Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, April 13, 2010

Exclusive Akamatwa Live Gesti na Denti wake!Mwalimu wa Shule ya Sekondari Muhanga, iliyopo Tabata Kinyerezi, Dar, Lucas Yusuph a.k.a Ticha Leizer, juzi alijikuta akipata aibu ya mwaka baada ya kukutwa ndani ya gesti akiwa na mwanafunzi wake wa kidato cha tatu (Jina linahifadhiwa).

Ijumaa Wikienda a.k.a the Biggest IQ Paper ndilo pekee lenye kuthubutu kuwa la kwanza kulianika tukio hilo ambalo lilichukua nafasi Ijumaa iliyopita (Aprili 9, 2010) ndani ya kuta za Mori Guest, Sinza, Dar na kusindikizwa na timbwili zito.


.....jamani nilikuwa namfundisha hesabu za square...square..!!

Awali, gazeti hili lilipata malalamiko kutoka kwa familia ya mwanafunzi huyo kuwa binti yao amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa walimu mbalimbali, hali inayomsababishia aathirike kisaikolojia na kushindwa kufanya vizuri katika masomo yake.

Walisema kuwa, kutokana na mazingira hayo wamekuwa wakilazimika kumhamisha kutoka shule moja hadi nyingine lakini haikuweza kumsaidia kwani hata alipofika katika shule Muhanga, aliendelea kupata usumbufu kutoka kwa walimu wakware.

“Kwakweli tumechoshwa na usumbufu ambao umekuwa akipata binti yetu kutoka kwa walimu wakimtaka kimapenzi. Tumekuwa tukimgharamia pesa nyingi ili aweze kusoma lakini walimu wamekuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo yake.

“Wanamchapa na kumpa adhabu nzito ikiwa ni pamoja na kumfelisha kwa makusudi kwenye mitihani yake. Hilo lilitokea kwenye shule aliyokuwa akisoma awali, tukamhamishia katika shule hii ya Muhanga ambako nako mambo yamekuwa ni yale yale,” alisema kaka wa binti huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake na kuongeza:
“Kuhusu hili la Mwalimu Leizer, huyu binti yetu amekuwa akimlalamikia kwa muda mrefu akieleza kuwa, amekuwa akimsumbua akimtaka kimapenzi. Licha ya kumkatalia mwalimu huyu amekuwa akimlazimisha na leo amemwambia wakutane katika gesti ya Mori, eti kuna mambo anataka kumwambia, tunaomba mtusaidie ili tuweze kumnasa fataki huyu.”

Kufuatia maelezo hayo, waandishi wetu kwa kushirikiana na wazazi wa binti huyo pamoja Polisi wa Kituo cha Alimaua A, Tandale waliweka mtego ambapo Ijumaa majira ya saa 11 jioni walifanikiwa kumnasa Ticha huyo ‘live’ akiwa na mwanafunzi wake ndani ya chumba namba 1 cha gesti hiyo.

Baada ya fumanizi hilo, mwalimu huyo alijitetea kuwa hakuwa na lengo baya na denti wake na kudai kuwa, walikutana pale ili amfundishe mwanafunzi wake somo la Hisababti.

Hata hivyo, Ticha huyo alipobanwa kuhusu kondomu zilizokuwa kitandani, alishindwa kutoa majibu ya kueleweka.

Vijana wa Mwema ambao wakati huo walikuwa eneo la tukio, walimchukua mwalimu huyo pamoja na mwanafunzi wake hadi Kituo cha Polisi cha Alimaua kwa ajili ya mahojiano.

Ticha Leizer wakati akijieleza, aliruka kimanga kwa kudai kwamba yeye siyo mwalimu na kuongeza kuwa hata binti huyo aliyekuwa naye gesti hakujua ni denti.
Hata hivyo, Ticha huyo alipobanwa kuhusu kondomu zilizokuwa kitandani, alishindwa kutoa majibu ya kueleweka.

Vijana wa Mwema ambao wakati huo walikuwa eneo la tukio, walimchukua mwalimu huyo pamoja na mwanafunzi wake hadi Kituo cha Polisi cha Alimaua kwa ajili ya mahojiano.

Ticha Leizer wakati akijieleza, aliruka kimanga kwa kudai kwamba yeye siyo mwalimu na kuongeza kuwa hata binti huyo aliyekuwa naye gesti hakujua ni denti.
linakemea vikali tabia ya walimu kuwatongoza wanafunzi wao na linaomba taasisi husika kuhakikisha walimu kama hao wanashughulikiwa ipasavyo kwani wamekuwa ni chanzo cha baadhi ya wanafunzi wa kike kufeli katika masomo yao.

No comments:

Post a Comment