Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, February 24, 2010

WATUHUMIWA WAFANYA KITUKO CHA MWAKA MAHAKAMANI TEMEKE


Habari zilizofikia udaku bongo.com leo na kuthibitishwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Helleni Liwa zilisema washtakiwa hao walifanya kituko hicho jana mchana ikiwa ni hatua ya kupinga kile walichokiita kubambikiwa mashtaka.

Habari zaidi zilieleza kuwa awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha, lakini waliachiwa juma lililopita kabla ya kukamatwa tena siku hiyohiyo na kufunguliwa mashtaka mengine.

Jana washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa lengo la kusomewa mashtaka upya, lakini walipoitwa kuingia mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka hayo walikataa, wakidai kuwa walikuwa wakimtaka Hakimu Mfawidhi ili wamwelezee malalamiko yao hayo.

Chanzo chetu cha habari kilichoshuhudia kituko hicho kilisema kuwa baada ya askari kuwalazimisha kuingia mahakamani, ndipo washtakiwa hao walipoamua kuvua nguo zote na kubaki kama walivyozaliwa.

Chanzo hicho kilidokeza zaidi kuwa baada ya kuvua nguo hizo walitoka mahabusu na kwenda kukaa nje karibu na mlango wa kuingilia mahakamani jambo ambalo liliwaacha vinywa wazi watu waliokuwepo mahakamani hapo.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu Hakimu Mfawidhia Liwa alithibitisha washtakiwa hao kufanya kituko hicho na kusema kwamba aliagiza washtakiwa hao wapandishwe kizimbani na kusomewa mashtaka mapya ya kuvua nguo hadharani.

"Ni kweli kabisa tukio hilo limetokea leo muda wa saa 8 hivi mchana, nami nimewashuhudia,"alisema Hakimu Liwa.

Alisema awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha, lakini walifuatiwa mashtaka na kuachiwa huru mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa kabla ya kukamatwa tena na kufunguliwa mashtaka mapya.

"Kwa hiyo jana walifikishwa mahakamani hapo mapema tu kwa ajili ya kusomewa tena mashtaka hayo upya. Walifikishwa mapema tu lakini walipoitwa kuingia mahakamani kusomewa mashtaka walikataa wakidai kuwa wanataka kuonana na mimi," alisema Hakimu Liwa na kuongeza;

"Ndipo nilipoamua kwenda kuwaona ili kuwasikiliza lakini nikawakuta wako uchi wa mnyama kama walivyozaliwa, na baada ya kuwakuta katika hali hiyo nikawambia siwezi kuzungumza nao wakiwa katika hali kama hiyo, hivyo wakawambeleza wakavaa nguo ndipo nikazungumza nao."

Hakimu Liwa alilieleza Mwananchi kuwa washtakiwa hao walimlalamikia kuwa wamechoka na mashtaka wanayofunguliwa kwani wanakamatwa na kubambikiwa kesi na wanapelekwa mahakamani lakini hakuna ushahidi.

"Lakini niliwaeleza wazi kuwa walichokifanya ni makosa kwani kwani walitakiwa watii kwanza kuingia mahakamani na kama wana malalamiko mengine ndio yangefuata na si kuvua nguo," alisema Hakimu Liwa, na kuongeaza;

"Hivyo kwa kuwa mimi nilikuwa ninaondoka kwenda Mahakama Kuu, nilimwagiza Hakimu Rose Kaliwa ambaye ndiye alikuwa awasomee mashtaka mapya ya leo, awasomee mashtaka ya kuvua nguo mbele ya hadhara"

No comments:

Post a Comment