Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, February 24, 2010

SHEIKH YAHYA AWAONYESHA NJIA WATOTO WA BABU SEYA


Siku chache baada ya watoto wa Mwanamuziki mwenye jina kubwa katika Muziki wa Dansi Bongo, Nguza Vicking a.k.a Babu Seya, Mbangu Nguza ‘Mashine’ na Francis Nguza ‘Chichi’ kuachiwa huru, mtabiri maarufu jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya Hussein amewaonesha njia za kumtoa baba na kaka yao gerezani...Akizungumzia utabiri wake dhidi ya hukumu iliyotolewa hivi karibuni katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Shekh Yahya alisema, alijua wazi kwamba tatizo hilo lingetokea lakini alidai kuwa lilitokana na sababu za kimila (za akina Babu Seya).

Alisema, anachokiona yeye ni upuuzwaji wa matambiko, kisomo au dua za kikwao, zilizotakiwa kufanywa na Babu Seya zamani, ndiyo matokeo ya mateso wanayoyapata hivi sasa huko gerezani.

Alitawaka watoto hao kutafakari kwanza maisha ya gerezani huku wakiziacha akili zao zitulie, kabla ya kuingia katika hatua ya pili ya kuhangaikia baba na ndugu yao watoke gerezani.

Alisema, baba yao anatoka katika ukoo wa kifalme ambao hutumia jina la Mbangu, lakini kuna mambo muhimu kufuatana na familia na mila za Kabila lao, ambayo mzee wao (Babu Seya) alitakiwa kuyakamilisha zamani, lakini hakufanya hivyo.

“Hakuna mbaya wa tatizo hili, kuna mambo ambayo mzee wenu aliyapuuza katika ukoo wenu, kwahiyo jambo kubwa kwenu kwasasa ni kumuombea na siyo kumuombea yeye tu bali ni kujiombea wote pamoja.
“Mnapaswa kumfanyia sadaka, msome kisomo kabla hajatoka, kwa mila za kwenu. Msije mkasema labda tatizo ni dansi, maana kama ni dansi mmeanza kuimba miaka mingi kabla, ila tatizo ni hilo la kusahau au kupuuza mila.

“Nimefurahi kuwaona, pumzikeni kwanza, halafu siku zijazo nitawaita na kuwaelekeza vizuri juu ya jambo hilo,” alisema Shekh Yahya.
Aidha mtabiri huyo aliwapatia vijana hao fedha kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya kuwasaidia katika mahitaji yao.
Juni 25, 2004, Babu Seya na wanaye, walihukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuwaingilia kimwili watoto wadogo kumi.

No comments:

Post a Comment