Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, August 20, 2010

Redd's yaanza mchakato wa kumpata balozi wake



Meneja wa bia ya Redd's,Dada Kabula Nshimo (kati) akifafanua jambo mbele ya warembo washiriki wa Miss Tanzania 2010.wengine ni Dada Edith (shoto) na Victoria



Baadhi ya Warembo watakaoshiriki kinyang'anyiro cha Miss Tanzania 2010 wakisikiliza kwa makini




utulivu na usikivu ulitawaka wakati Da Kabula akiongea





Warembo washiriki wa Miss Tanzania 2010 wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa bia ya Redd's mara baada ya mkutano wa kumsaka balozi wa Redd's kumalizika leo katika hotel ya Gerrafe,mbezi beach

Tuzo ya Balozi wa Mitindo wa REDD’S ilianza kwa mara ya kwanza mwaka 2005 ambapo ndio mwaka wa kwanza kwa REDD'S kudhamini Miss Tanzania. Na alieleza kushikilia taji hilo alikuwa ni Natalia Noel Yatera ambaye pia alikuwa mshindi wa pili wa Ocean Sandals Miss Tanzania 2005 na mshindi wa tuzo ya Miss Photogenic katika mashindano hayo ya urembo, akafuatwa na Jokate Mwegelo ambaye alikuwa mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2006, akafutwa na Victoria Martin ambaye alikuwa mshindi wa nne wa Miss Tanzania 2007, na mwaka uliofuata alieshikilia taji hili la Redds alikuwa Angela Lubala ambaye alikuwa Mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2008.

SIFA ZA BALOZI WA MITINDO WA REDD’S PREMIUM COLD

(i) Haiba: mchangamfu, mwenye ucheshi na mvuto.
(ii) Uwezo wa kutumia lugha za kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha na ushawishi.
(iii) Mwepesi wa kuelewa, mwenye uwezo wa kufikiria, kuchambua na kuelewa mambo.
(iv) Utulivu na kujiaminibila jazba.
(v) Hekima, busara na tabia njema
(vi) Miondoko ya kimaonyesho ya mitindo ya nguo yenye kulenga kuonyesha ubora na uzuri wa nguo.
(vii) Ufahamu na uelewa wa mabo ya mitindo ya Tanzania nay a kitaifa.
(viii) Ufahamu na uelewa wa kinywaji cha REDD’S.
(ix) Photogenic: Awe na mvuto katika picha.
(x) Bashasha: Mchangamfu mwenye mlahaka na mkabala mwema.
(xi) Kauli ya futi kamba:

Urefu/Kimo: Walau 5’8

Kiuno: 26”-28”

Kifua: 32”-34”

Hips: 36”-37”

Aidha utaratibu na mchakato wa kuchagua Balozi wa REDD’S 2010 utakuwa ni ule ule kama ulivyokuwa hapo awali. Jopo la majaji watano litafanya uteuzi huo. Mmoja wa majaji hao atatoa LINO/Kamati ya Miss Tanzania. Jaji mmoja au zaidi atatoka Tanzania Breweries Limited. Majina ya majaji yatatangazwa baadae.

Zawadi atakayotunukiwa Balozi wa REDD’S wa Mitindo ni allowance ya tshs.250,000= ya kila mwezi ka kipindi kisichozidi miezi 12 au mpaka atakapoteuliwa balozi mpya iwapo atateuliwa kabla miezi hiyo haijatimia kwa sababu yeyote ile.

Vilevile balozi wa REDD’S na TBL kwa ujumla hivyo atawezeshwa kupata kipato zaidi.

Mshindi wa tuzo ya Balozi wa REDD’S atatangazwa siku ya fainali za Miss Tanzania 2010.

No comments:

Post a Comment