Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, February 25, 2010

WAIMBA INJILI 10 MABACHELA NA MAMBO YAO SAFI


Kwa mujibu wa ‘makabrasha’ yetu, waimbaji hao ‘mabachela’ ni Rose Muhando, Neema Mwaipopo, Sarah Mvungi, Bahati Bukuku, Jane Miso, Upendo Nkone, Stela Joel, Christina Mwang’onda, Catherine Kyambiki na Queen Mchomvu.

MAKUNDI MAKUU MATATU:
Hata hivyo, imebainika kuwa, waimbaji hao wanaishi katika makundi makuu matatu na kila kundi likiwa na sababu yake ya kimaisha.

Imebainika kuwa, katika makundi hayo, wapo walioolewa wakatengana na waume zao kwa sababu zozote zile, kuna waliofiwa na kundi la mwisho ni la wale ambao hawajaipata neema ya kuolewa.
Mkoba wenye ‘vikorokoro’ vya taarifa hizi unasema kwamba, Rose Muhando (licha ya kuwa na watoto watatu kwa baba tofauti), Sarah Mvungi, Queen Mchomvu na Jane Miso hawajabahatika kupata marriage.

Iko ishu ya kidaku kitaa kuwa, Bahati Bukuku, Stela Joel na Catherine Kyambiki, wao kwa sababu moja au nyingine waliwahi kuolewa, lakini wametengana na waume zao na sasa wako alone.
Kimbelembele chetu hakikuishia hapo, kilizidi kupasha kuwa, majonzi yapo kwa waimbaji Christine Mwang’onda na Upendo Nkone ambao wanatumikia maisha ya ujane baada ya kuondokewa na wenza wao some years ago.

WASEMAVYO WAKRISTO:
Hata hivyo, baadhi ya wakristo walioongea na safu hii kwa kutoa ushirikiano makini kuhusu waimba Injili hao walisema kuwa, hakuna wa kumlaumu katika makundi yote matatu.
Walisema wale waimbaji ambao hawajaolewa siku itafika watajikuta wanapata wenzake wao, waliofiwa wapo huru kuolewa (kwa mujibu wa maandiko) na wale waliotengana, kwa neema watazirejea ndoa zao.

ANGALIZO:
Waimba Injili hao wakatakiwa kuishi maisha ya usafi ili iwe leson kwa kwa fansi wao hasa ikizingatiwa kuwa, wanayoyaimba ni maagizo ya Mungu yenye makatazo na maonyo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment