Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, May 2, 2010

CUF wamlalamikia Bujugo kuanza kampeni!!!CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimelalamikia kitendo cha Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo (CCM) kwa kitendo cha kuitisha mikutano ya hadhara na kisha kuwaada wananchi wa Kata hiyo iliapate kuchaguliwa tena nafasi ya Udiwani.

Malalamiko hayo yalitolewa na baadhi ya wazee wa CUF katika kijiwe cha Shibam, wazee hao ambao hawakutaka kutaja majina yao gazetini walidai kuwa, kitendo cha Bujugo kuzunguka katika mitaa hiyo na wapambe wake ni kukiuka katiba ya Uchaguzi.

“Haiwezekani Bujugoo kuanza kuitisha mikutano ya adhara na kuongea mambo ya kujifagilia wakati hajasaidia chochote katika Kata hii” alisema Mzee huyo ambaye nji Kada wa CUF.

Mwingine alisema kuwa, kitendo cha kujisifia kuwa ameweza kujenga barabara kwa kiwango cha lami huo ni uongo, wakati akijua ukweli barabara hiyo imejengwa chini ya kiwango kwa mradi wa Manispaa ya Kinondoni na wala si yeye kama anavyojitangazia” alisema Mzee huyo.

Mwandishi wa Habari hizi ambaye alikuwepo katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, ambapo Diwani huyo alikuwa akinadiwa na Makada mbalimbali wa CCM wa Kata hiyo akiwemo Mwenyekiti Shaweji Mkungura, walidai kuwa kwa kuona diwani wao huyo kuleta maendeleo Kata ya Mamogeni wameamua kumchagua aendelee kugombea awamu nyingine.

“Jamani Diwani wetu ametujengea barabara na ameweza kushirikiana na sisi kwa kila jambo hivyo tunaomba muendelee kumpa kura zenu za udiwani katika uchaguzi hapo baadae’ alisikika akimnadi Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo baada ya kuwasiliana na Bujugo juu ya kushutimiwa kuanza kampeni mapema kabla ya wakati, hakuweza kupatikana baada ya simu yake kutokuwa hewani muda mrefu.

No comments:

Post a Comment