Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, February 28, 2010

BERTHDEI YA MUGABE YATINGISHA DUNIA!

RAIS Robert Mugabe amefanya hafla ya siku ya kuzaliwa kwake Ijumaa iliyopita kwa gharama ya dola za Marekani 500,000 (Sh milioni 670/-), ambayo ilirushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa akitimiza umri wa miaka 86.

Sherehe hiyo iliyochukua saa 12 ilimhusisha pia mwanamuziki wa reggae kutoka Jamaica, Sizzla Kalonji, ambaye alisafirishwa na Serikali kutoka nchini mwake maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo, gazeti la Daily Telegraph lilisema.

Wageni katika sherehe hiyo walikula samaki mbalimbali wakiwamo kambakochi na kamba, huku wakinywa pombe kali aina ya Johnnie Walker Blue Label na Chivas Regal Scotch.

Wafuasi wengi wa chama pinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) kinachoongozwa na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai, waliiita sherehe hiyo kama ya ubadhirifu na isiyo na maana, hasa kutokana na nchi kukabiliwa na umasikini mkali, gazeti hilo la Uingereza lilisema.


Tendai Biti, ambaye ni Waziri wa Fedha kutoka MDC chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alikataa kutoa fedha kwa ajili ya sherehe hizo, maofisa walisema, hivyo fedha zilichangwa kutoka vyanzo binafsi na nchi zenye uhusiano na chama tawala cha Rais Mugabe cha Zanu-PF.

HUYU NDIE MTANZANIA ALIEPATA MCHONGO WA KURECORD NA AKON


Mwanadada Sarafina mmoja kati ya waafrika watatu tu waliopata bahati ya kuchaguliwa kutoka africa na kurecord ngoma pamoja na video ya nyimbo akon aliyoitengeza kwa ajili ya world cup akiwa na kerry hilson inayoitwa OOH AFRICA.ukiangalia vizuri video hiyo utamuona akiwa amechorwa bendera ya Tanzania.sarafina alipata nafasi ya kuingiza back vocal ya ngoma hiyo.kama humfahamu sarafina alishawahi kushiiriki katika bongo star search mwaka jana lakini hakufanikiwa kuingia kumi bora.

HUYU NDIE MTANZANIA ALIEPATA MCHONGO WA KURECORD NA AKON


Mwanadada sarafina mmoja kati ya waafrika watatu tu waliopata bahati ya kuchaguliwa kutoka africa na kurecord ngoma pamoja na video anyimbo akon aliyoitengeza kwa ajili ya world cup akiwa na kerry hilson inayoitwa OOH AFRICA.ukiangalia vizuri video hiyo utamuona akiwa amechorwa bendera ya Tanzania.sarafina alipata nafasi ya kuingiza back vocal ya ngoma hiyo.kama humfahamu sarafina alishawahi kushiiriki katika bongo star search mwaka jana lakini hakufanikiwa kuingia kumi bora.

Saturday, February 27, 2010

YANAYOJIRI

SPESHO SWALAMU ZA WEEKEND!

Uongozi mzima wa umbeabongo.blogspot.com unawatakia wasmaji wote wa blog hii weekend njema na yenye mafanikio!

ONYO KWA WATUMIAJI WA DAWA ZA KICHINA KUONGEZA MAKALIO




Tukio la karibuni la kijana Gasper Honza, mkazi wa Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam, mengi yameibuka baada ya kuelezwa kuwa, nyeti hiyo inazidi kukua.

Bado imesisitizwa kwamba, kukosewa kwa dozi ya ‘hipson’ ambayo ni maalum kwa ajili ya kukuzia makali ndiyo chanzo cha nyeti hiyo kugeuka ‘zigo’ la kilo 10.

Katika tukio hilo, Honza alikaririwa na gazeti moja la kila siku akielezea mkasa mzima kuwa alifanya uamuzi huo baada ya kutelekezwa na wanawake watatu kutokana na tatizo hilo, hivyo alitaka kuinusuru ndoa yake na mke wa nne.
Alisema kuwa, alitumia dawa hizo baada ya kupata ushauri kutoka kwa rafiki yake wa karibu aliyemtaja kwa jina la Sebastian Mkwema ambaye aliwahi kuwa na tatizo kama hilo.

“Mkwema aliniambia nimpe elfu 30 ili kupata dawa ya kukuza nyeti zangu, siku tatu baadaye aliniletea, nilianza kupaka na kuona nyeti zikiongezeka, nilipata furaha ya kuinusuru ndoa yangu.

“Kwa bahati mbaya nilikosea masharti, ilikuwa nipake kwa muda wa siku mbili tu, mimi nilitumia wiki nzima ambapo matokeo yake ni kama unavyoona sasa (huku akionesha nyeti zake) ni mzigo mkubwa, hata suruali sivai na tendo la ndoa sifanyi.
“Kazi nilishaacha tangu Septemba mosi, mwaka jana,” alinukuliwa.

Kwa upande wake, mke wa Honza, Nancy Kilungi, ambaye alimtelekeza mumewe baada ya nyeti hizo kuvimba alinukuliwa akisema: “Ndugu yangu ndoa ni unyumba …nitaishije? Hakuniambia tatizo lake tangu awali na alishakimbiwa na wake watatu, mimi ni wa nne.

“Alikuwa na ‘mashine’ ndogo kama kidole kidogo cha mkononi, tulishahangaika sana hadi kwa waganga wa kienyeji bila mafanikio,” alisema.

Ilielezwa kwamba, Mkwema ambaye kwa sasa amehamia visiwani Zanzibar, alikiri kumshauri Honza kutumia dawa hiyo ambayo alidai yeye ilimsaidia na sasa ndoa yake ina amani: “Hee ndoa yangu ilikuwa inawaka moto. Mke wangu alikuwa anataka talaka, nilikosa usingizi, lakini Mungu si Athuman… jamaa fulani alinishauri kutumia ‘hypson’ na sasa mambo si mabaya.”

Kwa upande wa familia ya Honza walisema jambo hilo ni la kusikitisha kwani amepoteza uwezo wa kufanya kazi na amekuwa mtu wa kukaa nyumbani tu.

“Yale yale ya akina Michael Jackson. Mungu anakuumba hivi, wewe unataka hivi na vile… tunafanya utaratibu wa kupata matibabu,” alisema mmoja wa wanafamilia hao.

Risasi lilipopiga simu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, mmoja wa watu aliyejitambulisha kwa jina la John Rumisha alitoa onyo kali kwa wale wanaopendelea kutumia dawa za kubadili maumbile kwani madhara yake ni makubwa zaidi ukilinganisha na gharama za dawa hizo.

Alisema kuwa, kumekuwa na ongezeko la watanzania wanaotumia dawa za Kichina kuongeza viungo mbalimbali vya mwili, lakini madhara yake ni makubwa kuliko mtu angeamua kuishi kama alivyoumbwa.

Wiki kadhaa zilizokatika, gazeti ndugu na hili, Ijumaa liliripoti habari ya mwanamke aliyekuwa akilalamika kuteswa na makalio ya Kichina ambaye alilenga kukuza ‘hips’ zake, lakini baadaye alijikuta akiharibika vibaya mwili wake.

Katika siku tulizonazo kumeibuka dawa ambazo zinaelezwa kuwa ni za Kichina ambazo baadhi ya watu waliopata kuzitumia wamekuwa wakikiri kupata madhara makubwa kama vile ‘kalio’ moja kuwa kubwa kuliko jingine, kujazia zaidi chini kuliko juu na mwili kufa ganzi.

WALAZAMISHWA KUFUNGA NDOA NA MBUZI


“Mmoja alikuwa amevua nguo zote na alikuwa amemshikilia mbuzi kichwani wakati mwingine akiendelea kumuingilia kwa nguvu,” aliongea shuhuda wa tukio hilo, Mario Creva wakati akihojiwa na Radio Mozambique.

Mmiliki wa mbuzi aliyefanyiwa kitendo hicho amedai mahakamani kuwa anachokitaka ni kwa watuhumiwa hao kumlipa fidia kwa kumsababishia maumivu mbuzi wake na pia kulipa mahari tayari kwa sherehe ya ndoa ya kimila kati ya vijana hao na mbuzi wake.

Mwendesha mashtaka wa wilaya, Bwana Leonides Mapasse alitoa ufafanuzi kuwa vijana hao watakabiliwa na shtaka la kuiba mbuzi na kumfanyia ukatili kinyume na haki za kimataifa za wanyama, na endapo watapatikana na hatia watahukumiwa kulingana na sheria.

Friday, February 26, 2010

HUKUMU YA LILWAYNE YAAHIRISHWA


Rapper Maarufu Dwayne Carter a.k.a LilWayne or the Best Rapper Alive alituhumiwa kumiliki silaha kinyume na sheria baada ya bunduki za kutosha kukutwa katika nyumba yake pamoja na Tour Bus yake. Rapper huyo alikubali makosa na hivi juzi alifika mahakamani na kunyamaza kimya kama mtu aliyemwagiwa maji ya baridi. Wakili wake alimtetea kwa kudai kwamba Lilwayne alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya meno yaliyompa maumivu makali kiasi cha kushindwa kuongea. Kwasababu hiyo, kesi yake imesogezwa mpaka march 2 mwaka huu ambapo hukumu yake itapitishwa.

OMBAOMBA, HALI YAZIDI KUWA TETE


Watoto wa mitaani wanaoishi katika mazingira magumu wakiwa wamelala nje ya jengo la PPF Tower leo asubuhi.Watoto hawa mara nyingi sana muda kama huo ndio wanakuwa katika mihangaiko yao ya kutafuta riziki lakini leo hii muda huu wamelala,sasa sijui ni kutokana na kukosa msaada kutokana na ile issue ya Manyoya??

SERENA KUJENGA SHULE NYINGI AFRIKA



MCHEZA tenisi namba moja katika ubora wa wachezaji tenisi wanawake duniani anayetokea Marekani Serena Williams amesema ana mpango wa kusaidia kujenga shule moja mpya katika sehemu mbalimbali za Afrika kila mwaka ili kuweza kuwasaidia watoto wa Afrika.

Serena ambaye hivi sasa yupo Barani Afrika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kijamii akiwa balozi wa kampuni ya HP ambayo inatengeneza kompyuta na vifaa vingine vya kiteknolojia, amesaidia ujenzi wa shule nchini Kenya, Senegal na Afrika Kusini, pia amesaidia kulipa ada za wanafunzi na amejiunga katika mpango wa kutokomeza malaria nchini Ghana.

"Ni dhamira yangu kufungua shule nyingi kwa ajili ya maelfu ya wanafunzi barani Afrika ambao hawajapata nafasi ya kwenda shule kupata elimu. Nimepanga kujenga shule moja kila mwaka,"alisema Serena mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa ziara yake ya siku tatu nchini Kenya, ambapo alifungua shule ya sekondari huko Makueni kilomita 150 kusini mashariki ya Nairobi.

JE WAYAJUA MAGARI MATATU GHALI KULIKO YOTE DUNIANI??



Namba moja inakamatwa na Bugati Veyron linalouzwa kwa dola za kimarekani $1,700,000, hili ndilo gari ghali kuliko yote linalopatikana sokoni kwa hivi sasa. Ni gari lenye speed na uwezo mkubwa kushinda yote likifika 60 mph ndani ya sekunde 2.6 likiwa na top speed ya 253mph

Lamborghini Reventon



Lamborghini Reventon imeshikilia nafasi ya pili likiwa linauzwa kwa dola za kimarekani $1600,000. Linachukua sekunde 3.3 kufika 60mph likiwa na top speed ya 211 mph

Mc Laren F1


McLaren F1 Inakamata nafasi ya tatu kwa kuuzwa $970,000. Mwaka 1994, McLaren F1 lilikuwa gari lenye spidi kushinda yote na ghali kuliko yote. Gari hili lina top speed top speed ya 240 mph na linafika 60 mph in 3.2 seconds.

JAMANI NANI ALAUMIWE NANI KATI YA SERIKALI NA MZAZI WA MTOTO HUYU!


Hii ni hali ya kusikitisha kwa mtoto kama huyu kukutwa anafanya biashara ya kuchoma mahindi na ilikuwa ni muda wake binafsi waku wa shule je nina alaumiwe kati ya mzazi au serikali wewe ukiwa kama mdau tunaomba mchango wako ili tuweze kuwanusuru watoto kama hawa!

miss vodacom tanzania 2009/10 miriam gerald apandishwa tena kizimbani jana!


Miss Vodacom Tanzania 2009/10 Miriam Gerald na mpenzi wake Kenedy Victor ‘Kenny’, jana wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kinondoni kwa mara nyingine, ambapo kesi yao ya kushambulia na kuharibu mali na vyombo vya muziki vya bendi ya Volcano Sound, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba ilitajwa.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21 na watuhumiwa hao wanaendelea kuwa nje kwa dhamana.

Polisi yakamata 14 ‘waporao’ barabarani leo asubuhi!


POLISI mkoani Morogoro imekamata watu sita wanaotuhumiwa kuhusika katika matukio ya uporaji kwa kuweka vizuizi barabarani nyakati za usiku kwenye barabara kuu mkoani hapa.

Kamanda wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa, Hemed Msangi, alisema jana kuwa watu hao wamekamatwa kwa siku tofauti katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam na kukiri kushiriki katika matukio hayo.

Alisema miongoni mwao, ni kiongozi wao ambaye aliwahi kuhukumiwa kwa makosa kama hayo na kutumikia kifungo cha miaka 30 katika Gereza la Dodoma na baadaye kuachiwa huru baada ya kukata rufaa ya hukumu hiyo.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Joseph Motuli (30), Peter Isilo (25) Yona Nyigana (34) wote wa Mlandizi B Pwani. Wengine ni James Mahende (29) Mkazi wa Yombo, Dar es Salaam, Samwel Gisine, wa Gairo, Morogoro na Mtigana Isaka (25) wa Buguruni, Dar es Salaam.

Kamanda alisema wanatuhumiwa kuhusika na uporaji Februari 19 mwaka huu saa 8.10 usiku katika kitongoji cha Msosa, Kata ya Mikumi barabara kuu iendayo Iringa.

Alisema katika tukio hilo, viliwekwa vizuizi katika barabara na kupora vitu na fedha taslimu vyenye thamani ya Sh 4,350,000.

Kwa mujibu wa Kamanda, polisi waliweka mtego na ndipo Dar es Salaam akakamatwa Mahende akiwa na bastola aina ya Browning namba 043553 ambayo iliripotiwa kuporwa katika tukio la Februari 19.

Alisema Mahende alifanikisha wenzake kukamatwa. Katika upekuzi uliofanyika katika nyumba za watuhumiwa, ilikutwa mali iliyoporwa.

Nazo ni simu za mkononi 28, kamera mbili, kompyuta mbili, bastola moja, begi lenye nguo za kike na tochi nne za mwanga mkali. Watu hao walikutwa na Sh 1,178,580 na fedha za Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) noti zenye thamani ya Sh 1,300.

MHESHIMIWA KIKWETE AREJEA BONGO


Pichani ni Mheshimiwa Rais kikwete katika Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili kutoka nje ya nchi ambapo alikuwa katika ziara ya kikazi Mashariki ya Kati.Pembeni yake ni mkuu wa mkoa wa Daresalaam na Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwilu

Thursday, February 25, 2010

JINI LA SALENDA LAMVAA JOTI


Habari zilizozagaa jijini Dar juzi (Jumanne) zilidai kwamba, muigizaji huyo wa ‘segimenti’ ya Asha Ngedere alipata ajali mbaya maeneo hayo alipokuwa katika harakati za kuandaa kipindi kwa kuigiza tukio la jini aliyeyuka na mrembo huyo ambalo linazidi kupata kasi kila kukicha.

Ilielezwa kwamba, mara tu baada ya mataa kuruhusu katika makutano ya Barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Umoja wa Mataifa, Joti alitoka kasi akikimbia ambapo gari ndogo ilimvaa na kumdondosha chini mita chache kutoka pale alipodaiwa kuyeyekuwa mwanamke huyo wiki iliyopita.

Mashuhuda wa ‘eksidenti’ hiyo waliliambia Amani lililofika eneo la tukio ‘fasta’ na kukuta Joti amekimbizwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili kwa huduma ya kwanza kwamba, eneo hilo kwa sasa limekuwa gumzo na hofu inazidi kutanda miongoni mwa wakazi wa jiji hasa wale wanaofanyia kazi zao maeneo ya Posta.

Safari ya umbea.com haikuishia hapo kwani lilitinga Muhimbili ambapo kwa mujibu wa taarifa hospitalini hapo, jamaa huyo alipatiwa huduma ya kwanza na kuruhusiwa kuondoka kwani hakuwa amepata majeraha makubwa isipokuwa michubuko kidogo.

Gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu Joti lakini hakuweza kupatikana na badala yake alipotafuta mwanakomedi mwenzake, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema: “Nilikuwa naye hospitalini, kwa sasa mimi niko ‘shooting’ Kariakoo lakini jamaa hajalazwa ameambiwa akapumzike kwa sababu hakuumia sana.”

MATUMAINI YA OWEN KUCHEZEA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND YAFIFIA


Mshambuliaji wa Manchester United Michael Owen.


Mshambuliaji wa timu ya Manchester United Michael Owen ameondoa matumaini ya kuwemo katika kikosi cha England cha kuwania Kombe la dunia mwaka huu.
Owen, mwenye umri wa miaka 30, ambaye alifunga mabao 40 katika michezo 89 aliyowahi kuichezea England, mara ya mwisho kuichezea timu ya taifa ilikuwa mwezi wa Machi mwaka 2008.
Meneja wa England Fabio Capello amesema wachezaji ni lazima wawe wanacheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza katika timu zao, lakini Owen bado hajachomoza zaidi katika kikosi cha kwanza cha Manchester United.

WAZIRI MKUU MH.PINDA ATOA TAMKO HANA KIU NA IKULU!


Waziri Mkuu ametoa msimamo huo jana mjini Tabora, baada ya mshairi Ramadhan Katwila ‘ Mv Liemba’, kusoma shairi akimwomba Mungu kumjaalia awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza ngwe yake mwaka 2015.

Pinda amesema hana hamu ya kuwa Rais, kwa sababu ni kazi ngumu tofauti na watu wanavyofikiri.

“Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere) alisema Ikulu si mahali pa kukimbilia, msifikiri kauli ile ni ya uongo.“Urais ni kazi ngumu. Hata hii kazi ya uwaziri mkuu ni ngumu sana, sema kwa vile tu ni lazima mzigo mzito akabidhiwe ‘Mnyamwezi’.

“Ni kazi ambayo kila mtu anakutupia lawama hata ambazo hustahili. Utasikia mwingine anasema kwanza liangalie lilivyo, kila siku utaandamwa na magazeti na kila mara utajikuta kwenye ‘The Komedi’,” alisema Waziri Mkuu.

Hata hivyo, alisema atakuwa tayari kumuunga mkono mtu yeyote atakayejitokeza kuwania urais baada ya kipindi cha Rais Kikwete kumalizika.

Awali Mwenyekiti mstaafu wa CCM wa Mkoa wa Tabora, Juma Nkumba, alimwomba Mungu ampe rehema Rais Kikwete aweze kumteua tena Pinda kuwa Waziri Mkuu mara baada ya kushinda uchaguzi mkuu ujao.

Jana Waziri Mkuu alikagua bwawa na lambo la Imalamihayo ambalo linatumika kama kuogesha mifugo ya wafugaji wa eneo hilo.

Akihutubia wafugaji hao, Pinda aliwataka wapunguze idadi ya mifugo ili kufuga kisasa na kuongeza tija na faida.

Alisema wilaya ya Tabora ina ng’ombe 54,000 ambao ni wengi kulingana na eneo hilo na hivyo kuathiri malisho ya mifugo hao hatua ambayo inawafanya kukosa afya inayotakiwa.

Baadaye Waziri Mkuu alifungua sekondari ya Nkumba ambayo ni kwa ajili ya wakazi wa kata ya Uyui na ambayo inakabiliwa na uchache wa walimu, ukosefu wa maabara, umeme na maji.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga, aliwachangia wafugaji wa Imalamihayo Sh 100,000 na kutangaza kujenga kisima cha maji shuleni Nkumba, hatua ambayo wananchi katika jimbo hilo walisema angeifanya mapema bila kusubiri ujio wa Waziri Mkuu.
Na mwana habari wetu DSM

HAHAHAHA


Pichani ni President wa America akiangua kicheko baada ya kucheki baadhi ya vitimbi vya wabongo. Tulipata kazi sana kuipata picha hii, ilitubidi tutumie njia za ukachero na hatimaye tulifanikiwa, hii yote ni kwasababu tunapenda wadau wetu mfurahi na mjue matukio yote yanayojiri katika dunia hii.

WAIMBA INJILI 10 MABACHELA NA MAMBO YAO SAFI


Kwa mujibu wa ‘makabrasha’ yetu, waimbaji hao ‘mabachela’ ni Rose Muhando, Neema Mwaipopo, Sarah Mvungi, Bahati Bukuku, Jane Miso, Upendo Nkone, Stela Joel, Christina Mwang’onda, Catherine Kyambiki na Queen Mchomvu.

MAKUNDI MAKUU MATATU:
Hata hivyo, imebainika kuwa, waimbaji hao wanaishi katika makundi makuu matatu na kila kundi likiwa na sababu yake ya kimaisha.

Imebainika kuwa, katika makundi hayo, wapo walioolewa wakatengana na waume zao kwa sababu zozote zile, kuna waliofiwa na kundi la mwisho ni la wale ambao hawajaipata neema ya kuolewa.
Mkoba wenye ‘vikorokoro’ vya taarifa hizi unasema kwamba, Rose Muhando (licha ya kuwa na watoto watatu kwa baba tofauti), Sarah Mvungi, Queen Mchomvu na Jane Miso hawajabahatika kupata marriage.

Iko ishu ya kidaku kitaa kuwa, Bahati Bukuku, Stela Joel na Catherine Kyambiki, wao kwa sababu moja au nyingine waliwahi kuolewa, lakini wametengana na waume zao na sasa wako alone.
Kimbelembele chetu hakikuishia hapo, kilizidi kupasha kuwa, majonzi yapo kwa waimbaji Christine Mwang’onda na Upendo Nkone ambao wanatumikia maisha ya ujane baada ya kuondokewa na wenza wao some years ago.

WASEMAVYO WAKRISTO:
Hata hivyo, baadhi ya wakristo walioongea na safu hii kwa kutoa ushirikiano makini kuhusu waimba Injili hao walisema kuwa, hakuna wa kumlaumu katika makundi yote matatu.
Walisema wale waimbaji ambao hawajaolewa siku itafika watajikuta wanapata wenzake wao, waliofiwa wapo huru kuolewa (kwa mujibu wa maandiko) na wale waliotengana, kwa neema watazirejea ndoa zao.

ANGALIZO:
Waimba Injili hao wakatakiwa kuishi maisha ya usafi ili iwe leson kwa kwa fansi wao hasa ikizingatiwa kuwa, wanayoyaimba ni maagizo ya Mungu yenye makatazo na maonyo mbalimbali.

IGNITION SWITCH


Wabongo kwa modifkesheni hawawezekani,sasa hii swichi sijui hata imewezekana wezekana vipi kupiga mzigo hapa. Hebu cheki jinsi kitu kimeungwa kwa kutumia mkasi,nafikiri hata yule alieunda hiLi gari siku akikutana nayo hii anaweza kuzimia.

BALOZI DAUDI MWAKAWAGO AFARIKI DUNIA!


HABARI ZILIZOTUFIKIA SASA HIVI ZINASEMA BALOZI DAUDI MWAKAWAGO (71) AMEFARIKI DUNIA AJFAJIRI LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA KWA TAKRIBAN SIKU TISA AKISUMBULIWA NA MALARIA NA BAADAE NIMONIA.

MSEMAJI WA FAMILIA, YASINI MWAKAWAGO, AMETHIBITISHA HABARI HIZO NA AMESEMA MSIBA UKO MSASANI MADUKA MAWILI JIJINI DAR, NA MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA JUMAMOSI.

BALOZI MWAKAWAGO ATAKUMBUKWA KAMA MWANASIASA NA MWANADIPLOMASIA MWANDAMIZI ALIYESHIKA NYADHIFA MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA WAZIRI WA HABARI NA UTAMADUNI, WAZIRI WA KAZI NA MAENDELEO, WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA.

BALOZI MWAKAWAGO PIA ALIKUWA BALOZI WETU HUKO ITALIA NA BAADAE UMOJA WA MATAIFA, KABLA YA KUSATAAFU. ALIWAHI PIA KUCHAGULIWA NA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA WAKATI HUO, KOFFI ANNAN KUWA MSULUHISHI WA MGOGORO NCHINI SIERRA LEONE.

JE HII ILISTAHILI KUWA PENALTY AU LA??


Pichani ni Salomon Kalou wa Chelsea akiwa amepigwa ngwara safi na Walter Samuel wa Intermillan. Inter iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya chelsea. Wababe hawa wa kandanda watakutana katika mechi ya marudiano huko Stamford Bridge tarehe 16 march.

SABUNI YA KICHINA YAHARIBU MAMBO


Honza alifanya uamauzi huo baada ya kutelekezwa na wake watatu kutokana na tatizo hilo, hivyo alitaka kuinusuru ndoa yake ya mke wa nne.

Honza, alisema alitumia dawa hiyo baada ya kupata ushauri kutoka kwa rafiki yake wa karibu Sebastian Mkwema ambaye aliwahi kuwa na tatizo hilo.

“Kwema aliniambia nimpe elfu 30 ili kupata dawa ya kukuza nyeti, ambapo baada ya siku tatu aliniletea dawa hiyo, nilianza kupaka na kuona nyeti zikiongezeka ndipo nilianza kupata furaha ya kuinusuru ndoa yangu.”

“Kumbe nilikosea masharti, ilikuwa nipake kwa muda wa siku mbili tu, mimi nilitumia kwa wiki nzima ambapo matokeo yake ni kama unavyoona sasa (akaonyesha) ni mzigo mkubwa hata suruali sivai na tendo la ndoa siwezi kufanya tena…

Kazi nilishaacha tangu Septemba mosi mwaka jana,” alisema.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mtanzania, mke wa Honza, Nancy Kilungi, ambaye alimtelekeza mumewe baada ya nyeti hizo kuvimba na kufikia wastani wa kilo kumi, alijibu “Ndugu yangu ndoa ni unyumba …nitaishije ? Hakuniambia tatizo lake tangu awali na alishakimbiwa na wake watatu mimi ni wa nne.

Alikuwa na nyeti ndogo mithili ya kidole kidogo cha mkononi, tulishahangaika sana hadi waganga wa kienyeji bila mafanikio, alisema.

Hata hivyo, Mkwema ambaye kwa sasa amehamia visiwani Zanzibar, alikiri kumshauri Honza kutumia dawa hiyo ambayo alidai yeye ilimsaidia na sasa ndoa yake ina amani: ”Hee ndoa yangu ilikuwa inawaka moto. Mke wangu alikuwa anataka talaka jambo ambalo lilininyima usingizi , lakini Mungu si Athuman… jamaa fulani alinishauri kutumia ‘hypson’ sasa mambo si mabaya,” alisema.

Kwa upande wa familia ya Honza walisema jambo hilo ni la kusikitisha kwani amepoteza uwezo wa kufanya kazi amekuwa mtu wa kukaa nyumbani tu.”Yale yale ya akina Michael Jackson. Mungu anakuumba hivi, wewe unataka hivi na vile… tunafanya utaratibu wa kupata matibabu,” alisema mmoja wa familia hiyo.
Uchunguzi unaonyesha kuwa dawa zilizozalisha maafa haya ni kati ya zile zinazotajwa kuwa ni za Kichina.

Wednesday, February 24, 2010

WATUHUMIWA WAFANYA KITUKO CHA MWAKA MAHAKAMANI TEMEKE


Habari zilizofikia udaku bongo.com leo na kuthibitishwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Helleni Liwa zilisema washtakiwa hao walifanya kituko hicho jana mchana ikiwa ni hatua ya kupinga kile walichokiita kubambikiwa mashtaka.

Habari zaidi zilieleza kuwa awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang̢۪anyi wa kutumia silaha, lakini waliachiwa juma lililopita kabla ya kukamatwa tena siku hiyohiyo na kufunguliwa mashtaka mengine.

Jana washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa lengo la kusomewa mashtaka upya, lakini walipoitwa kuingia mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka hayo walikataa, wakidai kuwa walikuwa wakimtaka Hakimu Mfawidhi ili wamwelezee malalamiko yao hayo.

Chanzo chetu cha habari kilichoshuhudia kituko hicho kilisema kuwa baada ya askari kuwalazimisha kuingia mahakamani, ndipo washtakiwa hao walipoamua kuvua nguo zote na kubaki kama walivyozaliwa.

Chanzo hicho kilidokeza zaidi kuwa baada ya kuvua nguo hizo walitoka mahabusu na kwenda kukaa nje karibu na mlango wa kuingilia mahakamani jambo ambalo liliwaacha vinywa wazi watu waliokuwepo mahakamani hapo.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu Hakimu Mfawidhia Liwa alithibitisha washtakiwa hao kufanya kituko hicho na kusema kwamba aliagiza washtakiwa hao wapandishwe kizimbani na kusomewa mashtaka mapya ya kuvua nguo hadharani.

"Ni kweli kabisa tukio hilo limetokea leo muda wa saa 8 hivi mchana, nami nimewashuhudia,"alisema Hakimu Liwa.

Alisema awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya unyang̢۪anyi wa kutumia silaha, lakini walifuatiwa mashtaka na kuachiwa huru mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa kabla ya kukamatwa tena na kufunguliwa mashtaka mapya.

"Kwa hiyo jana walifikishwa mahakamani hapo mapema tu kwa ajili ya kusomewa tena mashtaka hayo upya. Walifikishwa mapema tu lakini walipoitwa kuingia mahakamani kusomewa mashtaka walikataa wakidai kuwa wanataka kuonana na mimi," alisema Hakimu Liwa na kuongeza;

"Ndipo nilipoamua kwenda kuwaona ili kuwasikiliza lakini nikawakuta wako uchi wa mnyama kama walivyozaliwa, na baada ya kuwakuta katika hali hiyo nikawambia siwezi kuzungumza nao wakiwa katika hali kama hiyo, hivyo wakawambeleza wakavaa nguo ndipo nikazungumza nao."

Hakimu Liwa alilieleza Mwananchi kuwa washtakiwa hao walimlalamikia kuwa wamechoka na mashtaka wanayofunguliwa kwani wanakamatwa na kubambikiwa kesi na wanapelekwa mahakamani lakini hakuna ushahidi.

"Lakini niliwaeleza wazi kuwa walichokifanya ni makosa kwani kwani walitakiwa watii kwanza kuingia mahakamani na kama wana malalamiko mengine ndio yangefuata na si kuvua nguo," alisema Hakimu Liwa, na kuongeaza;

"Hivyo kwa kuwa mimi nilikuwa ninaondoka kwenda Mahakama Kuu, nilimwagiza Hakimu Rose Kaliwa ambaye ndiye alikuwa awasomee mashtaka mapya ya leo, awasomee mashtaka ya kuvua nguo mbele ya hadhara"

T. I AACHILIWA HURU



Habari Nzuri kwa wale wapenzi wa miondoko ya Hiphop, Nguli wa muziki wa aina hiyo ambaye jina lake kamili ni Clifford Joseph Harris Jr aliyezaliwa september 25 1980 huko mjini Atlanta Georgia, Usa. Alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja baada ya kukiri kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria. T.I Amewaahidi mashabiki wake mambo mazuri sababu anakaribia kumaliza album yake ya nne itakayokwenda kwa jina la KING.
Tukae mkao wa kula na tutarajie mengi kutoka kwa rapper T.I.

AFRICAN FOOD




KWA WALE WADAU WA PANDE HIZI LEO MCHANA HUU NILIKUWA KATIKA PITAPITA ZANGU PANDE ZA KL NIKAKUTANA NA MSHIKAJI
TOKA BONGO MAENEO YA NATIONAL STADIUM OPPOSITE GAGA GARDEN
AKISHUGHULIKIA MASWALA FLANI YA MENU YA KIAFRIKA
ITAKAYOFANYIKA IJUMAA HII TAREHE 26/02/2010 PALE GAGA GARDEN
FIKA BILA KUKOSA MENU YAKUFA MTU PESA KIDOGO
MENU ITAKUWA KAMA IFUATAVYO:
CHIPS KAVU RM 4
CHIPS ZEGE RM 8
NYAMA CHOMA MBUZI RM 10 NA 12
MISHIKAKI CHOMA RM 3
KARIBUNI NYOTE BILA KUKOSA WANANGU NAWAHAKIKISHIA HUDUMA BORA NA YA KISASA KABISA
KWA WALE MSIOPAJUA PIGA SIMU +60169960942

HAYA SASA PARTY HILOO WANANGU!!

UKITAZAMA PICHA HII KWA MAKINI, NANI MWENYE HAKI? Nipe Mtazamo Wako Mdau Wangu

MANUARI ZAIOKOA MELI YA TANZANIA



Taarifa iliyotolewa jana na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umesema, maharamia walitaka kuiteka meli hiyo Jumapili iliyopita. Maharamia hao walikamatwa, na kwa mujibu wa CNN walikuwa wanane.

“Baada ya kupokea taarifa ya kuomba msaada kutoka kwa nahodha wa mv Barakaale, helikopta aina ya SH-60B Seahawk, kutoka USS Farragut iliwasili na kuzuia mashambulizi mawili dhidi ya meli hiyo ya Tanzania,” taarifa hiyo ilisema.

Manowari Farragut ni sehemu ya kikosikazi cha kimataifa, kijulikanacho kama Combined Task Force 151, kilichoundwa Januari mwaka jana kwa lengo la kuzuia na kupambana na uharamia.

Lengo ni kulinda usalama wa vyombo vya usafirishaji majini na kuhakikisha kuwa vinakuwa na uhuru wa kupita katika eneo hilo kwa faida ya nchi zote.

Hata hivyo, habari zilizopatikana jana kutoka CNN zilisema jaribio hilo la utekaji nyara lilitokea katika eneo la Ghuba ya Aden.

Msemaji wa kikosi namba tano cha Marekani, Luteni Corey Barker alisema,watuhumiwa hao baadaye walichukuliwa na manowari hiyo ya Marekani.

Meli hiyo ya Tanzania ilishambuliwa katika eneo hilo hatari na kuvitaarifu vyombo vingine kwa njia ya redio kuhusu tukio hilo kabla ya helkopta kuwasili.

“Wakati wa shambulizi hilo … mabaharia walitumia mbinu za kujihami” ambazo zilisababisha watuhumiwa hao kudondoka baharini wakati wakijaribu kuingia ndani ya meli hiyo, kikosikazi hicho kilisema.

Mtuhumiwa mmoja aliokolewa na mashua ndogo ya maharamia, lakini alijaribu tena kuingia katika meli bila mafanikio.

Kuwasili kwa helkopta kuliwafanya maharamia hao kukimbia, huku helkopta hiyo ikiifuatilia mashua hiyo na kufyatua risasi kwenye tanga na mashua hiyo kusimama, taarifa ya kikosikazi ilisema.

Baada ya kusimama, askari wa USS Farragut waliingia kwenye mashua na kuwakamata maharamia hao wanane.

Kamanda Bernard Miranda wa majeshi ya wanamaji ya Jamhuri ya Singapore ambaye ndiye mkuu wa kikosikazi hicho, aliwapongeza mabaharia wa Barakaale kwa mbinu zao.

"Nahodha wa Barakaale alifanya kinachotakiwa kwa kukataa kusimamisha meli yake kwa kuiyumbisha na maharamia hao kushindwa kuiparamia,” Miranda alisema katika taarifa yake.

Kikosikazi hicho kiliundwa Januari mwaka jana,kinaendesha shughuli zake katika Ghuba ya Aden na maeneo ya pwani ya Somalia.

Ingawa idadi ya vitendo vya uharamia imekithiri katika eneo hilo, hususan mwaka jana, kikosi hicho kilisema juzi kuwa matukio ya utekaji yaliyofanikiwa yamepungua kwa asilimia 40.

Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Begum Tagi, alikiri kuwa wizara hiyo ina taarifa za tukio hilo, lakini kupitia tovuti ya Marekani.

Akaongeza kuwa bado inasubiri taarifa kutoka vyombo vya ndani kama vile Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra).

“Ni kweli tumesikia taarifa hizi kupitia tovuti ya Marekani ambayo imeonesha meli hiyo inapeperusha bendera ya Tanzania, lakini hatuna taarifa kupitia vyombo vyetu, ila kama wenye meli hiyo watatupatia taarifa pia itakuwa ni vizuri,” alisema Tagi.

Matukio ya uharamia katika pwani ya Somalia yamekuwa yakilenga meli nyingi za mizigo ikiwa ni pamoja na mafuta ambapo maharamia wa kisomali wamekuwa wakidai kikombozi.

Fedha hizo inadaiwa zimekuwa zikitumiwa na waasi wa Somalia wa kikundi cha Al Shabaab kwa ajili ya kupambana na majeshi ya Serikali dhaifu ya nchi hiyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa meli ya Tanzania kushambuliwa na maharamia hao wa kisomali, ambao mwaka jana walifanikiwa kuteka nyara meli iliyokuwa na shehena za silaha za Kenya, lakini wakaiachia baadaye.

SHEIKH YAHYA AWAONYESHA NJIA WATOTO WA BABU SEYA


Siku chache baada ya watoto wa Mwanamuziki mwenye jina kubwa katika Muziki wa Dansi Bongo, Nguza Vicking a.k.a Babu Seya, Mbangu Nguza ‘Mashine’ na Francis Nguza ‘Chichi’ kuachiwa huru, mtabiri maarufu jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya Hussein amewaonesha njia za kumtoa baba na kaka yao gerezani...Akizungumzia utabiri wake dhidi ya hukumu iliyotolewa hivi karibuni katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Shekh Yahya alisema, alijua wazi kwamba tatizo hilo lingetokea lakini alidai kuwa lilitokana na sababu za kimila (za akina Babu Seya).

Alisema, anachokiona yeye ni upuuzwaji wa matambiko, kisomo au dua za kikwao, zilizotakiwa kufanywa na Babu Seya zamani, ndiyo matokeo ya mateso wanayoyapata hivi sasa huko gerezani.

Alitawaka watoto hao kutafakari kwanza maisha ya gerezani huku wakiziacha akili zao zitulie, kabla ya kuingia katika hatua ya pili ya kuhangaikia baba na ndugu yao watoke gerezani.

Alisema, baba yao anatoka katika ukoo wa kifalme ambao hutumia jina la Mbangu, lakini kuna mambo muhimu kufuatana na familia na mila za Kabila lao, ambayo mzee wao (Babu Seya) alitakiwa kuyakamilisha zamani, lakini hakufanya hivyo.

“Hakuna mbaya wa tatizo hili, kuna mambo ambayo mzee wenu aliyapuuza katika ukoo wenu, kwahiyo jambo kubwa kwenu kwasasa ni kumuombea na siyo kumuombea yeye tu bali ni kujiombea wote pamoja.
“Mnapaswa kumfanyia sadaka, msome kisomo kabla hajatoka, kwa mila za kwenu. Msije mkasema labda tatizo ni dansi, maana kama ni dansi mmeanza kuimba miaka mingi kabla, ila tatizo ni hilo la kusahau au kupuuza mila.

“Nimefurahi kuwaona, pumzikeni kwanza, halafu siku zijazo nitawaita na kuwaelekeza vizuri juu ya jambo hilo,” alisema Shekh Yahya.
Aidha mtabiri huyo aliwapatia vijana hao fedha kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya kuwasaidia katika mahitaji yao.
Juni 25, 2004, Babu Seya na wanaye, walihukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuwaingilia kimwili watoto wadogo kumi.

MHH MHH JAMANI... BONGO YA SASA!!!!!!

BAJAJI NA KAUJUMBE KA KIUSHKAJI

TRAFFIC WAANZISHA KIKOSI KAZI


Na Innocent Lyimo,
Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini kimeanzisha mpango wa kufanyakazi kwa kuwashirikisha askari wa vikosi vingine kama njia ya kupunguza malalamiko kwa askari wa kikosi hicho na kupunguza ajali nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi ACP Mohammed Mpinga, wakati akitoa taarifa ya kikosi hicho hapa nchini. Amesema kuwa mpango huo utasaidia kudhibiti vitendo vya rushwa na kupunguza lawama kwa Polisi wa Usalama Barabarani na hata kupunguza matukio ya ajali za barabarani.
Akizungumzia suala la utoaji wa leseni mpya, Kamanda Mpinga amesema kuwa mikoa tisa imetengwa na imejengewa uwezo wa kutengeneza mifumo ya kompyuta kwa kushirikiana na Mamlaka ya Leseni nchini TRA. Ameitaja mikoa itakayohusika kwa utoaji wa leseni kwa awamu ya kwanza kuwa ni Arusha, Kilimanjaro,Tanga, Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya, Dodoma na Mwanza Kamanda Mpinga amesema kuwa kutakuwa na aina 14 ya Leseni badala ya 8 zinazotumika sasa.
Amezitaja leseni hizo kuwa ni Leseni A zitakuwa 4 A, A1, A2, A3 na Class “C” nitakuwa 4C, C1, C2 na C3. Amesema kuwa Mikoa yote hiyo itakuwa na vyumba maalum vya Komputa ambavyo vitakuwa na Komputer itakayotumiwa na Wakaguzi wa magari watakaochaguliwa kwa ajili ya kutuma cheti cha ushindi (certificate of comprotence) TRA kwa mtandao baada ya dereva kufanyiwa majaribio na kufaulu kupata leseni kwa gari alilojaribu nalo.
Amesema kuwa kwa upande wa TRA nako kutakuwa na vyumba vya Komputa sambamba na Polisi katika mikoa tajwa kwa ajili ya kupokea taarifa hizo hizo ili kutoa leseni baada ya kutumiwa nakala za karatasi za ushindi wa utedeva kutoka vituo vya Traffic. Kamanda Mpinga amesema kuwa utaratibu huu wa vikosi kazi zikienea kwa kila mkoa hapa nchini vitasaidia katika kupambana na makosa ya usalama barabarani na ajali kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Ameyataja matumizi ya vikosi kazi hivyo (Task force) kuwa ni kuongeza mafanikio ya kiutendaji kwa kikosi cha Usalama barabarani kama ilivyo kwa Kanda Maalum dar es Salaam ambapo kwa kutumia mpango huo, polisi wa Usalama barabarani wameweza kupata mafaniko makubwa katika kupunguza matukio ya ajali.
Nao baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa hapa nchini wakitoa taarifa kenye mkutano huo, wamesema kuwa baadhi ya abiria wamekuwa wakiwashabikia madereva waendao kasi na kulilaumu Jeshi la Polisi itokeapo ajali. Wakizungumzia masuala ya uchaguzi mkuu, Washiriki hao wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini kuendelea kutoa elimu kwa Viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wafuasi wao ili wajue wajibu wa Polisi nyakati za uchaguzi.
Na Maohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini kimeanzisha mpango wa kufanyakazi kwa kuwashirikisha askari wa vikosi vingine kama njia ya kupunguza malalamiko kwa askari wa kikosi hicho na kupunguza ajali nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi ACP Mohammed Mpinga, wakati akitoa taarifa ya kikosi hicho hapa nchini. Amesema kuwa mpango huo utasaidia kudhibiti vitendo vya rushwa na kupunguza lawama kwa Polisi wa Usalama Barabarani na hata kupunguza matukio ya ajali za barabarani.
Akizungumzia suala la utoaji wa leseni mpya, Kamanda Mpinga amesema kuwa mikoa tisa imetengwa na imejengewa uwezo wa kutengeneza mifumo ya kompyuta kwa kushirikiana na Mamlaka ya Leseni nchini TRA. Ameitaja mikoa itakayohusika kwa utoaji wa leseni kwa awamu ya kwanza kuwa ni Arusha, Kilimanjaro,Tanga, Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya, Dodoma na Mwanza Kamanda Mpinga amesema kuwa kutakuwa na aina 14 ya Leseni badala ya 8 zinazotumika sasa.
Amezitaja leseni hizo kuwa ni Leseni A zitakuwa 4 A, A1, A2, A3 na Class “C” nitakuwa 4C, C1, C2 na C3. Amesema kuwa Mikoa yote hiyo itakuwa na vyumba maalum vya Komputa ambavyo vitakuwa na Komputer itakayotumiwa na Wakaguzi wa magari watakaochaguliwa kwa ajili ya kutuma cheti cha ushindi (certificate of comprotence) TRA kwa mtandao baada ya dereva kufanyiwa majaribio na kufaulu kupata leseni kwa gari alilojaribu nalo.
Amesema kuwa kwa upande wa TRA nako kutakuwa na vyumba vya Komputa sambamba na Polisi katika mikoa tajwa kwa ajili ya kupokea taarifa hizo hizo ili kutoa leseni baada ya kutumiwa nakala za karatasi za ushindi wa utedeva kutoka vituo vya Traffic. Kamanda Mpinga amesema kuwa utaratibu huu wa vikosi kazi zikienea kwa kila mkoa hapa nchini vitasaidia katika kupambana na makosa ya usalama barabarani na ajali kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Ameyataja matumizi ya vikosi kazi hivyo (Task force) kuwa ni kuongeza mafanikio ya kiutendaji kwa kikosi cha Usalama barabarani kama ilivyo kwa Kanda Maalum dar es Salaam ambapo kwa kutumia mpango huo, polisi wa Usalama barabarani wameweza kupata mafaniko makubwa katika kupunguza matukio ya ajali.
Nao baadhi ya Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa hapa nchini wakitoa taarifa kenye mkutano huo, wamesema kuwa baadhi ya abiria wamekuwa wakiwashabikia madereva waendao kasi na kulilaumu Jeshi la Polisi itokeapo ajali. Wakizungumzia masuala ya uchaguzi mkuu, Washiriki hao wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa nchini kuendelea kutoa elimu kwa Viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wafuasi wao ili wajue wajibu wa Polisi nyakati za uchaguzi.