Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, February 25, 2010

JINI LA SALENDA LAMVAA JOTI


Habari zilizozagaa jijini Dar juzi (Jumanne) zilidai kwamba, muigizaji huyo wa ‘segimenti’ ya Asha Ngedere alipata ajali mbaya maeneo hayo alipokuwa katika harakati za kuandaa kipindi kwa kuigiza tukio la jini aliyeyuka na mrembo huyo ambalo linazidi kupata kasi kila kukicha.

Ilielezwa kwamba, mara tu baada ya mataa kuruhusu katika makutano ya Barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Umoja wa Mataifa, Joti alitoka kasi akikimbia ambapo gari ndogo ilimvaa na kumdondosha chini mita chache kutoka pale alipodaiwa kuyeyekuwa mwanamke huyo wiki iliyopita.

Mashuhuda wa ‘eksidenti’ hiyo waliliambia Amani lililofika eneo la tukio ‘fasta’ na kukuta Joti amekimbizwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili kwa huduma ya kwanza kwamba, eneo hilo kwa sasa limekuwa gumzo na hofu inazidi kutanda miongoni mwa wakazi wa jiji hasa wale wanaofanyia kazi zao maeneo ya Posta.

Safari ya umbea.com haikuishia hapo kwani lilitinga Muhimbili ambapo kwa mujibu wa taarifa hospitalini hapo, jamaa huyo alipatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa kuondoka kwani hakuwa amepata majeraha makubwa isipokuwa michubuko kidogo.

Gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu Joti lakini hakuweza kupatikana na badala yake alipotafuta mwanakomedi mwenzake, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema: “Nilikuwa naye hospitalini, kwa sasa mimi niko ‘shooting’ Kariakoo lakini jamaa hajalazwa ameambiwa akapumzike kwa sababu hakuumia sana.”

No comments:

Post a Comment