Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, February 24, 2010

TRAFFIC WAANZISHA KIKOSI KAZI

Na Innocent Lyimo,
Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini kimeanzisha mpango wa kufanyakazi kwa kuwashirikisha askari wa vikosi vingine kama njia ya kupunguza malalamiko kwa askari wa kikosi hicho na kupunguza ajali nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi ACP Mohammed Mpinga, wakati akitoa taarifa ya kikosi hicho hapa nchini. Amesema kuwa mpango huo utasaidia kudhibiti vitendo vya rushwa na kupunguza lawama kwa Polisi wa Usalama Barabarani na hata kupunguza matukio ya ajali za barabarani.
Akizungumzia suala la utoaji wa leseni mpya, Kamanda Mpinga amesema kuwa mikoa tisa imetengwa na imejengewa uwezo wa kutengeneza mifumo ya kompyuta kwa kushirikiana na Mamlaka ya Leseni nchini TRA. Ameitaja mikoa itakayohusika kwa utoaji wa leseni kwa awamu ya kwanza kuwa ni Arusha, Kilimanjaro,Tanga, Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya, Dodoma na Mwanza Kamanda Mpinga amesema kuwa kutakuwa na aina 14 ya Leseni badala ya 8 zinazotumika sasa.
Amezitaja leseni hizo kuwa ni Leseni A zitakuwa 4 A, A1, A2, A3 na Class “C” nitakuwa 4C, C1, C2 na C3. Amesema kuwa Mikoa yote hiyo itakuwa na vyumba maalum vya Komputa ambavyo vitakuwa na Komputer itakayotumiwa na Wakaguzi wa magari watakaochaguliwa kwa ajili ya kutuma cheti cha ushindi (certificate of comprotence) TRA kwa mtandao baada ya dereva kufanyiwa majaribio na kufaulu kupata leseni kwa gari alilojaribu nalo.
Amesema kuwa kwa upande wa TRA nako kutakuwa na vyumba vya Komputa sambamba na Polisi katika mikoa tajwa kwa ajili ya kupokea taarifa hizo hizo ili kutoa leseni baada ya kutumiwa nakala za karatasi za ushindi wa utedeva kutoka vituo vya Traffic. Kamanda Mpinga amesema kuwa utaratibu huu wa vikosi kazi zikienea kwa kila mkoa hapa nchini vitasaidia katika kupambana na makosa ya usalama barabarani na ajali kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Ameyataja matumizi ya vikosi kazi hivyo (Task force) kuwa ni kuongeza mafanikio ya kiutendaji kwa kikosi cha Usalama barabarani kama ilivyo kwa Kanda Maalum dar es Salaam ambapo kwa kutumia mpango huo, polisi wa Usalama barabarani wameweza kupata mafaniko makubwa katika kupunguza matukio ya ajali.
Nao baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa hapa nchini wakitoa taarifa kenye mkutano huo, wamesema kuwa baadhi ya abiria wamekuwa wakiwashabikia madereva waendao kasi na kulilaumu Jeshi la Polisi itokeapo ajali. Wakizungumzia masuala ya uchaguzi mkuu, Washiriki hao wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini kuendelea kutoa elimu kwa Viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wafuasi wao ili wajue wajibu wa Polisi nyakati za uchaguzi.
Na Maohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

No comments:

Post a Comment