Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, September 3, 2010

Warembo Miss TZ watifuana


Washiriki wa Mashindano ya Vodacom Miss Tanzania 2010 walioweka kambi katika Hoteli ya Giraffe iliyopo Mbezi jijini Dar es Salaam, wako katika hali ya kutifuana huku vijembe na majigambo vikichukua nafasi kubwa.

Ijumaa ambalo juzi lilipiga kambi katika eneo hilo kwa saa kadhaa, limebaini hali ya kujiamini kwa kila mrembo ambapo wengine walifikia hatua ya kuwaponda wenzao wakidai wao ndiyo washindi.

Akiongea kwa kujiamini mmoja wa warembo hao anayeliwakilisha Jiji la Dar es Salaam aliyeomba hifadhi ya jila lake alisema kuwa, hajisifii lakini yeye ana kila kigezo cha kuibuka mshindi.

“Hebu cheki mwenyewe figa na sura yangu, unadhani kuna wa kunipiku hapa, hawa wengine ni vinyago vya mpapure wamenisindikiza tu,”alisema mrembo huyo huku akimuonesha paparazi wetu mapozi ya kufa mtu.

Hata hivyo, uchunguzi umebaini kuwa karibia asilimia kubwa ya walimbwende wa mwaka huu ni wakali hali inayosababisha ugumu wa kutabiri nani atavaa viatu vya Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Septemba 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment