Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, September 3, 2010

MKURUGENZI WA MAENDELEO WIZARA YA AWAFUNDA WAREMBO WA MISS VODACOM 2010Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo nchini Hermas MwasoKo akiwapa hamasa warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania katika Hoteli ya Giraffe ambapo viongozi wa Wizara hiyo walitembelea kambi ya Miss Tanzania kwa nia ya kujionea na kutoa ushauri kwa warembo hao.(kulia) Mkurugenzi Msaidizi anayesaidia Sanaa katika Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Anna Ngoi,(kushoto) Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashimu LundengaMkurugenzi wa Kamati ya mashindano ya Vodacom Miss Tanzania Hashimu Lundega (kushoto) akiwatambulisha Viongozi wa Wizara ya Habari michezo na Utamaduni wakati walipotembelea kambi ya miss Tanzania iliyopo katika Hoteli ya Giraffe wapili kutoka kushoto Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Tanzania Hermas MwasoKo, Mkurugenzi msaidizi anayesaidia Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ANNA NGOI.Afisa Utamaduni Mkuu wa Wizara hiyo Chiku Shomari.Viongozi hao walitembelea kambi hiyo ili kuwapa ushauri mablimbali ikiwemo na kuwahamasisha kujiamini katika shindano la miss Tanzania litakalofanyika Septemba 11 mwaka huu.


Mkurugenzi Msaidizi anaye saidia Sanaa Anna Ngoi (kulia) akisalimiana na baadhi ya Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania Septemba 11 mwaka huu, baada ya kumalizika kwa kuwapa ushauri katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Giraffe,Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Hermas Mwasoko. wakati alipowatembelea kambini kwao katika Hoteli ya giraffe DAR ES sALAAM.

Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Hermas Mwasoko. wakati alipowatembelea kambini kwao katika Hoteli ya giraffe DAR ES sALAAM

No comments:

Post a Comment