Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, August 20, 2010

Wafanyakazi: Tutampigia kura Jakaya Kikwete


Rais Jakaya Kikwete

Wakati Shirikisho la Vyama vya Wanyakazi nchini (TUCTA) likidaiwa linajipanga kutoa tamko la kuwataka wafanyakazi wote nchini kutompigia kura Rais Jakaya Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu 2010, inaonekana mambo ni kinyume.

Sehemu kubwa ya wafanyakazi wanaeleza kufurahishwa na utawala wa JK, hivyo kuwa tayari kumuongezea kipindi kingine cha uongozi cha miaka mitano (2010-2015).

Wafanyakazi waliozungumza na gazeti hili kwa wiki nzima iliyopita, Dar es Salaam, walieleza kufurahishwa na kazi ya JK aliyoifanya Ikulu kwa miaka mitano, hivyo wanaamini ataendeleza mazuri endapo ataongezewa kipindi kingine.

Walisema kuwa Rais Kikwete ameweza kuonesha moyo mzuri kwa kuongeza mishahara ya wafanyakazi mara kwa mara pia kukabiliana na ufisadi, hivyo hawaoni sababu ya kuliunga mkono TUCTA endapo litasema JK asipigiwe kura.
Baadhi ya maoni ya wafanyakazi kama walivyozungumza ni kama ifuatavyo;

ITUS BILLA
Mfanyakazi wa Kampuni ya Big Bell.
Anasema: “Nafurahia kipindi chote cha Kikwete kuwepo madarakani, maana mengi aliyoahidi ametekeleza. Nawashauri Watanzania wenzangu tumuongezee kipindi kingine aweze kuleta maendeleo zaidi. Kuhusu nyongeza ya mshahara mimi naona maisha yatakuwa yale yale kwani kila mshahara ukitangazwa kupanda na bidhaa nazo zinapandishwa.”

SULEIMAN MAZINGE
Anasema: “Utawala wa Rais Jakaya Kikwete ni mzuri kwani nchi ina amani na hakuna njaa wala migogoro na hilo ndilo jambo kubwa, mambo mengine ni majaaliwa. Kuhusu ongezeko la mishahara hapo hakutakuwa na jipya kwani uzoefu unaonesha mishahara ikipanda na huduma nazo zinapanda.”

ANNA LUWENA
Anasema: “Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri na anaomba uendelee ingawa hauna tofauti kubwa na tawala zingine zilizopita. Kuhusu kupanda kwa mishahara ni bora ingebaki palepale kwani ongezeko la mishahara litasababisha kuongezeka maradufu kwa gharama za huduma mbalimbali.”

HUSSEIN MAKUBI
Anasema: “Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri kwani ameendeleza mazuri yaliyoachwa na marais waliopita. Kuhusu mishahara mwanzoni wananchi watafurahia ongezeko hilo lakini siku zinavyokwenda huduma nazo taratibu zitapanda na kufanya hali kuwa ile ile.”

BABY OMARY
Anasema: “Utawala wa Rais Kikwete ni mzuri hakuna dosari kubwa iliyojionesha ukilinganisha na tawala zilizopita.
Ongezeko la mishahara linatokana na kusonga kwa dunia lakini halina uhusiano wowote na ubora wa maisha kwani hapo zamani mfanyakazi alilipwa 6000/ (elfu sita) mfanyakazi huyo sasa hivi analipwa 600,000/ (laki sita) lakini maisha yake ni yaleyale afadhali ya zamani.

HADIJA HASSAN
Mfanyakazi wa Kampuni ya Vodacom anasema: “Utawala wa Rais JK ni mzuri na hasa kwa kuwa ametoa ajira kama alivyoahidi, hivyo kuwakomboa Watanzania. Ongezeko la mishahara anasema litakuwa na mafanikio kwa wenye malengo lakini wasio na malengo wataendelea kuumia.”

GHONCHE MATEREGO
Katibu Mtendaji wa BASATA, anasema: “Rais Kikwete uongozi wake ni mzuri sana pia ni mtu anayeona mbele zaidi ndiyo maana anawapa vijana kipaumbele tena anapenda kuwarithisha ili baadaye wawe viongozi wanaofaa kuongoza nchi. Amekuwa ni mchango mkubwa sana kwa vijana, lakini hajawaacha wazee anawataka kuelimisha vijana wao ili waweze kujikwamua kimaisha.

“Kwa upande wa mshahara kuongezwa hilo nalo ni jambo la heri na serikali imetimiza ahadi yake kwani kilikuwa ni kilio cha siku nyingi na sasa imefikia mahali na kuongeza tunashukuru kwa kutimiza ahadi hiyo.”

MBAZI OMBENI
Karani wa BASATA, anasema: “Utawala wa Rais Kikwete siyo mbaya sana lakini kuna ahadi ambazo naomba kama akichaguliwa tena awamu ya pili azitekeleze. Shule za Kata zimejengwa nyingi lakini vitendea bado tatizo, naomba aliangalie hilo pamoja na mfumuko wa bidhaa sokoni.
“Suala la mishahara kuongezwa nashuru kwa sababu kilikuwa kilio chetu cha siku nyingi.”

No comments:

Post a Comment