Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, August 23, 2010

NEWS TOKA JIACHIEBLOGSOT......suala la kujichukulia sheria mkononi litakoma lini ndani ya jamii yetu.


Mtu aliyeniletea picha hii alisema huu si ustaarabu hata kidogo na mimi nakubaliana naye. Aliyeleta taarifa hii aliniletea jumla ya picha kumi za mtu anayechomwa moto kwa kutuhimiwa wizi wa pikipiki.Zipo za karibu na nyingine ambazo hazitamaniki hii ina nafuu nimeibadika kuwasilisha ombi la mleta habari.Alisema kwamba polisi wa Kimara walifika eneo hilo muda mfupi kabla hajachomwa moto wakajiondokea ambapo wangeliweza kuokoa maisha ya mtuhumiwa huyu.Watu wamechukua sheria mkononi wameua na kumchoma moto mtu ambaye hana makosa kwa kudhani kwamba ameiba pikipiki wakati alikuwa ametumwa mafuta na fundi ambaye alikuwa anatengeneza pikipiki hiyo.

Tukio hili la kusikitisha limetokea Jumamosi wiki hii na mbaya zaidi nimeibandika kwenu japo haipendezi kuweka lalamiko la msomaji kwamba polisi hawakujitahidi kuzuia mauaji haya.Picha na Rahabu/Kimara

Blog ya Jiachie inalaani na itazidi kulaani vikali vitendo ya namna hii vya kujichukulia sheria mkononi,ambavyo vimekuwa vikiibuka mara kwa mara ndani ya jamii yetu na kusababisha kupoteza uhai wa watu,Wanajamii tuachane na tabia hii ya kujichukulia sheria mkononi,Sheria zipo kwa ajili ya kulinda na kutetea haki ya kila mwanajamii,basi na itumike njia hiyo ya kufuata sheria.
Asante,nawakilisha.

1 comment:

  1. kweli charia ishike mkono wake maana tunako elekea haijulikani ni wapi! kweli binanamu unamchoma binadamu mwenzako kama mnyama!! Tumridie Mungu jaman

    ReplyDelete