Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, February 25, 2010

BALOZI DAUDI MWAKAWAGO AFARIKI DUNIA!


HABARI ZILIZOTUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA BALOZI DAUDI MWAKAWAGO (71) AMEFARIKI DUNIA AJFAJIRI LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA KWA TAKRIBAN SIKU TISA AKISUMBULIWA NA MALARIA NA BAADAE NIMONIA.

MSEMAJI WA FAMILIA, YASINI MWAKAWAGO, AMETHIBITISHA HABARI HIZO NA AMESEMA MSIBA UKO MSASANI MADUKA MAWILI JIJINI DAR, NA MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA JUMAMOSI.

BALOZI MWAKAWAGO ATAKUMBUKWA KAMA MWANASIASA NA MWANADIPLOMASIA MWANDAMIZI ALIYESHIKA NYADHIFA MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA WAZIRI WA HABARI NA UTAMADUNI, WAZIRI WA KAZI NA MAENDELEO, WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA.

BALOZI MWAKAWAGO PIA ALIKUWA BALOZI WETU HUKO ITALIA NA BAADAE UMOJA WA MATAIFA, KABLA YA KUSATAAFU. ALIWAHI PIA KUCHAGULIWA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAKATI HUO, KOFFI ANNAN KUWA MSULUHISHI WA MGOGORO NCHINI SIERRA LEONE.

No comments:

Post a Comment