Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, June 12, 2010

Mtoto wa Will Smith na Jackie Chan ndani ya bonge la movie!!







Usikose kuichek hii!! Dogo kafanya maajabu humo ndani, ama kweli mtoto wa nyoka ni nyoka..

Friday, June 11, 2010

Kombe la Dunia laanza Kwa Majonzi!!


Kitukuu wa Nelson Mandela Zenani Mandela amefariki dunia.

Afisi ya uhusiano mema katika wakfu wa Nelson Mandela imesema kuwa msichana huyo wa miaka 13 alifariki katika ajali ya barabarani iliyompata hapo jana akiwa njiani kutoka sherehe za mkesha wa kombe la dunia mjini Soweto.

Duru za polisi zimesema uwa dereva aliyesababisha ajali hiyo amekamatwa.

Huku hayo yakiarifiwa, mechi ya kwanza kabisa ya kombe la dunia kuwahi kufanyika barani Afrika inatazamiwa kuanza wakati wowote kati ya wenyeji Afrika Kusini na Mexico.

Timu 32 zinachuana kuwania kombe hilo baada ya mwezi mmoja na aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela anatarajiwa kuhudhuria sherehe ya ufunguzi leo jioni.

Sawa Mheshimiwa yuko salama ila magari yanahitaji kazi ya ziada!


IKULU imewatoa wasiwasi wananchi kuhusu usalama wa Rais Jakaya Kikwete na kuwahakikishia kuwa mkuu wa nchi yuko katika mikono ya watu makini, salama na wazalendo wanaoifahamu kazi yao.


Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu, wakati akifafanua kuhusu tukio la magari matano yaliyokuwapo kwenye msafara wa Rais mkoani Kilimanjaro kupatwa na hitilafu na kushindwa kuwaka wakati wa ziara yake wiki hii.

Akifafanua kuhusu tukio hilo lililotokea Juni 8, mwaka huu, alisema sehemu ya magari ambayo ilikuwa yatumike kwenye msafara huo, yakiwa katika utaratibu wa maandalizi ya kumpokea Rais Kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), yalipelekwa katika kituo cha mafuta cha Rafiki.

“Baada ya kujazwa mafuta magari matatu kati ya hayo matano, yalikataa kuwaka, baada ya kuona hivyo, uamuzi ulichukuliwa wa kutoyawasha kabisa yale magari mengine mawili,” alisema Rweyemamu.

Hata hivyo, alisema kituo kilichotumika ni moja ya vituo ambavyo vimekuwa vinatumiwa kujaza mafuta ya magari ya Rais siku nyingi na kwamba uamuzi wa kuyajazia mafuta magari hayo katika kituo hicho haukuwa wa kushtukiza ama kubahatisha.

“Ukweli ni kwamba uamuzi wa wapi pa kujaza mafuta magari ya Rais, si wa madereva, bali huanzia ngazi za juu,” alifafanua.

Alisema kinachofahamika ni kwamba wakati magari hayo yanaingia kujazwa mafuta kituoni hapo, yalikuwa mazima, imara na salama kwa ajili ya kumpokea Rais Kikwete aliyekuwa anatokea Dar es Salaam na kwamba tatizo lilianza baada ya kujazwa mafuta hayo.

Hata hivyo, Rweyemamu alisema pamoja na hitilafu hiyo, msafara wa Rais ulipokelewa kama ilivyopangwa bila tatizo lolote kutokana na misafara ya aina hiyo mara zote huwa na mipango mbadala ya usafiri yenye kiwango cha juu cha usalama.

Alisema magari yaliyopata hitilafu hayakutumika kabisa katika msafara huo kwa kuwa yalikuwa yanasafishwa ambapo baada ya kusafishwa na kuwekewa mafuta mengine, yaliwashwa na kuwaka na yapo safarini kurejea Dar es Salaam.

“Uchunguzi wa tukio hili zima kwa sasa uko mikononi mwa vyombo vya usalama ikiwamo Polisi na Mamlaka ya Usimamizi wa Nishati na Maji (EWURA) na wakikamilisha uchunguzi wao, wananchi watajulishwa nini hasa kilitokea,” alisema.


Alisema tukio hilo haliathiri kitu chochote katika ziara hiyo na wala halikusababishwa na uzembe na kuhusu usalama wa Rais, hauna shaka yoyote na uko mikononi mwa watu wa kuaminika

Twanga kuazimisha Miaka Kumi!


Wazee wa Kisigino Twanga Pepeta bendi maarufu sana na ya muda mrefu inatarajia kutimiza miaka 10 toka kuanzishwa kwake kwa style ya kipekee ndani ya uwanja wao wa nyumbani pale Leaders Club.

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka “Jiwe” alisema kuwa pamoja na kusheherekea miaka hiyo Kumi lakini pia kutakuwa na uzinduzi wa album yao mpya na ya Kumi pia inayojulikana kama “Mwana Dar es Salaam”

“Kutakuwa na maandamano ambayo yataanzia ofisi zetu zilizopo Kinondoni mpaka viwanja vya Leaders ambako kutakuwa na bonanza ambalo litakuwa na michezo mbalimbali kuanzia kuvuta kamba, mbio za kuku, mpira wa wavu kwa wanawake, mpira wa miguu na zaidi ya hilo kutakuwa na burudani mbalimbali za wasanii wa kibongo na nje ya bongo ambao watasindikiza sherehe hizo” alisema Asha Baraka.

Soko la nyama nchini laelezwa kuimarika


Soko la nyama ya ngombe nchini limeelezwa kukua kwa kasi nzuri, kutokana na kuuza nje ya nchi kati ya tani 6 na 10, kiwango ambacho hakikuwahi kuuzwa katika kipindi cha nyuma.

Akielezea mafanikio hayo, Afisa mauzo wa Bodi ya nyama nchini Kaiza Kuwana amesema soko la ndani na nje ya nchi kwa sasa ni kubwa kwa bidhaa hiyo, na kwamba juhudi zinafanyika kuuza wanyama wetu katika nchi ya Kenya kwa njia sahihi zitakazoingiza fedha za kigeni kwa Taifa, tofauti na inavyofanyika kimagendo kwa sasa.

Amesema kilo moja ya nyama inauzwa hadi Dola 4.25 za Kimarekani, na kwamba iwapo uzalishaji utaendelea kuborewshwa, nchi itazidi kunufaika.

Ukarabati barabara za jiji wapamba moto



Zoezi la ukarabati wa maeneo yenye kasoro katika barabara za jiji la Dar es Salaam limeendelea kupamba moto katika Wilaya ya Kinondoni, ambapo leo shughuli za kuziba viraka chakavu vya lami katika barabara ya Sinza Makaburini ilifanyika.

Akielezea maendeleo ya zoezi hilo, msimamizi wa ujenzi huo Immam Mvungi amesema shughuli inayofanyika ni kuvunja sehemu zilizoharibika na kuweka vipande vipya, kupanua maeneo finyu ya barabara pamoja na kuzibua mifereji iliyoziba katika barabara hizo.

Aidha ameeleza kuwa lengo la hayo yote ni kuimarisha barabara hizo ili kuweza kuondoa msongamano wa magari, pale yanapolazimika kupunguza mwendo kutokana na mashimo pamoja na kupita upande mmoja wa barabara kutokana uchakavu wa upande wa pili.

JK awamwagia Twiga Stars Mamilioni!!




Rais Kikwete ametoa shilingi milioni 53 kwa ajili ya kambi ya ya timu ya Taifa ya wanawake TWIGA STARS kujiandaa na fainali za mataifa ya Afrika ya wanawake nchini AFRIKA KUSINI ameyasema hayo leo katika sherehe za kuwapongeza timu hiyo zilizofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Pichani ni Rais Jakaya Kikwete akiwa na wachezaji wa Timu ya Twiga Stars pamoja na viongozi wao.