Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, September 4, 2010

TAIFA STARS YAWIKA MBELE YA WAARABU WA ALGERIA NA KUTOKA SARE 1-1!!Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo imetoka kifua mbele nyumbani kwa waarabu wa Algeria baada ya kutoka suluhu ya magoli 1-1 mjini Argels na kugawana pointi moja ya kwanza katika kundi lake usiku huu katika kipute kigumu na cha kusisimua ambacho ndiyo kwanza kimemalizika. Ulikuwa ni mpira mgumu lakini pia ulikuwa ni mchezo mgumu katika maamuzi ya refa yaliyokuwa yakikatisha tamaa wakati wote wakati mpira ukiendelea hasa katika kipindi cha pili, Hata hivyo mungu alisimama upande wa Taifa Stars na kulazimisha suluhu hiyo. Shujaa wa mchezo wa leo kwa timu ya Tifa Stars na watazania ni Mchezaji Abdi Kassim "Babi" aliyefunga goli katika kipindi cha kwanza kwa mpira wa mbali na kuifanya Taifa Stars kuongoza kabla ya timu hiyo ya Algeria kusawazisha goli hilo. Kazi kubwa inabaki kwa kocha mkongwe Jean Paulsen, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na watanzania kwa ujumla kujipanga katika mchezo mwingine dhidi ya Moroco m mwanzoni mwa mwezi Oktoba utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Tunatakiwa kujipanga na kuhakikisha tunasonga mbele katika michuano hii ili nasi tuweze kunusa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika miaka miwili ijayo ambazo zimetutupa mkono kwa muda mrefu ukiachilia mbali kumbukumbu iliyoachwa na Kocha Joel Bendera ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo.

No comments:

Post a Comment