Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, March 19, 2010

NILIKUWA MZIMA, NILIPATA ULEMAVU WAKATI NAJIFUNGUA-MUME WANGU HANITAKI TENA

Taarifa ya Mama huyu imenisikitisha sana, imenitoa machozi, kuna watu wanapata shida sana jamani, tumsaidie kwa mawazo, ajuwe nini cha kufanya, inaumiza sana.

Habari yako mdogo wangu INNOCENT WA UMBEA.COM, naandika kwa uchungu sana, moyo wangu unaniuma na machozi yananimwagika. Maana sina thamani ya kuishi kama binadamu wengine, naamini nilizaliwa kwa bahati mbaya, Naona bora hata ningekufa nilipozaliwa tu kama alivyokufa mwanangu. alienipa matatizo

Miaka nane iliyopita nikiwa chuoni Tabora, nilizaa na baba mmoja, baada ya kutoka chuo tukaamua kuishi pamoja kwa makubaliano, mtoto akuwe kidogo ndio tubariki ndoa, but since there tukawa busy na kuendelea kufurahia maisha yale, hatukuwa interested tena na kufunga ndoa, (ni kosa ambalo nakubali nililifanya) tulikuwa na maisha ya kawaida sana, ila kwenye upendo hata kama kuna shida huwezi kuona karaha sana, upendo unafunika kila kitu, Nikiwa na Yule baba tulikuwa tumepanga, badae tukajenga kwetu huku Shinyanga. Tukahamia hapa, akanifungulia biashara, nikawa nafuga, Catering, grocery, mambo yakawa safi kabisa,

Mwaka juzi nilipata mimba, tukakubaliana kabisa nizae, na alinihudumia sana hadi naenda kujifungua, nilipofika hospitali wakati najifungua nilipata kifafa cha mimba, nilizaa mtoto ambae alikaa siku tatu akafariki, mwanangu alikuwa wa kike, wakwanza ni wa kiume, niliumia sana,

Kitu ambacho sikielewi hadi sasa, nikwamba baada ya mwanangu kufariki, nilikuwa bado niko hospitali, siku ya nne nikawa siwezi kuamka, yani nikikaa tu miguu haisogei kwenda kokote, ikawa inajaa maji tu, na sehemu ya kiunoni nikawa sihisi chochotekile, nilijua nia maradhi tu na yatakwisha, lakini siku zina kwenda, ikabidi hospitali wanipatie wheel Chair, ili kunisogeza

Nimeumiasana, maana mume wangu amebadilika ghafla, kipnindi cha mwanzo alikuwa ananipendapenda, lakini ss ananichukia ile direct, miradi amempa dada yake ndie awe msimamizi, anasema mimi siwezi, nilijuwa nitapata support yake, roho inauma sana, Napata support toka kwa mwanangu James, nampenda mwanangu, yeye ndie atake nizika,

Kuna watu walinishauri nirudi kwetu, maana ilifikia kipindi akawa ananikashfu, anasema mm ni mzigo, kwanza hatuna vyeti vya ndoa, nimwachie mwanae niondoke, sasa mimi nitaenda wapi na hali hii jamani? Bila yeye kutaka nizae tena ningepata ulemavu huu, Dunia imeniangukia jamani, sina wa kunitetea, mama alishakufa zamani, baba yangu ni mgonjwa nae alikuwa ananitegemea mimi,

Tumechuma mali nyingi sana na baba James, nilimwambia basi nipe nyumba moja(maana ziko tatu) na mtaji kidogo kasha mimi nikakae huko na mwanangu, nitatafuta mtu atakuwa ananisaidia kusimami vibiashara vyangu, anasema atanipa kwa misingi ipi, anasema eti karibia nakufa, hizo mali nitaziharibu tu!, anatamani nife siku yeyote ile anaona kama namchelewesha, inauma sana INNOCENT

Kuna dada mmoja , alinipa jina la blogu yako, akanieleza ilivyo, nikaona namimi niandike ili nipatiwe ushauri, nifanye nini? Natamani hata kujiua, lakini moyo unagoma kufanya hivyo, nisaidieni mwenzenu.

3 comments:

  1. usijiuwe dada mungu simjinga amekutengea mambomazuri nautafanikiwa usijali dada

    ReplyDelete
  2. comment nilotuma nimesahau dada mungu akupe mengi mazuri amin ahmedsha47@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. pole sana mama mungu yupo anakuona

    ReplyDelete