Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, August 16, 2010

Ufafanuzi kuhusu Mwakalebela vs Mramba na Chenge
Baada ya jina la Frederick Mwakalebela kuenguliwa katika orodha ya wagombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, baadhi ya watu wamekuwa wakihoji uhalali wa kufanya hivyo il hali wana-CCM wengine wanaogombea viti hivyo katika majimbo mengine nchini wana kesi mahakamani lakini wameruhusiwa kuendelea na kinyang'anyiro hicho. Maswali hayo yaliifikia CCM na hapa ni ufafanuzi wake:Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC-CCM), John Chiligati amesema kesi inayomkabili mshindi wa kura za maoni aliyepokwa ‘haki’ ya kuteuliwa kugombea ubunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Frederick Mwakalebela, haifanani na washindi wengine wa kura za maoni walioteuliwa ambao ni Basil Mramba anayegombea jimbo la Rombo na Andrew Chenge anayegombea jimbo la Bariadi Mashariki licha ya kuwa na kesi mahakamani kama yeye.

Alisema, Mwakalebela ameachwa kwa sababu kukosa kwake maadili.

“Suala kwa Mwakalebela ni maadili tu, katika mchakato huu, kakamatwa kwa tuhuma za rushwa na TAKUKURU wamesema wanayo sababu ya kumpeleka mahakamani." “Lakini alikuwa ndio kwanza kaingia katika mchezo wenyewe na katika mchezo huu huu kabla ya dakika 90, akapigiwa filimbi kuwa amecheza faulo,” alisema Chiligati.

Kuhusu tofauti ya Mramba, Chenge na Mwakalebela Chiligati alisema, “ kisheria wote ni watuhumiwa na hawakutwa na hatia, lakini kimaadili ni tofauti… Mramba anatuhumiwa kutumia vibaya madaraka, tuliita wanasheria wakasema hiyo kesi haimuondolei sifa ya kuwa mgombea.”

Hata hivyo alikiri kuwa Mramba alipitishwa baada ya kufanyika mjadala kati ya wajumbe hao wa NEC.
“Katika Mkoa wa Shinyanga Jimbo la Bariadi Mashariki aliteuliwa Chenge kutetea nafasi yake, anayo kesi ya trafiki, haimkoseshi haki ya kuwa mgombea,” alisema Chiligati.

No comments:

Post a Comment