Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, February 26, 2010

Polisi yakamata 14 ‘waporao’ barabarani leo asubuhi!


POLISI mkoani Morogoro imekamata watu sita wanaotuhumiwa kuhusika katika matukio ya uporaji kwa kuweka vizuizi barabarani nyakati za usiku kwenye barabara kuu mkoani hapa.

Kamanda wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa, Hemed Msangi, alisema jana kuwa watu hao wamekamatwa kwa siku tofauti katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam na kukiri kushiriki katika matukio hayo.

Alisema miongoni mwao, ni kiongozi wao ambaye aliwahi kuhukumiwa kwa makosa kama hayo na kutumikia kifungo cha miaka 30 katika Gereza la Dodoma na baadaye kuachiwa huru baada ya kukata rufaa ya hukumu hiyo.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Joseph Motuli (30), Peter Isilo (25) Yona Nyigana (34) wote wa Mlandizi B Pwani. Wengine ni James Mahende (29) Mkazi wa Yombo, Dar es Salaam, Samwel Gisine, wa Gairo, Morogoro na Mtigana Isaka (25) wa Buguruni, Dar es Salaam.

Kamanda alisema wanatuhumiwa kuhusika na uporaji Februari 19 mwaka huu saa 8.10 usiku katika kitongoji cha Msosa, Kata ya Mikumi barabara kuu iendayo Iringa.

Alisema katika tukio hilo, viliwekwa vizuizi katika barabara na kupora vitu na fedha taslimu vyenye thamani ya Sh 4,350,000.

Kwa mujibu wa Kamanda, polisi waliweka mtego na ndipo Dar es Salaam akakamatwa Mahende akiwa na bastola aina ya Browning namba 043553 ambayo iliripotiwa kuporwa katika tukio la Februari 19.

Alisema Mahende alifanikisha wenzake kukamatwa. Katika upekuzi uliofanyika katika nyumba za watuhumiwa, ilikutwa mali iliyoporwa.

Nazo ni simu za mkononi 28, kamera mbili, kompyuta mbili, bastola moja, begi lenye nguo za kike na tochi nne za mwanga mkali. Watu hao walikutwa na Sh 1,178,580 na fedha za Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) noti zenye thamani ya Sh 1,300.

No comments:

Post a Comment