Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, August 27, 2010

SAFARI YA MWISHO YA COSTA MOWO KWENDA KUPUMZIKA MILELE


Rest In Peace, binadamu wote ni kama maua yanaweza kunyauka pasipokutarajia

Thursday, August 26, 2010

SKENDO


The Talented Cute wa Kiwanda cha Filamu Bongo, Jacqueline Wolper anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine na safari hii anasimulia jinsi alivyokoswa-koswa kwenye jaribio la kubakwa na mjomba wake anayeitwa Axaud Macha.

The 5star Paper, Risasi Mchanganyiko lina kisa kamili baada ya kufanya mahojiano na Jacqueline, wiki iliyopita, jijini Dar ambapo pamoja yote aliyosimulia, alisema kuwa lilikuwa ni tukio ambalo anamshukuru Mungu kwamba aliponea chupuchupu.

Alisema, alinusurika kubakwa Jumatatu ya Agosti 16, 2010 nyumbani kwake, Chentemba, Kinondoni, Dar na tukio hilo lipo Kituo cha Polisi Oysterbay likiwa limenakiliwa kwenye kitabu cha Ripoti za Rolisi (Report Book “RB”) nambari OB/RB/14500/2010.

Akisimulia tukio hilo kwa ‘paparazi’ wetu, Jacqueline alisema kuwa alikuwa anamheshimu mjomba wake ndiyo maana hakusita kumkaribisha nyumbani kwake, lakini alichomfanyia kimemfanya amtoe thamani.

Alisema, ni Mungu tu ndiye aliyemsaidia kupona katika jaribio hilo la kubakwa kwasababu mjomba wake alikuwa amekwishamvua nguo za juu na kubakiwa na brazia a.k.a sidiria.

“Jamani nyie waoneni hivi wajomba, kumbe wakati mwingine wana yao kutaka kuonja watoto wa dada zao, huyo mjomba wangu nimemtoa thamani,” alisema Jacqueline.

Akisimulia ‘in&out’, Jacqueline alisema, alianza kuwa karibu na mjomba wake alipotaka kununua gari.



“Nilikuwa na shilingi milioni tatu, nikamuomba mjomba anikopeshe shilingi milioni nne akanikubalia, kwahiyo nikanunua gari aina Crester lenye namba za usajili T704 BBL.

“Nikiwa sijui hili wala lile, mjomba akaenda kuzungumza na polisi wakanikamata eti gari langu ni la wizi na mpaka sasa lipo polisi.

“Siku hiyo akaja nyumbani kwangu, tukiwa wawili tunazungumza, ghafla alinigeuzia kibao na kutaka kunibaka. Akanivua nguo na kuanza kunipiga picha za utupu. Alipotaka kunivua nguo zote nikapiga kelele akakimbia,” alisema Jacqueline.

Akaendelea: “Baada ya hapo amekuwa akitembea huku na huko ili kunichafua na anatishia kuzitoa picha ambazo alinipiga siku hiyo magazetini ili kunichafua.”

Baada ya kupata ishu hiyo, gazeti hili ‘lilimvutia waya’, Macha ambaye alisema kuwa Jacqueline anataka kupotosha ukweli kwa sababu ni demu wake wa muda mrefu.

Alisema, hata gari ambalo Jacqueline anadai ni lake si kweli na kwamba hilo ni mali yake.
“Nilimpa gari na nikampangia nyumba. Yule siyo mtoto wa dada yangu, ni demu wangu. Nilikwenda Magomeni Polisi kutoa taarifa baada ya kuona amekaa nalo muda mrefu bila kurudisha,” alisema Macha na kuongeza:

“Gari nilimuazima na sikumpa, kwahiyo nilipoona harudishi kwanza nikwenda Kijitonyama ambako nilikuwa nimempangia, nikaambiwa amehama. Nikaambiwa yupo Magomeni ambako nako niliambiwa amehama, nikawa sina jinsi nikaenda Polisi Magomeni.
“Polisi aliitwa, alipoulizwa akasema gari ni lake, akaambiwa aoneshe vielelezo vya kumiliki gari akakosa.”

Katika maelezo ya Macha, alisema kuwa baadaye msanii wa maigizo, Rashid Nassor ‘Chiddy’ alikwenda Polisi Magomeni na kujieleza yeye ndiye mmiliki wa gari hilo na alimuazima Jacqueline lakini alipoombwa nyaraka zinazomuonesha yeye ndiye mwenye mali, alikosa.

Gazeti hili, linaendelea kulifanyia kazi sakata hilo na linaahidi kwamba mwisho wa siku litamaliza huu mpira ambao wahusika wanatupiana.

SWAUMU INAPOZIDI

Picha chafu yamtesa Lulu


Staa anayeshikilia kipaji chake kwa mikono miwili ndani ya chimbo la filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, anateswa na picha chafu aliyodai ni ya kutengenezwa inayosambaa mitandaoni huku vijana wakipasiana kama mpira kwenye simu, Risasi Mchanganyiko linaripoti.

Akifafanua ishu hiyo mbele ya gazeti ‘first class’ la mastaa Bongo, Risasi, alipotinga makao makuu ya ‘pepa’ hili, Sinza-Bamaga, Dar hivi karibuni, Lulu alidai kwamba picha hiyo siyo yake asilani bali imetengenezwa na wabaya wake wenye lengo la kumchafulia jina.

Lulu alidai kwamba, picha hiyo inayopatikana zaidi katika Mtandao wa Facebook, inafananishwa na yake hivyo kuiweka kuwa moja ya vitu vinavyoutesa moyo wake kwasasa

Hii ndiyo picha inayomtesa Lulu

“Teknolojia inatuharibia, ukweli ni kwamba ile picha siyo yangu, imetengenezwa kwani kiwiliwili siyo changu, kinachoonekana ni sura yangu lakini sina maumbile ya aina ile,” alisema Lulu na kuongeza:

“Ni moja ya vitu vinavyoutesa moyo wangu kwa sasa.”
Muigizaji huyo ‘Sidanganyiki’ alisema kwamba, amekuwa akijitahidi kuwaelewesha baadhi ya watu wakiwemo wazazi na wanafunzi wenzake wanaomtuhumu kuwa picha hiyo ni yake lakini wanaonekana kutomwelewa.

Lulu alitumia ‘intavyu’ hiyo kuwaomba watanzania waelewe kwamba picha hiyo ambayo Risasi ina ‘kopi’ yake hakuipiga yeye na kwamba watu wanamfananisha tu na katika maisha yake hajawahi kupiga picha za utupu.

“Watanzania ambao ndiyo mashabiki wa kazi zangu wanapaswa kujua kwamba sijawahi kupiga picha ya utupu kama hiyo maishani mwangu na wala sitegemei kufanya hivyo hadi Yesu atakaporudi mara ya pili kuchukua walio hai na wafu,” alisema Lulu na kuongeza:

“Natumia fursa hii kuifahamisha jamii kwamba mimi ni msanii mwenye maadili na ni kioo cha jamii hivyo waendelee kunielewa hivyo na si vinginevyo.”

Tuesday, August 24, 2010

KIFAA KIKO SOKONI KAZI KWENU WADAU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Huyu mtoto ni hot n’ sexy kiasi cha kumtoa nyoka kwenye shimo lake, anakwenda kwa jina la Moshi Mahona (23), aliwahi kushiriki katika Kijiji cha Maisha Plus, Season 0ne, anapatikana Mitaa ya Sinza, White-Inn Dar, in short sistaduu huyu anatafuta mchumba atakayemuoa na kwamba yuko tayari ku-testiwa kwa sharti moja tu, kupima ngoma kwanza. If u need to have dat chick…..plz use 0754-557440 or 0712-956910. watch out to mateja20, mizigo kama hii iko ya kumwaga na tutakuletea mara kwa mara!!!

AJALI MBAYA ILIYOTOKEA ASUBUHI MAENEO YA SHEKILANGO!!


Wakazi wa jijini wakiangalia gari namba T 729 BFD aina ya Fiati likiwa lililopinduka baada ya kugongana na gari lingine aina ya Fuso lililokuwa limebeba nyanya katika makutano ya barabara ya Morogoro na ile inayotoka Sinza maeneo ya shekilango Dar es Salaam asubuhi leo. Katika ajali hiyo dereva wa fuso na kondakta wake walifariki papo hapo na wale waliokuwepo katika Fiati wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili.

KITCHEN PARTY ZA SIKUHIZI NI BALAAA TUPU!!!


Mambo ya kuonyesha bikini yalivyokuwa: kila mtu kivyake.

MIJIMAMA na wasichana kadhaa hivi karibuni “walizishusha heshima zao” kwa muda na kushindana kufanya mambo ya ajabu ikiwa pamoja na kuonyesha nguo zao za ndani (bikini) kwenye sherehe ya kumfunda bibi harusi mteule (kitchen party) iliyofanyika katika ukumbi wa Hedema maeneo ya Msamvu mjini Morogoro.

Baadhi ya watu waliokuwa hapo walionekana kuchefuliwa na vitendo hivyo ambapo baadhi ya waliovifanya ni wake za watu

KITU HADHARANI KWEUPE


Mnenguaji wa Akudo Impact akiwa bize na staili ya pekechapekecha!!!!!!!!!!!ILA DAAAH WADAU DIS IZ TOOO MUCH JAMANI!!

Monday, August 23, 2010

NEWS TOKA JIACHIEBLOGSOT......suala la kujichukulia sheria mkononi litakoma lini ndani ya jamii yetu.


Mtu aliyeniletea picha hii alisema huu si ustaarabu hata kidogo na mimi nakubaliana naye. Aliyeleta taarifa hii aliniletea jumla ya picha kumi za mtu anayechomwa moto kwa kutuhimiwa wizi wa pikipiki.Zipo za karibu na nyingine ambazo hazitamaniki hii ina nafuu nimeibadika kuwasilisha ombi la mleta habari.Alisema kwamba polisi wa Kimara walifika eneo hilo muda mfupi kabla hajachomwa moto wakajiondokea ambapo wangeliweza kuokoa maisha ya mtuhumiwa huyu.



Watu wamechukua sheria mkononi wameua na kumchoma moto mtu ambaye hana makosa kwa kudhani kwamba ameiba pikipiki wakati alikuwa ametumwa mafuta na fundi ambaye alikuwa anatengeneza pikipiki hiyo.

Tukio hili la kusikitisha limetokea Jumamosi wiki hii na mbaya zaidi nimeibandika kwenu japo haipendezi kuweka lalamiko la msomaji kwamba polisi hawakujitahidi kuzuia mauaji haya.Picha na Rahabu/Kimara

Blog ya Jiachie inalaani na itazidi kulaani vikali vitendo ya namna hii vya kujichukulia sheria mkononi,ambavyo vimekuwa vikiibuka mara kwa mara ndani ya jamii yetu na kusababisha kupoteza uhai wa watu,Wanajamii tuachane na tabia hii ya kujichukulia sheria mkononi,Sheria zipo kwa ajili ya kulinda na kutetea haki ya kila mwanajamii,basi na itumike njia hiyo ya kufuata sheria.
Asante,nawakilisha.

Mwanamke Shurti Utundu..Kitandani..


Unakuta msichana mzuri,she got it all lakini mpenzi wake au mume ana-mcheat…..Sometimes sisi (wanawake) tunakuwa sababu ya wapenzi wetu kwenda nje na kutuacha ndani….You dont need to act like he is your brother na wakati unajua kabisa ni Mpenzi wako….Do something extra on bed uweze kumchanganya mpenzio.
A friend of mine,I mean Male friend was telling me kisa ambacho kikanigusa hata nikasema itabidi tu nikiweke ili tujifunze kutoka kwa wenzetu.He told me alikuwa anadate this girl,presentable one lakini msichana mwenyewe anabore to the extent when it comes to sexy bcause she feeeling shy and all that..Mwisho wa siku akaamua abwage manyanga ingawa relationshiop is not all about sexy but it matterz banaaa!kaka wa watu akaamua KUSEPA loll!



Sasa ukijiuliza bi dada alikuwa anaona aibu ya nini na wakati wako wawili tu chumbani jamani?????Hapo inakuja my point kuwa saingine sisi wanawake tunachangia kuvunja mahusiano yetu kwasababu when he goes outside,atakutana na yule ambaye Kichaa to the maximum na anafanya mautundu yote ikiwa ni pamoja na kumchanganya mwanaume…Sasa wewe aibu ya nini???Grow Up ,show what you got from your mama!

Sunday, August 22, 2010

MCHINA WA KIBONGO!!!!!!!!!!!!!!!!


Baba,Mama na Mtoto wakiwa katika pikipiki yao kwa staili ya kichina china,sasa sijui inakuwaje katika swala zima la kiusalama.maana huyo dereva anaonekana ni mwanafunzi kutokana na hiyo alama hapo nyuma,pili hicho kiti hapo nyuma kilichokaliwa na mtoto,tatu wao wazazi wamevaa kofia za kiusalama na mtoto amepozi kimpango wake.daah hii kweli bongo daslam

AKU MIE SIMO!!!!!

Saturday, August 21, 2010

SAFARI YA WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA KUTOKA DAR ES SALAAM-ARUSHA!!



Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakipita kando ya daraja la mto Wami lililop[o Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani jana wakiwa safarini kuelekea mikoa ya Kilimnjaro na Arusha katika mbuga za Wanyama na vivutio vya Utalai



Baadhi ya Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakipiga picha kando ya daraja la mto Wami lililop[o Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani jana wakiwa safarini kuelekea mikoa ya Kilimnjaro na Arusha katika mbuga za Wanyama na vivutio vya Utalaii

Baadhi ya Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakifanya manjonjo yao mbele ya Kamera ya Video kando ya daraja la mto Wami lililopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani jana wakiwa safarini kuelekea mikoa ya Kilimnjaro na Arusha katika mbuga za Wanyama na vivutio vya Utalaii.

Friday, August 20, 2010

MATUKIO YA WADAU XUL LEO!!!!!!!!!



Msiba Algeria


Uongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa kitanzania wanaosoma nchini Algeria (ATSA), wanasikitika kutoa taarifa ya kifo cha mwanafunzi mwenzao ndugu Felix Matela, kilichotokea siku ya tarehe 05/08/2010 Jijini Algiers nchini Algeria.

Ndugu Felix alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Houari Boumediene (USTHB) Kilichopo jijini Algiers , Algeria . Alikuwa akiishi katika Hostel za chuo zinazotambulika kwa jina la CUB 3.

Uongozi unatoa shukrani za dhati kwa wizara ya elimu na ufundi na ubalozi wa Tanzania-Paris, Ufaransa kwa ushirikiano wao mkubwa katika kuhakikisha usafirishaji wa mwili wa marehemu kurudishwa nyumbani unakamilika pia uongozi unatoa shukrani kwa serikali ya Algeria kwa kujitolea kusafirisha mwili wa marehemu mpaka Tanzania.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa hivi karibuni mara tu taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu zitakapo kamilika.

Tunawasihi familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehem.

Uongozi – ATSA.
00213551713920,
00213553271791
tz_students@yahoo.fr

AMBULANCE


Shida ya usafiri kwa wagonjwa sio vijijini tu, bali hata kwa watu wa hali ya chini ambao wako Dar es salaam ama miji mingine mikubwa yanawakumba kama haya. Sijui hali itaendelea mpaka lini landa zikijengwa zahanati kila kijiji

Wafanyakazi: Tutampigia kura Jakaya Kikwete


Rais Jakaya Kikwete

Wakati Shirikisho la Vyama vya Wanyakazi nchini (TUCTA) likidaiwa linajipanga kutoa tamko la kuwataka wafanyakazi wote nchini kutompigia kura Rais Jakaya Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010, inaonekana mambo ni kinyume.

Sehemu kubwa ya wafanyakazi wanaeleza kufurahishwa na utawala wa JK, hivyo kuwa tayari kumuongezea kipindi kingine cha uongozi cha miaka mitano (2010-2015).

Wafanyakazi waliozungumza na gazeti hili kwa wiki nzima iliyopita, Dar es Salaam, walieleza kufurahishwa na kazi ya JK aliyoifanya Ikulu kwa miaka mitano, hivyo wanaamini ataendeleza mazuri endapo ataongezewa kipindi kingine.

Walisema kuwa Rais Kikwete ameweza kuonesha moyo mzuri kwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi mara kwa mara pia kukabiliana na ufisadi, hivyo hawaoni sababu ya kuliunga mkono TUCTA endapo litasema JK asipigiwe kura.
Baadhi ya maoni ya wafanyakazi kama walivyozungumza ni kama ifuatavyo;

ITUS BILLA
Mfanyakazi wa Kampuni ya Big Bell.
Anasema: “Nafurahia kipindi chote cha Kikwete kuwepo madarakani, maana mengi aliyoahidi ametekeleza. Nawashauri Watanzania wenzangu tumuongezee kipindi kingine aweze kuleta maendeleo zaidi. Kuhusu nyongeza ya mshahara mimi naona maisha yatakuwa yale yale kwani kila mshahara ukitangazwa kupanda na bidhaa nazo zinapandishwa.”

SULEIMAN MAZINGE
Anasema: “Utawala wa Rais Jakaya Kikwete ni mzuri kwani nchi ina amani na hakuna njaa wala migogoro na hilo ndilo jambo kubwa, mambo mengine ni majaaliwa. Kuhusu ongezeko la mishahara hapo hakutakuwa na jipya kwani uzoefu unaonesha mishahara ikipanda na huduma nazo zinapanda.”

ANNA LUWENA
Anasema: “Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri na anaomba uendelee ingawa hauna tofauti kubwa na tawala zingine zilizopita. Kuhusu kupanda kwa mishahara ni bora ingebaki palepale kwani ongezeko la mishahara litasababisha kuongezeka maradufu kwa gharama za huduma mbalimbali.”

HUSSEIN MAKUBI
Anasema: “Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri kwani ameendeleza mazuri yaliyoachwa na marais waliopita. Kuhusu mishahara mwanzoni wananchi watafurahia ongezeko hilo lakini siku zinavyokwenda huduma nazo taratibu zitapanda na kufanya hali kuwa ile ile.”

BABY OMARY
Anasema: “Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri hakuna dosari kubwa iliyojionesha ukilinganisha na tawala zilizopita.
Ongezeko la mishahara linatokana na kusonga kwa dunia lakini halina uhusiano wowote na ubora wa maisha kwani hapo zamani mfanyakazi alilipwa 6000/ (elfu sita) mfanyakazi huyo sasa hivi analipwa 600,000/ (laki sita) lakini maisha yake ni yaleyale afadhali ya zamani.

HADIJA HASSAN
Mfanyakazi wa Kampuni ya Vodacom anasema: “Utawala wa Rais JK ni mzuri na hasa kwa kuwa ametoa ajira kama alivyoahidi, hivyo kuwakomboa Watanzania. Ongezeko la mishahara anasema litakuwa na mafanikio kwa wenye malengo lakini wasio na malengo wataendelea kuumia.”

GHONCHE MATEREGO
Katibu Mtendaji wa BASATA, anasema: “Rais Kikwete uongozi wake ni mzuri sana pia ni mtu anayeona mbele zaidi ndiyo maana anawapa vijana kipaumbele tena anapenda kuwarithisha ili baadaye wawe viongozi wanaofaa kuongoza nchi. Amekuwa ni mchango mkubwa sana kwa vijana, lakini hajawaacha wazee anawataka kuelimisha vijana wao ili waweze kujikwamua kimaisha.

“Kwa upande wa mshahara kuongezwa hilo nalo ni jambo la heri na serikali imetimiza ahadi yake kwani kilikuwa ni kilio cha siku nyingi na sasa imefikia mahali na kuongeza tunashukuru kwa kutimiza ahadi hiyo.”

MBAZI OMBENI
Karani wa BASATA, anasema: “Utawala wa Rais Kikwete siyo mbaya sana lakini kuna ahadi ambazo naomba kama akichaguliwa tena awamu ya pili azitekeleze. Shule za Kata zimejengwa nyingi lakini vitendea bado tatizo, naomba aliangalie hilo pamoja na mfumuko wa bidhaa sokoni.
“Suala la mishahara kuongezwa nashuru kwa sababu kilikuwa kilio chetu cha siku nyingi.”

Redd's yaanza mchakato wa kumpata balozi wake



Meneja wa bia ya Redd's,Dada Kabula Nshimo (kati) akifafanua jambo mbele ya warembo washiriki wa Miss Tanzania 2010.wengine ni Dada Edith (shoto) na Victoria



Baadhi ya Warembo watakaoshiriki kinyang'anyiro cha Miss Tanzania 2010 wakisikiliza kwa makini




utulivu na usikivu ulitawaka wakati Da Kabula akiongea





Warembo washiriki wa Miss Tanzania 2010 wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa bia ya Redd's mara baada ya mkutano wa kumsaka balozi wa Redd's kumalizika leo katika hotel ya Gerrafe,mbezi beach

Tuzo ya Balozi wa Mitindo wa REDD’S ilianza kwa mara ya kwanza mwaka 2005 ambapo ndio mwaka wa kwanza kwa REDD'S kudhamini Miss Tanzania. Na alieleza kushikilia taji hilo alikuwa ni Natalia Noel Yatera ambaye pia alikuwa mshindi wa pili wa Ocean Sandals Miss Tanzania 2005 na mshindi wa tuzo ya Miss Photogenic katika mashindano hayo ya urembo, akafuatwa na Jokate Mwegelo ambaye alikuwa mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, akafutwa na Victoria Martin ambaye alikuwa mshindi wa nne wa Miss Tanzania 2007, na mwaka uliofuata alieshikilia taji hili la Redds alikuwa Angela Lubala ambaye alikuwa Mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2008.

SIFA ZA BALOZI WA MITINDO WA REDD’S PREMIUM COLD

(i) Haiba: mchangamfu, mwenye ucheshi na mvuto.
(ii) Uwezo wa kutumia lugha za kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha na ushawishi.
(iii) Mwepesi wa kuelewa, mwenye uwezo wa kufikiria, kuchambua na kuelewa mambo.
(iv) Utulivu na kujiaminibila jazba.
(v) Hekima, busara na tabia njema
(vi) Miondoko ya kimaonyesho ya mitindo ya nguo yenye kulenga kuonyesha ubora na uzuri wa nguo.
(vii) Ufahamu na uelewa wa mabo ya mitindo ya Tanzania nay a kitaifa.
(viii) Ufahamu na uelewa wa kinywaji cha REDD’S.
(ix) Photogenic: Awe na mvuto katika picha.
(x) Bashasha: Mchangamfu mwenye mlahaka na mkabala mwema.
(xi) Kauli ya futi kamba:

Urefu/Kimo: Walau 5’8

Kiuno: 26”-28”

Kifua: 32”-34”

Hips: 36”-37”

Aidha utaratibu na mchakato wa kuchagua Balozi wa REDD’S 2010 utakuwa ni ule ule kama ulivyokuwa hapo awali. Jopo la majaji watano litafanya uteuzi huo. Mmoja wa majaji hao atatoa LINO/Kamati ya Miss Tanzania. Jaji mmoja au zaidi atatoka Tanzania Breweries Limited. Majina ya majaji yatatangazwa baadae.

Zawadi atakayotunukiwa Balozi wa REDD’S wa Mitindo ni allowance ya tshs.250,000= ya kila mwezi ka kipindi kisichozidi miezi 12 au mpaka atakapoteuliwa balozi mpya iwapo atateuliwa kabla miezi hiyo haijatimia kwa sababu yeyote ile.

Vilevile balozi wa REDD’S na TBL kwa ujumla hivyo atawezeshwa kupata kipato zaidi.

Mshindi wa tuzo ya Balozi wa REDD’S atatangazwa siku ya fainali za Miss Tanzania 2010.

ZITTO KABWE/CHADEMA IS ASKINGFOR YOUR CONTRIBUTION!


Dear Friends,
I would like to express my heartfelt gratitude for all your support.

Today we mark the start of a new journey

This morning I submitted my nominations forms for re-election for the Kigoma North parliamentary seat ready to serve again the people of Kigoma North and my country TANZANIA.

In order to make it happen am humbly asking for your support; if you would like to see Zitto back in Parliament and serving our nation I ask for your support.

I am ready to serve you once again.

DONATE:
Help Zitto keep fighting for our future and our country. Join the campaign by making a donation today. Your contribution and support will help us in our campaign.

To donate, please: Make a Deposit to Our Campaign Account:

NAME: ZITTO KABWE ZUBERI
BANK: CRDB BANK
ACCOUNT NUMBER: 01J2082022500

Contact Details:
Contact Person: Mhonga Ruhwanya
Mobile Number: +255 0758 000 111
E-mail Address: zitto2010@gmail.com

Find me on: facebook.com/zittokabwe or twitter.com/zittokabwe or youtube.com/zittokabwe or flickr.com/photos/zittokabwe and on my blog: zittokabwe.wordpress.com

credit source: http://www.wavuti.com/4/post/2010/08/contribute-to-zitto-kabwechademas-campaign.html#ixzz0x73kon1G

Wanawake washindana kuonyeshana bikini kwenye ‘kitchen party’


Mambo ya kuonyesha bikini yalivyokuwa: kila mtu kivyake.
Na Dunstan Shekidele, Morogoro
MIJIMAMA na wasichana kadhaa hivi karibuni “walizishusha heshima zao” kwa muda na kushindana kufanya mambo ya ajabu ikiwa pamoja na kuonyesha nguo zao za ndani (bikini) kwenye sherehe ya kumfunda bibi harusi mteule (kitchen party) iliyofanyika katika ukumbi wa Hedema maeneo ya Msamvu mjini Morogoro.

Baadhi ya watu waliokuwa hapo walionekana kuchefuliwa na vitendo hivyo ambapo baadhi ya waliovifanya ni wake za watu

Thursday, August 19, 2010

daya ya kibaka


dawa ya kibaka ni kumniga kama hivI

MAMBO YA UPAKO

ACCOMPLICE IN MURDER



Hali ya kusikitisha pale kwa Michuzi Jr. Watu kadhaa wamesimama kwa amani wakiangalia binaadamu mwingine akiuwawa kwa kuchomwa moto. Kwa namna moja au nyengine wale waliosimama wanaweza kuchukuliwa kama ni washiriki katika mauaji. Hawakuchukua hatua chanya katika tukio zima.

Polisi wako wapi?

JK Akabidhi Tamko La Kisheria


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Mwenza Dr. Mohamed Gharib Bilal wakisaini tamko la Kisheria linalothibitisha usahihi wa taarifa alizozitoa kwenye fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Jaji Mkuu Agostino Ramadhani akishuhudia.Tamko hilo lilisainiwa jana asubuhi na kukabidhiwa ofisini kwa Jaji Mkuu jijini Dar es Salaam.

JK Akabidhi Tamko La Kisheria


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Jaji Mkuu Agostino Ramadhani tamko la kisheria linalothibitisha usahihi wa taarifa alizotoa kwenye fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ofisini kwa Jaji mkuu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.Anayeshuhudia kulia ni mgombea mwenza Dr.Mohamed Gharib Bilal.

Aliyetaka kumuuza albino afungwa miaka 17


RAIA wa Kenya aliyeianza safari yake nchini mwao akifuatana na rafiki albino kwa kumrubuni kumtafutia kazi jijini Mwanza, lakini badala yake akataka kumuuza kwa Sh milioni 400, amehukumiwa kifungo cha miaka 17 jela.

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani hapa jana ilimhukumu Nathan Mtei (28) kifungo hicho na faini ya Sh milioni 80, baada ya kupatikana na hatia ya kumsafirisha na kumtorosha binadamu kwa lengo la kumuua.

Awali akimsomea maelezo ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Angelo Rumisha, Mwanasheria wa Serikali, David Kakwaya, alisema mshitakiwa alitenda makosa hayo Agosti 15 mwaka huu kwa kudhamiria kumuua Robinson Mtwana (20) raia mwenzake wa Kenya ambaye ni albino.

Baada ya mshitakiwa kusomewa maelezo, Kakwaya alisema kitendo cha kusafirisha binadamu ni kosa la kisheria hivyo kuiomba mahakama ifikirie adhabu dhidi ya mshitakiwa kwa kuwa makosa hayo yanadhalilisha utu wa binadamu.

“Vitendo vya kusafirisha binadamu kwa lengo la kumuuza vilikuwa vikifanyika enzi za biashara ya Utumwa, kwa kuwa vilikuwa vikidhalilisha utu wa binadamu … biashara hiyo ilizuiwa,” alisema Mwanasheria wa Serikali.

Aliongeza kuwa mwathirika wa tukio hilo ni mlemavu wa ngozi, watu ambao wamekuwa wakiandamwa nchini na matukio ya kuuawa na inaonesha wazi lengo la mshitakiwa lilikuwa ni kuua.

“Madhara ambayo yangetokea endapo mshitakiwa angetekeleza azma yake ni makubwa na yangesababisha mwathirika huyo kuuawa, hivyo tunaiomba Mahakama itoe adhabu kali dhidi ya mshitakiwa,ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye nia kama ya mshitakiwa,” alisisitiza Kakwaya.

Akisoma hukumu, Hakimu alisema tukio hilo limeleta picha mbaya kwa Tanzania, kwani imekuwa na matukio kama hayo.

Aliongeza kuwa adhabu aliyopewa mshitakiwa kwa kosa la kwanza atatumikia kwa miaka tisa jela au kulipa faini ya Sh milioni 80 na kwa kosa la pili atatumikia miaka minane.

Lakini kama atalipa faini adhabu zote zitatumika tofauti. Alibainisha kuwa adhbu hiyo imetolewa dhidi ya mshitakiwa ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye uroho na tamaa ya fedha kama aliyonayo mshitakiwa.

Kabla ya kutoa hukumu, Hakimu alimtaka mshitakiwa ajitetee.

Aliiomba Mahakama imsamehe au iruhusu kesi ikasikilizwe Kenya kwa kuwa anategemewa na familia yake.

Mshitakiwa aliongeza kuwa mganga wa kienyeji alichangia kutenda kosa hilo, kwani anahisi alimfanyia dawa hata kuingia tamaa.

Hata hivyo, Hakimu alisema mshitakiwa anaruhusiwa kukata rufaa Mahakama Kuu ndani ya siku 45 kuanzia jana, ikiwa hajaridhishwa na hukumu iliyotolewa dhidi yake.

Neno La Leo: Kuvua Au Kutokuvua? Ni Swali La Kizushi!


Jana jioni jamaa mmoja wa Idara ya intelijensia ( Tanzania) aliniuliza swali la ‘ kizushi’ ; “E bwana nataka kuifahamu Jiografia ya hapa, hivi wewe unakaa nyumba ‘A’ au’ B’? ” Aliniuliza. Jamaa huyu amekaa mahali hapo kwa miaka 20. Anafahamu kuwa nakaa nyumba ‘ B’ na kuna siku alinitambia kwa kuniambia alichosikia kwenye mazungumzo yangu ya simu wakati akipita nje ya nyumba ‘ B’ ninayoishi, yalikuwa mazungumzo ya kawaida tu. Iweje leo aniulize swali hili? Nilijiuliza. Kila swali lina tafsiri yake. Usikimbilie kujibu swali kabla hujalitafsiri. Jamaa yangu huyu alitakla kujua kati ya mawili yafuatayo; Mosi, kama nitajibu nakaa nyumba ‘ B’ nitamwambia nani anakaa nyumba ‘ A’. Huenda kuna mtu ameingia nyumba ‘ A’ lakini hajamjua ni nani. Pili; anamfahamu anayekaa nyumba ‘ A’ lakini anataka kujua kama namfahamu jirani yangu huyo. Jibu langu likawa; ” Mimi nakaa nyumba ‘ B’ na bila shaka unafamhamu anayekaa nyumba ‘ A’ , ni fulani. Hilo la mwisho nilimaanisha pia kuwa alimfahamu anayekaa nyumba ‘ B’. Naam. Kuvua au Kutokuvua, ni swali la kizushi. Na hasa kama anayeuliza swali tayari ameshashika mshipi na ndoano yenye chambo! Na hilo ni neno la leo.

POMBE SI CHAI YA MAZIWA!!!!


Mwanamke na mwanaume mmoja, mwishoni mwa wiki iliyopita 'walikata network' na lijikuta wakilala barabarani usiku kucha,baada ya kudaiwa kufakamia pombe za kienyeji katika klabu ya pombe hizo maeneo ya Mji Mpya mkoani hapa.

Watu hao ambao haijafahamika mara moja kama ni mke na mume,walikutwa na mwandishi wetu,jirani kabisa na kilabu hicho cha pombe za kienyeji wakiwa 'wamenoki' kwa kupoteza mawasiliano kiasi cha kudhaniwa wamekufa.

Daadhi ya majirani wanaoishi katika eneo hilo waliueleza mtandao huu kwamba jamaa walilala hapo usiku kucha, ambapo imedaiwa walizinduka saa mbili asubuhi baada ya kumwagiwa maji ya baridi na wasamaria wema! Pombe si......

Wednesday, August 18, 2010

PIKI PIKI ZA JAYDEE?????????

WARAKA WA MTOTO WA VITOTO KWA WASANII KUELEKEA UCHAGUZI


Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi october mwaka 2010,huu ni waraka wangu kwa wasanii wote wa mziki wa kibongo!. Najua kuna miaka mingi sana ya kuukomboa huu mziki wetu lakini wazungu wanasema "One step at a time"...na muda ndio huuu..........!!!!
Miaka kibaao sasa wasanii mmekuwa mkilalamika juu ya kudhulumiwa haki zenu kwa kuibiwa kazi zenu na kulipwa malipo madogo ya album zenu kiwango kisichokidhi mahitaji yenu,hilo ni sawa kabisaaa!!
LAKINI je!! mmejipanga vp kumaliza hili tatizo lenu? kila kukicha viongozi wanawa-ahidi kwa mdomo kuwa watamaliza tatizo lenu bila utekelezaji wa vitendo kitu ambacho mimi nakiona kama ni kiini macho na nyinyi wenyewe mnakifahamu....
Viongozi hawa hawa ambao wanakataa kwa "makusudi" kusimamia maslahi yenu ndio hao hao wanaokuwa wa kwanza kuwachukua nyinyi wakati wa uchaguzi ili muwasaidie kuwapigia kampeni kwa kutoa burudani pindi wanapokuwa kwenye mikutano yao,,,,
Sasa inakuwaje mnatumika kirahisi namna hii? wakati kwenye interview zenu wengi wenu mnajinadi kuwa nyinyi ni wanaharakati na sasa mnafanya mageuzi ya huu mziki wenu,vp mageuzi ndio haya? Mnapotumiwa kwenye kampeni mnacheka cheka kwa furaha pale mnapopewa laki kadhaa au vimilioni kama shukrani ya "kinafki" kutoka kwa hao watu waliowatumia!!!! Na baada ya kumaliza kampeni zao hao hao wakiwa madarakani wanawasahau na kujifanya hawawakumbuki tena hadi wakati mwingine wa uchaguzi.....(huu ni utumwa wa kifikra) najua mtasema mnaangalia pesa na ndio mana mnawafanyia kazi yao na sio kitu kingine!!! Sawa sikatai huenda ni kweli pesa ndio mnayofuata,,, sasa je? nyie wasanii wa kiume ikitokea wamama wakiwapa pesa za kutosha na kuwataka mkatumbuize kwenye "kitchen party" yao mtaenda kudhalilishwa sababu ya pesa au mtakataa?
Sidhani kama ntapata dhambi nikisema kuwa kitendo cha wasanii kutumiwa kwa muda na hawa watu mi nakifananisha na binti wa kike ambae bwana wake huwa anajifanya kumjali na kumfuata pale anapotaka penzi lake tu!! na akishamaliza shida zake anaondoka na kumuacha binti huyo akiteseka na hali ngumu ya maisha bila ya msaada wowote na hurudi tena pale anapokuwa na shida hiyo!!
Enyi wasanii kwanini mnajipa thamani ndogo kiasi hicho???
Huu ndio wakati wenu wasanii kuonesha mapinduzi yenu na misimamo yenu na zile harakati ambazo kila kukicha mmekuwa mkizitaja kwenye nyimbo zenu na interview zenu,,,yawapasa kudai maslahi yenu kwanza kuliko kutumika kuhangaikia maslahi ya watu wengine....
Sitoona ajabu nikiwaona wasanii wale wale wanaokuwa wa kwanza siku zote kudai haki zao wakitumika kwenye kampeni mwezi october na kisha baada ya uchaguzi mwakani wasanii hao hao tutawaskia tena wakilalamika kutokumbukwa na viongozi husika!!!
"CALCULATE THE RISK,BEFORE YOU JUMP"
By Mtoto wa vitoto..
(Ze' son of babiez)
2010...

Mtoto wa Kingunge adaiwa kutapeli Sh mil 424

MTOTO wa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, Tonny Mwiru amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu, Dar es Salaam, akikabiliwa na mashitaka ya kujipatia Sh milioni 424 kwa njia za udanganyifu.

Inspecta wa polisi, Emma Mkonyi, leo amesoma mashitaka yanayomkabili mtoto huyo wa Mbunge wa Kuteuliwa.

Katika shitaka la kwanza,mshitakiwa Mwiru, kwa kushirikiana na wenzake wasiofahamika, katika tarehe na mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam walikula njama ya kuiibia kampuni ya SCI (TZ) LTD kiasi hicho cha fedha.

Katika shitaka la pili, mshitakiwa alidaiwa kughushi fomu ya benki ya kuhamishia fedha yenye namba E17 ya Agosti 29, 2008.

Kwa mujibu wa Mkonyi, kijana huyo alighushi fomu hiyo kwa nia ya kuonesha kuwa ilikuwa halali na imesainiwa na Ravishankar Rasiman, Mkurugenzi wa kampuni hiyo huku akifahamu si kweli.

Shitaka la tatu, amedaiwa mahakamani kuwa, Agosti 29, 2008, katika benki ya Barclays katika Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam aliwasilisha fomu hiyo kwa mfanyakazi wa benki hiyo,Bituni Chiza,huku akifahamu kuwa haikuwa halali.

Imedaiwa pia kuwa,kati ya Septemba na Octoba 2008 katika benki ya CRDB tawi la Kijitonyama, Dar es Salaam mshitakiwa alijipatia Sh 424,458,799.29 kutoka katika akaunti namba 01j014293000 akionyesha kuwa fedha hizo ni halali zimetolewa na kampuni ya SCI (TZ) LMD kwenda kwenye kampuni ya Temm Power Solution.

Mshitakiwa huyo amerudishwa rumande baada ya kukana mashitaka yote na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili.

Mwiru pia alitakiwa atoe Sh milioni 10 pamoja na hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.Kesi hiyo itatajwa Agosti 31 mwaka huu.

Hakimu Mkazi, Gabriel Mirumbe, alimuuliza kama Tonny ni mtoto wa Kingunge Ngombale Mwiru,akajibu kuwa Kingunge ni baba yake mzazi.

"Konfyushen" inayowapata waathirika Kura za Maoni

Tuesday, August 17, 2010

KIBAKA ALA KICHAPO ASUBUHI KWEUPE!


KIBAKA MMOJA AMBAYE JINA LAKE HALIKUPATIKANA MARA MOJA AKIWA AMEPOTEZA FAHAMU KUTOKANA NA KUPEWA KICHAPO CHA KUFA MTU BAADA YA KUMWIBIA MMOJA WA ABIRIA ALIYEKUWA NDANI YA GARI AKIWA AMETOKEA ENEO LA TANDIKA AKIELEKEA MWENGE, KIBAKA HUYO ALIMPORA ABIRIA HUYO SIMU KUPITIA DIRISHANI NDANI YA DARADARA HIVYO WANANCHI WENYE HASIRA WALIMKIMBILIA WAKAMKAMATA NA KUMPA KICHAPO CHA MAWE, ENEO LA KARUME SOKONI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM, AMBAPO TUKIO HILO LIMETOKEA JANA SAA NNE ASUBUHI
KIBAKA AKIWA HAJITAMBUI KWA KIPIGO ALICHOKIPATA KUTOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA.

Monday, August 16, 2010

Utafiti global publishers!


Mwandishi Wetu na Mashirika ya Habari
Utafiti wa kisayansi uliofanywa hivi karibuni nchini Marekani na Uingereza kisha kuripotiwa na Jarida la New Study umebainisha kwamba, wanawake wenye matiti makubwa huwasisimua zaidi wanaume kimapenzi kuliko wengine.

Jane Pincott Mwandishi wa masuala ya sayansi amekiri katika kitabu chake cha ‘Do Gentleman Really Prefer Brondes’ kwa kueleza kinagaubaga juu ya utafiti huo kuwa , nguvu ya mvuto wa wanawake wa aina hiyo ni kubwa na kufafanua kwamba ina uwezo mara dufu wa kuteka hisia za wanaume.

“Hakuna mwenye kupinga kuhusu hili, dunia nzima inafahamu na hasa wanaume wenyewe…kigezo cha kwanza cha kumtambua mwanamke ni matiti, …kadiri yanavyokuwa makubwa utambulisho wake hukua na mvuto huongezeka.

“Mwanamke kuwa na sura nzuri peke yake haitoshi…ingawa wanaume hupenda hilo pia, lakini si jambo linaloamsha hisia zao za mapenzi haraka, tumetafiti na kubaini ukweli huu tunaoueleza,” alisema Pincott alipozungumza na New Study.

Timu ya wataalamu iliyoendesha utafiti huo, ilihusisha zaidi ya wanaume 4,000, kwa kuwaweka kwenye chumba chenye picha za wanawake wenye matiti makubwa na madogo, ambapo ilibainika asilimia 79 ya waliotazama picha za wanawake wenye matiti makubwa walisisimka kimapenzi.

Naye Dk. Grazyna Jasienska wa Chuo cha Harvard aliongezea nyama kwenye uchunguzi huo kwa kusema kuwa, mwanamke mwenye matiti makubwa ana uwezo wa kushika ujauzito haraka kuliko aliyenayo madogo.

Ripoti hiyo ya watafiti wa nje inaweza kuwa na ukweli hata kwa wanawake wa kibongo ambao nyakati hizi wamekuwa wakiacha nje sehemu kubwa ya matiti yao makubwa, bila kubainisha sababu wazi za kufanya hivyo.

“Nakubaliana kwa kiasi fulani na utafiti huo kwa sababu za kitaalamu, matiti ni kiungo nyeti chenye hisia za mapenzi, kinapoonekana kwa wazi huvutia, hii haijalishi kama ni matiti ni makubwa au madogo.

“Lakini kwa kuwa matiti makubwa huonekana kirahisi mwanamke anapokuwa amevaa nguo, hiyo inaweza kuwa sababu ya wenye matiti hayo kuvutia,” alisema Richard Manyota mwanasaikolojia mahiri nchini.

Warembo wa kibongo wenye matiti makubwa ambao wamekuwa na tabia ya kuyaweka wazi bila kueleza kama wanatumikia utafiti huu ama la ni pamoja na Aisha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ (pichani), Aunt Ezekiel, Moureen Gislary, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Fideline Iranga, Rehema Chalamila ‘Ray C’ na wengineo.

WACHINAAAAAAAAAAAAAAAA!

Ufafanuzi kuhusu Mwakalebela vs Mramba na Chenge




Baada ya jina la Frederick Mwakalebela kuenguliwa katika orodha ya wagombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, baadhi ya watu wamekuwa wakihoji uhalali wa kufanya hivyo il hali wana-CCM wengine wanaogombea viti hivyo katika majimbo mengine nchini wana kesi mahakamani lakini wameruhusiwa kuendelea na kinyang'anyiro hicho. Maswali hayo yaliifikia CCM na hapa ni ufafanuzi wake:Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC-CCM), John Chiligati amesema kesi inayomkabili mshindi wa kura za maoni aliyepokwa ‘haki’ ya kuteuliwa kugombea ubunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Frederick Mwakalebela, haifanani na washindi wengine wa kura za maoni walioteuliwa ambao ni Basil Mramba anayegombea jimbo la Rombo na Andrew Chenge anayegombea jimbo la Bariadi Mashariki licha ya kuwa na kesi mahakamani kama yeye.

Alisema, Mwakalebela ameachwa kwa sababu kukosa kwake maadili.

“Suala kwa Mwakalebela ni maadili tu, katika mchakato huu, kakamatwa kwa tuhuma za rushwa na TAKUKURU wamesema wanayo sababu ya kumpeleka mahakamani." “Lakini alikuwa ndio kwanza kaingia katika mchezo wenyewe na katika mchezo huu huu kabla ya dakika 90, akapigiwa filimbi kuwa amecheza faulo,” alisema Chiligati.

Kuhusu tofauti ya Mramba, Chenge na Mwakalebela Chiligati alisema, “ kisheria wote ni watuhumiwa na hawakutwa na hatia, lakini kimaadili ni tofauti… Mramba anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka, tuliita wanasheria wakasema hiyo kesi haimuondolei sifa ya kuwa mgombea.”

Hata hivyo alikiri kuwa Mramba alipitishwa baada ya kufanyika mjadala kati ya wajumbe hao wa NEC.
“Katika Mkoa wa Shinyanga Jimbo la Bariadi Mashariki aliteuliwa Chenge kutetea nafasi yake, anayo kesi ya trafiki, haimkoseshi haki ya kuwa mgombea,” alisema Chiligati.

Shoo Love kwa umpendae bwana!