Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, February 28, 2010

BERTHDEI YA MUGABE YATINGISHA DUNIA!

RAIS Robert Mugabe amefanya hafla ya siku ya kuzaliwa kwake Ijumaa iliyopita kwa gharama ya dola za Marekani 500,000 (Sh milioni 670/-), ambayo ilirushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa akitimiza umri wa miaka 86.

Sherehe hiyo iliyochukua saa 12 ilimhusisha pia mwanamuziki wa reggae kutoka Jamaica, Sizzla Kalonji, ambaye alisafirishwa na Serikali kutoka nchini mwake maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo, gazeti la Daily Telegraph lilisema.

Wageni katika sherehe hiyo walikula samaki mbalimbali wakiwamo kambakochi na kamba, huku wakinywa pombe kali aina ya Johnnie Walker Blue Label na Chivas Regal Scotch.

Wafuasi wengi wa chama pinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) kinachoongozwa na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai, waliiita sherehe hiyo kama ya ubadhirifu na isiyo na maana, hasa kutokana na nchi kukabiliwa na umasikini mkali, gazeti hilo la Uingereza lilisema.


Tendai Biti, ambaye ni Waziri wa Fedha kutoka MDC chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alikataa kutoa fedha kwa ajili ya sherehe hizo, maofisa walisema, hivyo fedha zilichangwa kutoka vyanzo binafsi na nchi zenye uhusiano na chama tawala cha Rais Mugabe cha Zanu-PF.

No comments:

Post a Comment