chadema kutumia Sh 5 bilioni uchaguzi mkuu!!!


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimetuma salamu kwa Chama cha Mapinduzi(CCM), kuwa kitakigaragaza hama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa bajeti ya Sh 5 bilioni.


Chama hicho ambacho pia kimethibitisha kusimamisha mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kimetangaza ratiba ya kuanza kuchukua fomu kwa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani ambazo zinaanza kutolewa leo nchi nzima.

Vilevile chama hicho kimepanga kuwa Agosti 11 mwaka huu baraza la kuu la Chadema, litapendekeza majina ya wagombea urais, makamu wa rais muungano na rais wa Zanzibar na ilani ya chama, Agosti 12 utafanyika mkutano mkuu wa kuteua jina la mgombea urais na kuthibitisha ilani yao.

Katibu mkuu wa chama hicho Dk, Wilbroad Slaa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akitoa taarifa maalumu, kwa umma kuhusu mkutano mkuu wa halmashauri ya kuu ya Chadema uliofanyika Aprili 25 na 26 mwaka huu.

“Ni kwa kutumia fedha hizo tutawashinda CCM na mabilioni yao, sisi hatuwezi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya uchaguzi katika nchi masikini na inayokabiliwa na matatizo makubwa kama nchi yetu,”alisema Dk Slaa na kuongeza,

“Chadema tunaamini katika nchi masikini kama hii ambayo watu wake wanakabiliwa na shida mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto wao kukosa masomo, wafanya kazi kukosa mishahara bora na huduma bora za jamii kwa ujumla Sh 5 bilioni zinatosha katika kuandaa vikao na kupiga kampeni kwa nafasi zote ikiwemo ya uraisi kutumia Helcopter,”.

Akitaja vyanzo vya fedha alisema chama hicho kinategemea michango ya wanachama, marafiki na kwamba kinaweza kikakopa kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment