Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, March 19, 2010

Kama kazi ndiyo hii…..................................


Kama jeshi ndiyo hivi……Mmmh naghairi kwakweli.


Wajeshi to be jamani wakiwa mazoezini huko Dodoma,Kurutaz..chokoza uone!

NILIKUWA MZIMA, NILIPATA ULEMAVU WAKATI NAJIFUNGUA-MUME WANGU HANITAKI TENA

Taarifa ya Mama huyu imenisikitisha sana, imenitoa machozi, kuna watu wanapata shida sana jamani, tumsaidie kwa mawazo, ajuwe nini cha kufanya, inaumiza sana.

Habari yako mdogo wangu INNOCENT WA UMBEA.COM, naandika kwa uchungu sana, moyo wangu unaniuma na machozi yananimwagika. Maana sina thamani ya kuishi kama binadamu wengine, naamini nilizaliwa kwa bahati mbaya, Naona bora hata ningekufa nilipozaliwa tu kama alivyokufa mwanangu. alienipa matatizo

Miaka nane iliyopita nikiwa chuoni Tabora, nilizaa na baba mmoja, baada ya kutoka chuo tukaamua kuishi pamoja kwa makubaliano, mtoto akuwe kidogo ndio tubariki ndoa, but since there tukawa busy na kuendelea kufurahia maisha yale, hatukuwa interested tena na kufunga ndoa, (ni kosa ambalo nakubali nililifanya) tulikuwa na maisha ya kawaida sana, ila kwenye upendo hata kama kuna shida huwezi kuona karaha sana, upendo unafunika kila kitu, Nikiwa na Yule baba tulikuwa tumepanga, badae tukajenga kwetu huku Shinyanga. Tukahamia hapa, akanifungulia biashara, nikawa nafuga, Catering, grocery, mambo yakawa safi kabisa,

Mwaka juzi nilipata mimba, tukakubaliana kabisa nizae, na alinihudumia sana hadi naenda kujifungua, nilipofika hospitali wakati najifungua nilipata kifafa cha mimba, nilizaa mtoto ambae alikaa siku tatu akafariki, mwanangu alikuwa wa kike, wakwanza ni wa kiume, niliumia sana,

Kitu ambacho sikielewi hadi sasa, nikwamba baada ya mwanangu kufariki, nilikuwa bado niko hospitali, siku ya nne nikawa siwezi kuamka, yani nikikaa tu miguu haisogei kwenda kokote, ikawa inajaa maji tu, na sehemu ya kiunoni nikawa sihisi chochotekile, nilijua nia maradhi tu na yatakwisha, lakini siku zina kwenda, ikabidi hospitali wanipatie wheel Chair, ili kunisogeza

Nimeumiasana, maana mume wangu amebadilika ghafla, kipnindi cha mwanzo alikuwa ananipendapenda, lakini ss ananichukia ile direct, miradi amempa dada yake ndie awe msimamizi, anasema mimi siwezi, nilijuwa nitapata support yake, roho inauma sana, Napata support toka kwa mwanangu James, nampenda mwanangu, yeye ndie atake nizika,

Kuna watu walinishauri nirudi kwetu, maana ilifikia kipindi akawa ananikashfu, anasema mm ni mzigo, kwanza hatuna vyeti vya ndoa, nimwachie mwanae niondoke, sasa mimi nitaenda wapi na hali hii jamani? Bila yeye kutaka nizae tena ningepata ulemavu huu, Dunia imeniangukia jamani, sina wa kunitetea, mama alishakufa zamani, baba yangu ni mgonjwa nae alikuwa ananitegemea mimi,

Tumechuma mali nyingi sana na baba James, nilimwambia basi nipe nyumba moja(maana ziko tatu) na mtaji kidogo kasha mimi nikakae huko na mwanangu, nitatafuta mtu atakuwa ananisaidia kusimami vibiashara vyangu, anasema atanipa kwa misingi ipi, anasema eti karibia nakufa, hizo mali nitaziharibu tu!, anatamani nife siku yeyote ile anaona kama namchelewesha, inauma sana INNOCENT

Kuna dada mmoja , alinipa jina la blogu yako, akanieleza ilivyo, nikaona namimi niandike ili nipatiwe ushauri, nifanye nini? Natamani hata kujiua, lakini moyo unagoma kufanya hivyo, nisaidieni mwenzenu.

JAMANI MAANDALIZI YA MOVIE YA HITAJI MOYO MMMMM JIONEE MWENYEWE


Aunty na The great katika moja ya scene za kifamilia zaidi,katika movie hii Aunty kaonesha mabadiliko makubwa sana tofauti na mwanzo,kiwango ni kikubwa zaidi ya mwanzo maana nimeshafanya nae kazi nyingi kama Fake smile,Village paster,Unfortunate love n.k.

VITUKO LOCATION wakati tuko ndani tunashoot Mzee Magali yuko nje anacheza na paka.

Hakika hii ilikuwa burudani ya aina yake maeneo tunayofanyia shooting ya movie yangu kwa siku ya leo.

Mzee Magali akicheza nae bila wasiwasi

hahahah hapa cjui anaongea na nani au paka mtu!

Picha zote kwa hisani ya kanumba blogu.umbea .com yawatakia kila la heri katika filamu hiyo!
UMBEA.COM LEO IKO KAZINI TENA KUWALETEA MAANDALIZI YA UCHAGUZI YANAVYOENDELEA NCHINI TANZANIA,KWA BAHATI NZURI NILIKUTANA NA MBUNGE WA CHUNYA {MH. VICTOR MWAMBALASWA} KULE KWA WANYAKYUSA KUPITIA TIKETI YA C.C.M NA KUFANYA NAE MAHOJIANO MAFUPI JUU YA MKAKATI WAKE NA JINSI GANI ALIVYOJIPANGA JUU YA UCHAGUZI HUU UNAOTARAJIA KUFANYIKA OKTOBA MWAKA HUU!IFUATAYO NI SEHEMU TU YA MAHOJIANO HAYO

UMBEA.COM MZEE ASLAAM ALYEKUM!
MH.MBUNGE,ALYEKUM MUISLAM HABARI YAKO KIJANA

UKATILI HUU UMEPITA KIASI NCHINI NIGERIA!!!



Ama kweli Kiama Kimekaribia!! Binadamu amekosa utu hata kushinda kipindi cha sodoma na gomora. Hao waliolala ni baadhi ya wachache kamera yetu ya umbea iliyobahatika kuwapiga picha baada ya kushuhudia bus likitekwa nyara na maharamia. Abiria hao walitakiwa kutoa kila walichonacho na baadhi yao kubakwa. Wale ambao hawakuwa na kitu chochote waliamuriwa kulala chini kisha dereva wa basi akalizimishwa kuwakanyaga kwa basi!!
Jamani huu ni unyama wa hali ya juu, umbea.com inalaani kitendo hichi kwa nguvu zote, wote waliohusika wachukuliwe hatua kali za kisheria!

Thursday, March 18, 2010

Tanzania kukaa giza kwa saa 5 kila siku


BAADA ya katikakatika ya umeme bila utaratibu kwa siku kadhaa, hatimaye Shirika la Umeme (Tanesco) limetangaza rasmi mgawo kwa mikoa yote Tanzania Bara kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne usiku kila siku.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Stephen Mabada, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, alisema sababu ya hatua hiyo ni kuharibika kwa baadhi ya mitambo katika vituo vya kuzalishia umeme.

Mitambo iliyotajwa kuharibika iko katika vituo vya kuzalisha umeme vya Kidatu, Kihansi, Pangani na cha gesi cha Ubungo.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza kiasi cha megawati zitakazokosekana baada ya mitambo hiyo kuharibika.

Badala yake taarifa hiyo ilisisitiza kuwa kuharibika kwa mitambo hiyo kumesababisha upungufu wa nishati hiyo kwenye Gridi ya Taifa, hali inayolilazimu shirika kuanzisha mgawo mikoa yote.

“Athari za upungufu huo zimelilazimu shirika kuanza mgawo wa umeme kwa maeneo mbalimbali wakati wa matumizi makubwa ya umeme kuanzia saa 12 jioni hadi saa nne usiku,” ilisema taarifa hiyo. Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, alipoulizwa kiasi cha megawati kitakachokosekana kwenye Gridi, alisema hawezi kuitaja kwa vile shirika bado linafanya jitihada za kurejesha baadhi ya megawati kwa kutengeneza mitambo hiyo haraka.

“Siwezi kukutajia kiasi kitakachokosekana maana naweza kukutajia idadi ya megawati, mafundi walioko kwenye mitambo wakarejesha baadhi ya megawati … hilo kwa leo siwezi kukutajia,” alisema Masoud.

Wastani wa megawati zinazotumika nchini ni takribani 700 kwa siku. Kwenye taarifa ya Mabada, kuna ahadi ya Tanesco kufanya haraka matengenezo ya mitambo iliyoharibika, ili kuondoa adha ya mgawo huo, lakini taarifa hiyo haielezi idadi ya siku za matengenezo.

Masoud alipotakiwa kueleza huo mgawo utadumu hadi lini, alisema mafundi ndio kwanza wako kwenye vituo na hawajajua ukubwa wa tatizo.

Alipotakiwa kutoa ufafanuzi kama mashine hizo ziliharibika kwa siku moja katika vituo hivyo, alijibu kuwa uhabirifu huo umetokea kwa nyakati tofauti na ndiyo maana kukawa na kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Awali Tanesco ilipoulizwa juu ya matukio ya kukatika ovyo kwa umeme hususan jioni, ilijitetea kuwa inatokana na njia kuzidiwa mzigo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji.

Hata hivyo, jana Masoud alikiri kuwa mgawo ulishaanza wiki kadhaa zilizopita na walisita kutangaza kwa kuamini kuwa matengenezo hayo yangechukua siku chache.

“Lakini baada ya kuona ripoti za kuharibika mashine zinatokea kwenye vituo vingine, tumeona tuutarifu umma juu ya kuwapo kwa mgawo,” alisema Masoud.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alipoulizwa lini mgawo huo utamalizika, alisema hajui ila akasisitiza kuwa mafundi wako kwenye maeneo ya kazi usiku na mchana kuhakikisha hali inatengemaa.

“Tutahakikisha mitambo hiyo inapona haraka, maana ni suala la dharura na siwezi kutabiri lini watamaliza matengenezo,” alisema Ngeleja. Katika siku za karibuni yamekuwapo matukio ya kukatika umeme na Tanesco kuomba radhi huku wakati mwingine yakitokea nchi nzima.

Masoud katika taarifa yake ya kuomba radhi alieleza kuwa umeme huo ulikatika kutokana na hitilafu katika mashine za mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi wa Songas katika kituo cha Ubungo.

“Tatizo hilo lilifanya mitambo mingine katika mfumo wa Gridi hiyo ya Taifa kuelemewa na mzigo, hali iliyosababisha mitambo hiyo nayo kupata hitilafu na umeme kukatika,” alisema katika taarifa yake wiki iliyopita.

Alisema juhudi zilifanyika mara baada ya tatizo hilo kutokea na shirika kufanikiwa kuurejesha umeme huo katika hali ya kawaida, ingawa kulikuwa na baadhi ya maeneo yaliyochelewa kupata umeme kutokana na matatizo madogo yaliyotokea, hali ambayo pia imeshughulikiwa.

Lakini jana Masoud alikiri kwamba kuharibika kwa mashine kwenye vituo hivyo, ndio chanzo cha kukatika umeme, jambo ambalo jana aliliweka wazi kuwa ulikuwa ni mgawo ambao ulishaanza.

Hali hii inadhihirisha kauli aliyowahi kuitumia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kuwa “ombhisabhisa obhurweri kiriro kirimbura (mficha maradhi kilio humuumbua)”.
CHANZO HABARI LEO

AFANDE ACHUNIA RUSHWA YA DOLA 3000, AZAWADIWA SH 4,000,000





skari namba E. 7235 PC John Anthony Mwesongo wa kituo cha polisi cha Polisi Kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere ambaye ni mtunza vielelezo wa kituo hicho, akionyesha hundi ya T. Sh. 4,000,000 motisha baada ya kukataa rushwa ya dola za kimarekani 3,000 na watu waliokamatwa na madawa ya kulevya waliomtaka abadilishe vielelezo hivyo.
Hundi hiyo alikabidhiwa na Inpekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema Jana (13/3/2010) katika ukumbi wa maofisa wa polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Hongera PC John Anthony Mwesongo.
Watoa hongo kuweni makini!!