Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, September 4, 2010

MC KESSY ALIVYOPATA JIKO TAREHE 28/08/2010


Mimi ni MC KESSY (Michael F. Kessy ) Wa Millenium Tower Makumbusho,
Hizi ni picha za harusi yangu iliyofanyika katika ukumbi wa Police
Mercie baada ya kutoka kanisa la Katoliki St Joseph Jumamosi ya tarehe
28/08/2010 hizi ni baadhi tu ya picha za ukumbini nikiwa na mke
wangu kwenye keki.

TAIFA STARS YAWIKA MBELE YA WAARABU WA ALGERIA NA KUTOKA SARE 1-1!!



Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo imetoka kifua mbele nyumbani kwa waarabu wa Algeria baada ya kutoka suluhu ya magoli 1-1 mjini Argels na kugawana pointi moja ya kwanza katika kundi lake usiku huu katika kipute kigumu na cha kusisimua ambacho ndiyo kwanza kimemalizika. Ulikuwa ni mpira mgumu lakini pia ulikuwa ni mchezo mgumu katika maamuzi ya refa yaliyokuwa yakikatisha tamaa wakati wote wakati mpira ukiendelea hasa katika kipindi cha pili, Hata hivyo mungu alisimama upande wa Taifa Stars na kulazimisha suluhu hiyo. Shujaa wa mchezo wa leo kwa timu ya Tifa Stars na watazania ni Mchezaji Abdi Kassim "Babi" aliyefunga goli katika kipindi cha kwanza kwa mpira wa mbali na kuifanya Taifa Stars kuongoza kabla ya timu hiyo ya Algeria kusawazisha goli hilo. Kazi kubwa inabaki kwa kocha mkongwe Jean Paulsen, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na watanzania kwa ujumla kujipanga katika mchezo mwingine dhidi ya Moroco m mwanzoni mwa mwezi Oktoba utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Tunatakiwa kujipanga na kuhakikisha tunasonga mbele katika michuano hii ili nasi tuweze kunusa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika miaka miwili ijayo ambazo zimetutupa mkono kwa muda mrefu ukiachilia mbali kumbukumbu iliyoachwa na Kocha Joel Bendera ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo.

AKUTWA AMEKUFA KWENYE BANDA LA MAMA LISHE!


Askari Kanzu wa Kituo Cha Chang'ombe jijini,wakiwa wameubeba mwili wa kijana ambaye hakufahamika, uliokutwa, katika banda la mama lishe, maeneo ya Sokota, Dar es Salaam , chanzo cha kifo chake hakikufahamika.(PICHA NA DOTTO MWAIBALE)

Friday, September 3, 2010

MAMA SALAMA KIKWETE ASHUHUDIA AJALI HANANG




Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete juu kushoto pichani anayewatambulisha wagombea wa udiwani Hanang jana alisimamisha msafara wake na kwenda kuwapa pole wananchi waliopatwa na ajali ya basi lililokuwa likitokea Babati kuelekea Hanang , katika ajali hiyo hakuna mtu aliekufa ila kulikuwa na majeruhi ambapo walikimbizwa hospitalini.



Basi lenye namba za usajili T477 AQN likikwa limepata ajali katika wilaya ya Hanag kata ya Dareda jana hakuna mtu aliyekufa katika ajali hiyo.

Hawa ni wanachi walinusurika katika ajali hiyo wakiwa wamesimama pembezoni mwa barabara wasijue la kufanya mama Salam Kikwete alisimamisha msafara wake na kuwapa pole kwa ajali hiyo.

MKURUGENZI WA MAENDELEO WIZARA YA AWAFUNDA WAREMBO WA MISS VODACOM 2010



Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo nchini Hermas MwasoKo akiwapa hamasa warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania katika Hoteli ya Giraffe ambapo viongozi wa Wizara hiyo walitembelea kambi ya Miss Tanzania kwa nia ya kujionea na kutoa ushauri kwa warembo hao.(kulia) Mkurugenzi Msaidizi anayesaidia Sanaa katika Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Anna Ngoi,(kushoto) Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashimu Lundenga



Mkurugenzi wa Kamati ya mashindano ya Vodacom Miss Tanzania Hashimu Lundega (kushoto) akiwatambulisha Viongozi wa Wizara ya Habari michezo na Utamaduni wakati walipotembelea kambi ya miss Tanzania iliyopo katika Hoteli ya Giraffe wapili kutoka kushoto Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Tanzania Hermas MwasoKo, Mkurugenzi msaidizi anayesaidia Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ANNA NGOI.Afisa Utamaduni Mkuu wa Wizara hiyo Chiku Shomari.Viongozi hao walitembelea kambi hiyo ili kuwapa ushauri mablimbali ikiwemo na kuwahamasisha kujiamini katika shindano la miss Tanzania litakalofanyika Septemba 11 mwaka huu.


Mkurugenzi Msaidizi anaye saidia Sanaa Anna Ngoi (kulia) akisalimiana na baadhi ya Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania Septemba 11 mwaka huu, baada ya kumalizika kwa kuwapa ushauri katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Giraffe,



Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Hermas Mwasoko. wakati alipowatembelea kambini kwao katika Hoteli ya giraffe DAR ES sALAAM.

Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Hermas Mwasoko. wakati alipowatembelea kambini kwao katika Hoteli ya giraffe DAR ES sALAAM

Ustaadhi awaliza watu Mahakamani



Hatimaye yule Ustadhi anayedaiwa kukibaka kibinti cha miaka saba habari zake kuripotiwa na gazeti ndugu na hili la Amani, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Septemba 1, mwaka huu na kusababisha vilio kwa ndugu, jamaa na marafiki zake.

Ustadhi huyo aliyetajwa kwa jina la Abdul Swama Shabani mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, aliliza watu mahakamani hapo baada ya kupandishwa kizimbani na kusomewa madai ya kumbaka binti mwenye umri wa miaka saba (Jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili).

Awali paparazi wetu alishuhudia mahakamani hapo Ustadh huyo akisindizwa na askari Polisi hadi kwa Hakimu, Mhe. Beda aliyesikiliza kesi hiyo.

Mara baada ya kufikishwa kizimbani, Ustaadhi Shabani alisomewa mashitaka na karani wa mahakama hiyo kuwa anadaiwa kumbaka binti huyo ambaye ni miongoni mwa wanafunzi wanaosoma katika chuo anachofundisha.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa binti huyo baada ya kubakwa na mtuhumiwa alirejea nyumbani kwao akiwa analia huku akitembea kwa shida.

Mtuhumiwa amepelekwa rumande, hali iliyosababisha baadhi ya ndugu jamaa na marafiki zake kumlilia huku wengine wakisikitika zaidi kutokana na mkasa wenyewe kutokea kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Warembo Miss TZ watifuana


Washiriki wa Mashindano ya Vodacom Miss Tanzania 2010 walioweka kambi katika Hoteli ya Giraffe iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam, wako katika hali ya kutifuana huku vijembe na majigambo vikichukua nafasi kubwa.

Ijumaa ambalo juzi lilipiga kambi katika eneo hilo kwa saa kadhaa, limebaini hali ya kujiamini kwa kila mrembo ambapo wengine walifikia hatua ya kuwaponda wenzao wakidai wao ndiyo washindi.

Akiongea kwa kujiamini mmoja wa warembo hao anayeliwakilisha Jiji la Dar es Salaam aliyeomba hifadhi ya jila lake alisema kuwa, hajisifii lakini yeye ana kila kigezo cha kuibuka mshindi.

“Hebu cheki mwenyewe figa na sura yangu, unadhani kuna wa kunipiku hapa, hawa wengine ni vinyago vya mpapure wamenisindikiza tu,”alisema mrembo huyo huku akimuonesha paparazi wetu mapozi ya kufa mtu.

Hata hivyo, uchunguzi umebaini kuwa karibia asilimia kubwa ya walimbwende wa mwaka huu ni wakali hali inayosababisha ugumu wa kutabiri nani atavaa viatu vya Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.