Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, September 3, 2010

Ustaadhi awaliza watu MahakamaniHatimaye yule Ustadhi anayedaiwa kukibaka kibinti cha miaka saba habari zake kuripotiwa na gazeti ndugu na hili la Amani, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Septemba 1, mwaka huu na kusababisha vilio kwa ndugu, jamaa na marafiki zake.

Ustadhi huyo aliyetajwa kwa jina la Abdul Swama Shabani mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, aliliza watu mahakamani hapo baada ya kupandishwa kizimbani na kusomewa madai ya kumbaka binti mwenye umri wa miaka saba (Jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili).

Awali paparazi wetu alishuhudia mahakamani hapo Ustadh huyo akisindizwa na askari Polisi hadi kwa Hakimu, Mhe. Beda aliyesikiliza kesi hiyo.

Mara baada ya kufikishwa kizimbani, Ustaadhi Shabani alisomewa mashitaka na karani wa mahakama hiyo kuwa anadaiwa kumbaka binti huyo ambaye ni miongoni mwa wanafunzi wanaosoma katika chuo anachofundisha.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa binti huyo baada ya kubakwa na mtuhumiwa alirejea nyumbani kwao akiwa analia huku akitembea kwa shida.

Mtuhumiwa amepelekwa rumande, hali iliyosababisha baadhi ya ndugu jamaa na marafiki zake kumlilia huku wengine wakisikitika zaidi kutokana na mkasa wenyewe kutokea kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment